Makamba: Gesi ya Mtwara kuanza kuchimbwa 2025

Makamba: Gesi ya Mtwara kuanza kuchimbwa 2025

Wait a minute [emoji848][emoji848][emoji848] Mmmhhh okay.

Mkataba unasemaje? Sisi kama nchi tunapata % ngapi? So gharama tu ya uchimbaji ni tril 70? Eti? Gharama hizi kubwa mno wamezipataje kabla hata mradi haujamalizika? Yaani deni la Taifa tokea uhuru hadi sasa ni Tril 78. Sasa gharama za uchimbaji gesi hata pamoja na kujenga LNG plant zote ni tril 70? Hizi gharama kubwa sanaaa, something haiko sawa.

Jamani, nawaza tu, usikute waka zidisha gharama sana tukaanza kupigwa mapemaaaaaa. Nawaza tu, uuwiii, OMG.

Sasa kaka Kama wasilozidiwa gharama ili wapate faida,Watapataje faida?
Sababu gharama zikiwa juu wakikupa ina maana huwezi kumtiza kodi wakati hapati faida.
Kwanza wewe kama Mtanzania Huna Uzoefu wa miradi kama hiyo na mikataba...Lazima Upigwe tuu hakuna Namna wala huruma.
Sasa mkuu ulitakaje sasa...Mradi usianze ili tukose hela?
Au wewe ulitakaje sasa???[emoji851][emoji851]
Tumechelewa sana ujue[emoji30]
Kuna faida nyingi za Kuanza kuliko kuendelea kuchelewa.
Hebu Nipe Sababu kwanini Mradi Usianze?
Cc: Chige
 
Pamoja na mapungufu yake jiwe ila ungese huu alikua hakubaliani nao kabisa.
Gesi ya mwanzo ilivyoanza kuchimbwa wananchi waliahidiwa faida kibao watazozipata kutokana na hio gesi ikiwa ni pamoja na punguzo la gharama za umeme.
 
Ungese upi Kiongozi?

Tatizo watu mnachanganya sana madesa...

Kwanza, ukisema "gesi ya mwanzo" ina maana ni ile ya Songosongo na Msimbati ambayo iligundulika tangu enzi za Nyerere, na hii ni ONLY 7.5 Trillion Cubic Feet, wakati gesi iliyogunduliwa wakati wa JK ni 47 Trillion Cubic Feet, na haijachimbwa wala tone!!

Sasa gesi ya mwanzo ipi?

Na wengi wenu kwavile mlimuamini sana JPM basi mlikuwa mnaamini kila kinachosemwa. Kwa mfano, watu waliaminishwa enzi za JK kulikuwa na mgao wa kutisha kwa sababu watu walikuwa wanaziba maji lakini alipoingia JPM, akawatia adabu waziba maji, na hatimae umeme ukaanza kuwa bwelele!!!

Hizo zilikuwa ni siasa tu, kwa sababu hadi sasa, umeme tunaotegemea zaidi ni wa gesi ambao ni 57% wakati ule wa maji ni ONLY 37%!

Sasa pamoja na wengi kukejeli wanaopigia debe gesi lakini ukweli ni kwamba tunategemea zaidi umeme wa gesi kuliko wa maji! Na huo umeme wa gesi unatokana na gesi ya Songosongo na Mnazi Bay peke yake ambayo kama nilivyosema, it's 7.5 TRillion Cubic Feet wakati kuna gesi nyingi zaidi imekaa tu baharini!!!

Haya sasa... huyo JPM alidanganya watu kwamba gesi YOTE imeuzwa, sasa huo mkataba wa Trillion 70 ni kwa gesi ipi wakati gesi ilishauzwa?! Tumeambiwa sana kuhusu mafisadi kwenye gesi... JPM kabla hajatangulia mbele za haki, ametawala kwa miaka 5!!

Je, ulishawahi kusikia hao mafisadi wakipelekwa mahakamani?! Unawaacha vipi watu waliouza GESI YOTE kwa Mchina? Na hakuwahi kumtumbua James Mataragio kwa tuhuma hizo hizo za ufisadi kwenye gesi? Sasa ikawaje akamrudisha tena pale TPDC?

Man, hamtaki tu kukubali lakini ukweli ni kwamba, MMEDANGANYWA mambo mengi sana huku watu waki-take advantage ya Watanzania kutpfuatilia mambo!!

Na utakapojua Watanzania sio wafuatiliaji wa mambo, ni hili suala la Trillion 70!

Wengi wanadhani hiyo Trillion 70 ni mradi ulioanza wakati wa Makamba na Wapigaji wenzake wakati ni mradi wa tangu 2015, na hata Kalemani wakati wa Magufuli, alihusika moja kwa moja kwenye majadiliano!! Sasa kwavile JPM alionesha gesi kutokuwa priority kwake, ndo mradi ukawa unasuasua!!

And on top of that, hiyo Trillion 70 sio ya UCHIMBAJI GESI bali ya ujenzi wa kiwanda cha KUCHAKATA GESI!

Narudia, wakati mkiendelea kushangilia Wapiga Porojo Wanaopinga Gesi, ukweli ni kwamba 57% ya umeme wetu unatokana na gesi! Na 57% hiyo unatokana na ONLY 7.5 TCF of gas wakati tuna 57.5 TCF of gas, na zaidi ya 47 TCF hazijachimbwa hata tone!!

Sasa jiulizeni tu, ikiwa 7.5TCF of gas zinatutapatia 57% ya umeme wetu... je, tungeweza kuchumba angalau 20 TCF? Oh! Nilisahau... hatuwezi kuchimba hizo 20TCF kwa sababu Gesi Yote Ameuziwa Mchina.... na Watanzania mkiambiwa hivyo, "mnapiga makofi"
 
Bila shaka taarifa inamaanisha uchimbaji na uchakataji, kwamba kutakuwa na plant ya LNG onshore

Kwa sababu kama ni uchimbaji tu, si unafanyika offshore na gesi inasafirishwa kuja Dar kwa bomba ya TPDC na lile la Pan African (Songosongo) kwa matumizi ya kufua umeme na nyumbani (kwa nyumba chache sanaaaaa)
Hiyo 70 Trillion is ONLY for Gas Processing Plant ambayo itajengwa pale Lindi!!

Kama ulivyosema, uchimbaji unafanyika offshore... several kilometers away from the shore! Ikishachimbwa huko offshore, inasafirishwa in raw form na ma-impurity yake hadi nchi kavu kwenye hiyo plant ya 70 Trillion!!

Pesa ni ndefu sana kwa sababu...

1. Serikali ilikataa kujenga kiwanda baharini
2. Vitalu vipo zaidi ya 100km from nchi kavu
3. Gesi yenyewe nayo ipo kwenye kina kirefu... hapa tunazungumzia kilometers!!

Sasa kutandaza mabomba umbali wote huo, hadi nchi kavu kwenye processing plant, anyway, inawezekana ni kweli tunapigwa lakini sio kazi nyepesi! Hii ni tofauti na gesi kama ile ya Mkambakofi ambayo ipo nchi kavu, au hata ile ya Songosongo!!

Kwamba kusambaza kwenye nyumba chache sana... uchache utatokana na ama sisi wenyewe kushindwa kusambaza miundombinu kwa watu wengi zaidi, au kama priority yetu itakuwa kwenye export ingawaje ukisoma Sheria ya 2015 kuhusu Matumizi ya Fedha za Mafuta na Gas, inasema priority ya kwanza iwe for domestic use, na ziada ndipo isafirishwe!!

Ni kutokana na hilo ndo maana TPDC walitangaza tenda ya kusambaza miundombinu ya gesi nchi mzima, na kwahiyo inawezekana kabisa kuwafikia wananchi wengi kwa sababu, as of now, kuna roughly 47 Trillion Cubic Feet of gas ambazo hazijaguswa kabisa!!
 
Sasa kaka Kama wasilozidiwa gharama ili wapate faida,Watapataje faida?
Sababu gharama zikiwa juu wakikupa ina maana huwezi kumtiza kodi wakati hapati faida.
Kwanza wewe kama Mtanzania Huna Uzoefu wa miradi kama hiyo na mikataba...Lazima Upigwe tuu hakuna Namna wala huruma.
Sasa mkuu ulitakaje sasa...Mradi usianze ili tukose hela?
Au wewe ulitakaje sasa???[emoji851][emoji851]
Tumechelewa sana ujue[emoji30]
Kuna faida nyingi za Kuanza kuliko kuendelea kuchelewa.
Hebu Nipe Sababu kwanini Mradi Usianze?
Cc: Chige
Hakuna atakayekupa sababu ya kwanini mradi usianze...

Kwanza kabisa, wengi wanachanganya madesa... wanashindwa kutofautisha kati ya Gas ya Songosongo & Msimbati kwa upande mmoja, na ile inayojengewa kiwanda cha Trillion 70 kwa upande mwingine!!

Kingine, wengi walimezeshwa sana propaganda kuhusu huu mradi!! Ambacho hawafahamu, waliyemwamini alikuwa anawadanganywa!! Inawezekana alikuwa anawadanganya kwa sababu nae alikuwa anadanganywa na watu wa karibu au alikuwa anawadanganya kwa sababu tu hakuwa na interest na gas industry!!

Ni hawa hawa ndio walikuwa wanadanganywa kwamba unaweza kujenga mtambo wa kuchenje makinikia kirahisi tu lakini hadi Shujaa anatangulia mbele za haki, huo mtambo haukujengwa!!

Sie wengine tuliposema wazi kujenga Copper Smelters kwa lengo la kuondoa copper ili ubaki na dhahabu sio jambo jepesi kiasi hicho, wale wale wakatukejeli sana hapa JF kwamba sisi ni Vibaraka wa Mafisadi, lakini hadi leo, mtambo HUJAJENGWA!
 
Chige tatizo wananchi tunalalamika kwa upande wetu hatuoni unafuu wowote baada ya hio gesi kuzalishwa.
Mfano kipindi kile cha mchakato wa uchimbaji msimbati, tulipewa ahadi kemkem na waziri wa nishati kipindi kile prefesa Muhongo, alitukokotelea mpaka gharama ya unit moja ya umeme tutanunua chini ya shilingi 100, ila baada ya mradi maisha yanabaki vilevile,
Mfano wa pili kabla ya mradi wa gesi huko Mtwara tulikua tunanunua gesi ya kupikia kwa bei nafuu na hio gesi yenyewe ilikua inatoka nje ya nchi, sasa baada ya kuzalisha gesi yetu wenyewe gharama inapanda baada ya kushuka, hali hii kwa sisi wananchi wa kawaida tunaona miradi hii mikubwa inayotumia pesa nyingi haina faida ni bora hizo pesa zikatumike katika miradi mingine yenye impact kubwa inayoonekana kwa wananchi.
Mfano Sukari, Cement n.k tunazonunua nje ya nchi bei yake ni ndogo sana ukilinganisha na bidhaa hizohizo zinazozalishwa hapa nchini, sasa hapa mwananchi wa kawaida anajiuliza kunafaida gani ya kuhangaika kufuga ng'ombe ili upate maziwa na nyama ikiwa utatumia gharama kuubwa kumhudumia tofauti na kununua maziwa na nyama yanayouzwa kwa bei ya chini?
 
Man,

Tofauti na watu wanavyodhani... Gesi ya Msimbati haikuanza kuchimbwa wakati wa JK bali tangu wakati wa Mkapa!!

Ambacho kilitokea, baada ya gesi kuchimbwa, Kampuni ya ARTMAS ikawa inazalisha umeme kule kule Mtwara! Sasa kama unavyojua uchumi wa Mikoa ya Kusini, umeme uliokuwa unazalishwa ulikuwa mwingi mno kulingana na mahitaji ya mikoa hiyo!

Na usidhani ulikuwa mamia ya MW, hell no... kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ulikuwa less than 30MW but still southern economy failed to consume that amount in electricity!

Sasa baada ya JK kuona Mtwara kuna gesi inayozalisha umeme kwa mikoa ya kusini, lakini mikoa haina uchumi wa kuweza ku-utilize huo umeme, ndipo serikali ikaamua kuisafirisha hiyo gesi hadi Dar es salaam, kisha uzalishwe umeme utaokaongizwa kwenye grid ya taifa na kutumika nchi nzima!!!

Na hata gesi aliyokuwa anaizungumzia sana Muhongo hadi kufikia kuwaita Wafanyabiashara wa Tanzania hawana pesa ya kuingia kwenye gas industry wala alikuwa hamaanishi hiyo gas ya Msimbati ambayo ilikuwa imeshaanza kuchimbwa bali alikuwa anamaanisha hiyo iliyogundulika deep sea ambayo haijachimbwa!!

REMEMBER, hiyo ya Msimbati na Songosongo kwa ujumla wake ni only 7.5 TCF wakati tuliyoahidiwa Tanzania kuwa kama Dubai, ni 47 TCF!

Bado tunaagiza gesi kutoka nje ya nchi!! Huo unafuu labda unaweza kupatikana endapo tutachimba hiyo gas ya baharini!! Na kama unafuatilia, TPDC waliitisha tenda ya kusambaza mabomba nchi mzima kwa ajili ya hiyo gesi ili ifike majumbani na viwandani!!

Kwa maana nyingine, ikishachimbwa, gasi itakuwa inasambazwa kwa mabomba na sio kwa matungi ingawaje pia mitungi itakuwepo kwa ajili ya maeneo yasiyofikika kwa mabomba!!

Hili la sukari ni pasua kichwa manake sijui tunakwama wapi...

Labda Bakheresa na kiwanda chake cha Bagamoyo atapunguza kama sio kumaliza tatizo hili!!

Hilo la saruji... of course, sote tuliamini Dangote angetatua lakini kwa kila mfuatiliaji anafahamu ni namna gani Kiwanda cha Dangote kilikumbwa na misukosuko mara kadhaa iliyosababisha kupunguza uzalishaji! Kubwa zaidi, ni pale alipopewa ahadi ya kupunguziwa gharama za gesi ili azalishe umeme wake binafsi, lakini ahadi hiyo haikutimizwa!!

Na hata pale alipoamua kugeukia Makaa ya Mawe, I hope unafahamu what happened!!
 
Kujuwa gharama sio issue ni jambo la kawaida kujuwa investment cost ila kwa swali lako pesa nyingi hilo sasa linategemea huo mradi wa LNG utakuwa na train ngapi ila kwa experiance yangu kufananisha na miradi mingine kama hiyo ya ukubwa wa kiasi ni kama Trillion 10 mpaka 15 tunafanye na mengine hautazidi trillion 20 hili na uhakika unless tunaenda kushindana na kina Qatar huko kwa kuwa sijui ukubwa wa plant yenyewe inataka maelezo kidogo. Kwa mwekezaji kupandisha gharama ni faida kwa kwake maana cost recovery hiyo.
Wait a minute 🤔🤔🤔 Mmmhhh okay.

Mkataba unasemaje? Sisi kama nchi tunapata % ngapi? So gharama tu ya uchimbaji ni tril 70? Eti? Gharama hizi kubwa mno wamezipataje kabla hata mradi haujamalizika? Yaani deni la Taifa tokea uhuru hadi sasa ni Tril 78. Sasa gharama za uchimbaji gesi hata pamoja na kujenga LNG plant zote ni tril 70? Hizi gharama kubwa sanaaa, something haiko sawa.

Jamani, nawaza tu, usikute waka zidisha gharama sana tukaanza kupigwa mapemaaaaaa. Nawaza tu, uuwiii, OMG.
 
Man,

Tofauti na watu wanavyodhani... Gesi ya Msimbati haikuanza kuchimbwa wakati wa JK bali tangu wakati wa Mkapa!!

Ambacho kilitokea, baada ya gesi kuchimbwa, Kampuni ya ARTMAS ikawa inazalisha umeme kule kule Mtwara! Sasa kama unavyojua uchumi wa Mikoa ya Kusini, umeme uliokuwa unazalishwa ulikuwa mwingi mno kulingana na mahitaji ya mikoa hiyo!

Na usidhani ulikuwa mamia ya MW, hell no... kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ulikuwa less than 30MW but still southern economy failed to consume that amount in electricity!

Sasa baada ya JK kuona Mtwara kuna gesi inayozalisha umeme kwa mikoa ya kusini, lakini mikoa haina uchumi wa kuweza ku-utilize huo umeme, ndipo serikali ikaamua kuisafirisha hiyo gesi hadi Dar es salaam, kisha uzalishwe umeme utaokaongizwa kwenye grid ya taifa na kutumika nchi nzima!!!

Na hata gesi aliyokuwa anaizungumzia sana Muhongo hadi kufikia kuwaita Wafanyabiashara wa Tanzania hawana pesa ya kuingia kwenye gas industry wala alikuwa hamaanishi hiyo gas ya Msimbati ambayo ilikuwa imeshaanza kuchimbwa bali alikuwa anamaanisha hiyo iliyogundulika deep sea ambayo haijachimbwa!!

REMEMBER, hiyo ya Msimbati na Songosongo kwa ujumla wake ni only 7.5 TCF wakati tuliyoahidiwa Tanzania kuwa kama Dubai, ni 47 TCF!

Bado tunaagiza gesi kutoka nje ya nchi!! Huo unafuu labda unaweza kupatikana endapo tutachimba hiyo gas ya baharini!! Na kama unafuatilia, TPDC waliitisha tenda ya kusambaza mabomba nchi mzima kwa ajili ya hiyo gesi ili ifike majumbani na viwandani!!

Kwa maana nyingine, ikishachimbwa, gasi itakuwa inasambazwa kwa mabomba na sio kwa matungi ingawaje pia mitungi itakuwepo kwa ajili ya maeneo yasiyofikika kwa mabomba!!

Hili la sukari ni pasua kichwa manake sijui tunakwama wapi...

Labda Bakheresa na kiwanda chake cha Bagamoyo atapunguza kama sio kumaliza tatizo hili!!

Hilo la saruji... of course, sote tuliamini Dangote angetatua lakini kwa kila mfuatiliaji anafahamu ni namna gani Kiwanda cha Dangote kilikumbwa na misukosuko mara kadhaa iliyosababisha kupunguza uzalishaji! Kubwa zaidi, ni pale alipopewa ahadi ya kupunguziwa gharama za gesi ili azalishe umeme wake binafsi, lakini ahadi hiyo haikutimizwa!!

Na hata pale alipoamua kugeukia Makaa ya Mawe, I hope unafahamu what happened!!
Mkuu Chige naheshimu sana na kuthamini mchango wako mkubwa hapa jamii forum, kupitia kwako nimejifunza mambo mengi ambayo nilikua siyafahamu, wewe ni katika miongoni mwa watu nnaojivunia uwepo wao hapa jukwaani, ila yote ya yote katika hii miradi kunakukuwa na propaganda na ahadi nyingi za uongo.
Kwa upande wako unajitahidi kutetea kua profesa Muhongo alikua hazungumzii gesi ile ya msimbati iliyosababisha jeshi kupelekwa Mtwara ili tu kufanikisha kujenga bomba la gesi ki ukweli kabisa sikubaliana na wewe kuhusu zile ahadi na propaganda zilihusu hio gesi ya trilion 70.
 
Mkuu Chige naheshimu sana na kuthamini mchango wako mkubwa hapa jamii forum, kupitia kwako nimejifunza mambo mengi ambayo nilikua siyafahamu wewe ni katika miongoni mwa watu nnaojivunia uwepo wao hapa jukwaani, ila yote ya yote katika hii miradi kunakukuwa na propaganda na ahadi nyingi za uongo.
Kwa upande wako unajitahidi kutetea kua profesa Muhongo alikua hazungumzii gesi ile ya msimbati iliyosababisha jeshi kupelekwa Mtwara ili tu kufanikisha kujenga bomba la gesi ki ukweli kabisa siwezi kukubaliana na wewe.
Kwanini hukubaliani na mimi Chifu?

Hivi una habari ile gesi ya Msimbati ni ONLY 5 Trillion Cubic Feet, out of 57.54 Trillion Cubic Feet of total gas discoveries huku 47 Trillion Cubic zikiwa hazijaguswa?!

Na hadi sasa, kama nilivyosema hapo awali, umeme wa gesi kwenye grid ya taifa ni 57%, na asilimia inayobaki ni kwa vyanzo vingine! Sasa kabla hatujaenda mbali, kama hadi sasa umeme wa gesi ni 57%, na bado tunaendelea kutafuta vyanzo vingine; nini hapo tafsiri yake kama sio hata huo umeme unaokuwa supplied na gas kwa sasa bado hautoshi?

Na kama hautoshi, hivi hiyo si ndo ile Wachumi wanaita Low Supply?! Kitu kikiwa in low supply, bei inakuwaje?!

Ni kweli Muhongo alisema bei itapungua lakini sio katika mazingira ya sasa ambayo hata huo umeme wenyewe bado hautoshi!! Unaweza kupungua endapo utazalishwa umeme mwingi zaidi!! Na umeme mwingi zaidi utazalishwa baada ya kukamilika Bwawa la Nyerere au tukianza kuchimba ile gesi ya kina kirefu!!

Hata hivyo, napo kupungua kwenyewe kwa bei kutategemeana na principle ipi ya kiuchumi itatumika! Kwa bahati mbaya sana, watu wanaamini kwenye kuongeza bei ili kuongeza mapato, wakati mtu kama mimi naamini kwenye kuongeza mauzo kama njia bora ya kuongeza mapato, wakati factors zingine zinabaki constant!!

Maana yake ni nini?! Hata Bwawa la Nyerere likishakamilika, ndio umeme utakuwa mwingi sana lakini hapo hapo taifa litakuwa limeingia gharama kubwa za uwekezaji kwenye hilo bwawa!!

Sasa basi, kwenye hizo principle nilizotaja hapo juu, Serikali inaweza ku-opt kubakisha bei ya umeme kama ilivyo ikidhani bei kubwa inawaongezea mapato ya ku-finance gharama walizoingia kwenye ujenzi wa bwawa, huku wakisahau ukifanya hivyo unakuwa una-discourage matumizi ya umeme!

Tafsiri ya haraka ya ku-discourage matumizi ya umeme inafanya TANESCO wauze units chache!! Kwa mazingira ya sasa, LAZIMA u-discourage matumizi kwa sababu watu wakianza kutumia umeme kadri watakavyo, umeme uliopo hautatosha! Lakini kama tayari una umeme wa kutosha, hapatakuwa na sababu ya ku-discourage matumizi ya umeme!!

Yaani, ningekuwa mimi ningeshusha bei ili ku-encourage matumizi ya umeme! Ukishusha bei, hata wale wanaoogopa kutumia majiko ya umeme hatimae wataanza kutumia! Watu watapiga pasi hadi sidiria na boksa, na hivyo kupelekea TANESCO kuuza units nyingi zaidi ya umeme, na hatimae kupata mapato makubwa zaidi... win win game!!

Ninachotaka kusema hapo ni kwamba, Muhongo sio mjinga wa kudhani kwamba ile gesi iliyoanza kuchimbwa peke yake ingeleta umeme wa ziada na hivyo kusababisha bei ipungue!! Lakini pamoja na hayo, bado alikuwa na matumaini in the future tutazalisha umeme mwingi zaidi kwa sababu imegundulika gesi nyingi zaidi, na ndo maana hata lile bomba, ni kubwa maradufu kuliko hata gesi inayosafirishwa hivi sasa!!

CAG.png
 
Back
Top Bottom