Kwanini hukubaliani na mimi Chifu?
Hivi una habari ile gesi ya Msimbati ni ONLY 5 Trillion Cubic Feet, out of 57.54 Trillion Cubic Feet of total gas discoveries huku 47 Trillion Cubic zikiwa hazijaguswa?!
Na hadi sasa, kama nilivyosema hapo awali, umeme wa gesi kwenye grid ya taifa ni 57%, na asilimia inayobaki ni kwa vyanzo vingine! Sasa kabla hatujaenda mbali, kama hadi sasa umeme wa gesi ni 57%, na bado tunaendelea kutafuta vyanzo vingine; nini hapo tafsiri yake kama sio hata huo umeme unaokuwa supplied na gas kwa sasa bado hautoshi?
Na kama hautoshi, hivi hiyo si ndo ile Wachumi wanaita Low Supply?! Kitu kikiwa in low supply, bei inakuwaje?!
Ni kweli Muhongo alisema bei itapungua lakini sio katika mazingira ya sasa ambayo hata huo umeme wenyewe bado hautoshi!! Unaweza kupungua endapo utazalishwa umeme mwingi zaidi!! Na umeme mwingi zaidi utazalishwa baada ya kukamilika Bwawa la Nyerere au tukianza kuchimba ile gesi ya kina kirefu!!
Hata hivyo, napo kupungua kwenyewe kwa bei kutategemeana na principle ipi ya kiuchumi itatumika! Kwa bahati mbaya sana, watu wanaamini kwenye kuongeza bei ili kuongeza mapato, wakati mtu kama mimi naamini kwenye kuongeza mauzo kama njia bora ya kuongeza mapato, wakati factors zingine zinabaki constant!!
Maana yake ni nini?! Hata Bwawa la Nyerere likishakamilika, ndio umeme utakuwa mwingi sana lakini hapo hapo taifa litakuwa limeingia gharama kubwa za uwekezaji kwenye hilo bwawa!!
Sasa basi, kwenye hizo principle nilizotaja hapo juu, Serikali inaweza ku-opt kubakisha bei ya umeme kama ilivyo ikidhani bei kubwa inawaongezea mapato ya ku-finance gharama walizoingia kwenye ujenzi wa bwawa, huku wakisahau ukifanya hivyo unakuwa una-discourage matumizi ya umeme!
Tafsiri ya haraka ya ku-discourage matumizi ya umeme inafanya TANESCO wauze units chache!! Kwa mazingira ya sasa, LAZIMA u-discourage matumizi kwa sababu watu wakianza kutumia umeme kadri watakavyo, umeme uliopo hautatosha! Lakini kama tayari una umeme wa kutosha, hapatakuwa na sababu ya ku-discourage matumizi ya umeme!!
Yaani, ningekuwa mimi ningeshusha bei ili ku-encourage matumizi ya umeme! Ukishusha bei, hata wale wanaoogopa kutumia majiko ya umeme hatimae wataanza kutumia! Watu watapiga pasi hadi sidiria na boksa, na hivyo kupelekea TANESCO kuuza units nyingi zaidi ya umeme, na hatimae kupata mapato makubwa zaidi... win win game!!
Ninachotaka kusema hapo ni kwamba, Muhongo sio mjinga wa kudhani kwamba ile gesi iliyoanza kuchimbwa peke yake ingeleta umeme wa ziada na hivyo kusababisha bei ipungue!! Lakini pamoja na hayo, bado alikuwa na matumaini in the future tutazalisha umeme mwingi zaidi kwa sababu imegundulika gesi nyingi zaidi, na ndo maana hata lile bomba, ni kubwa maradufu kuliko hata gesi inayosafirishwa hivi sasa!!
View attachment 2010039