BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza leo Oktoba 12, 2022 jijini Dar es Salaam Waziri wa Niashati, January Makamba amesema, “Kupika ni moja ya tukio pekee linalounganisha watu wa hali zote kuanzia wa juu, kati na chini, lakini Watanzania wengi hawajui na wala hawahoji aina ya nishati inayotumika katika kupika vyakula wanavyokula kila siku.
Makamba amesema 72% ya nishati yote inayozalishwa nchini Tanzania inatumika majumbani na uchafuzi wa mazingira hasa hewa kwa njia moshi unachangiwa na 89.7% ya Nishati yote inayotumika majumbani.
Amefafanua kuwa 63.5% ya kaya nchini zinatumia Kuni kupikia, 26.2% hutumia Mkaa, 5.1% ya kaya zinatumia Gesi za Mitungi, 3% Umeme na 2.2% ikiwa ni nishati nyingine.
Waziri Makamba amesema hayo kwenye mkutano wa kuandaa Kongamano la Nishati Safi Ya Kupikia ‘Clean Cooking Conference’ ili kuchunguza vikwazo vinayodumaza matumizi ya nishati za kisasa za kupikia. Kongamano hilo linalenga kupendekeza mikakati ya kufanikisha upatikanaji wa nishati safi, za bei nafuu na endelevu nchini Tanzania.
Litafanyika Novemba 1 na 2 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha watunga sera, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wawekezaji, wafadhili, wanataaluma na wananchi kwa ujumla.
Siku ya ufunguzi wa kongamano itahudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa Mgeni Rasmi. “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa Kongamano la Nishati safi ya Kupikia yaani ‘Clean Cooking Conference’ ili kuchunguza vikwazo vinavyodumaza matumizi ya nishati za kisasa za kupikia”- amesema Waziri Makamba