Pre GE2025 Makamba: Hata kama hatumkubali Rais Samia, ni wetu

Pre GE2025 Makamba: Hata kama hatumkubali Rais Samia, ni wetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu hivyo tunatakiwa kuacha siasa hasa kuhusu ziara zake nje ya nchi kwani zimeleta manufaa makubwa kwa nchi.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Zaidi sikiliza hii link mpaka mwisho

Ameonyesha hisia zake,hamkubali kama ilivyo kwa sisi wengine.
 
Hivi hata ingekuwa wewe upige billion 60 za ghafla utaacha kumsifia Mama kweli?😂
Umezipiga na umemsifia sawa,lakini hayo yote yanaonyesha kwamba you are morally corrupt.A real person cannot do that,hata iwe 100 trillion.After all
itamsaidia mtu nini kupata ulimwengu wote,halafu katika umilele apate hasara ya nafsi yake(Marko 8:36).Jesus Christ said no to such an offer by Satan in Matthew 4:8-10

Mathayo 4:8-10
8 Kisha Ibilisi akamchukua Bwana Yesu mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
 
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu hivyo tunatakiwa kuacha siasa hasa kuhusu ziara zake nje ya nchi kwani zimeleta manufaa makubwa kwa nchi.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Zaidi sikiliza hii link mpaka mwisho


Hiyo KAULI ya Makamba ina UKAKASI .... Labda kwa kuwa mimi ni wa Bara sielewi vizuri hicho Kiswahili chake.....!!
 
Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Dalili dhahiri bila chenga kwenye screen ya televisheni tunaona na kusikia kuwa ndani ya chama dola kongwe CCM kuna mtafaruku uliozua nyufa katika chama, kugawanyika mitizamo, makundi kuwepo na mayowe ya wengi kutomkubali kiongozi wao athibitisha balozi namba mbili (balozi namba moja ni rais) waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Januari Yusuf Makamba.

Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri wa Muungano Tanzania kauli zake huchukuliwa kwa uzito ndani hadi mataifa ya nje ikiwemo JF ya watu makini great thinkers.

Tukirejea historia ya mawaziri wa mambo ya nje Tanzania baadaye waliteuliwa kuwa mawaziri wakuu hata marais.

Mawaziri wa mambo ya nje waliokuwa marais baadaye ni Jakaya Kikwete, Benjamin Mkapa. Waliokuwa mawaziri wakuu intaneti inatupa majina ya John Malecela, Salim Ahmed Salim, waliowania urais Bernard Membe, Oscar Kambona n.k mtandao wa intanet na google search inaonesha
1717683916305.png

Picha maktaba: Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje yaani balozi namba mbili kwa uzito Tanzania akikutana na Fidel Castro kiongozi wa Cuba. Source : salimAhmedSalim.com


Kauli hii ya January au Januari kama mzee Makamba anavyomuita ni kauli nzito za ndani kabisa ya hali ya kisiasa ilivyo katika dhoruba la makundi kupingana kuhusu kiongozi wao mkuu kama anatosha au la.

Nchi zingine kauli tata za waziri wa mambo ya nje huweza kuleta mtafaruku na pia kumpunguzia uzito ktk ushawishi kisiasa boss wake machoni mwa jumuiya ya kimataifa mbali na umma wa ndani ya nchi ya asili.

Vyombo makini vya nje, na balozi za kigeni nchini watakuwa wamenukuu kauli hii nzito ya balozi namba mbili wa Tanzania kuhusu kinachoendelea ndani ya taasisi kubwa ya chama dola kongwe upinzani wa ndani ya chama cha mapinduzi kwa bosi wake na kuitia taarifa hii katika mizania ya mahusiano ya kimataifa
 
Maamuzi, kauli, matendo na mienendo ya balozi namba mbili yaani waziri wa mambo ya nje zinaweza kusababisha afutwe kazi mara moja mfano ..... hata kama waziri alifanya kazi kidiplomasia nzuri lakini inakwenda kinyume na sera za serikali ya Libya ikabidi atimuliwe..

Sasa January Makamba kwenda kinyume cha desturi na mila za Chama Dola CCM, kauli yake hata kama ni kweli, lakini siyo utamaduni ya CCM kumtweza kiongozi mkuu kuonesha hakubaliki na wengi lakini ipo namna kwa kupoka demokrasia atabaki ...


Al Jazeera
www.aljazeera.com
Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Najla al-Mangoush apewa karipio na kutimuliwa mbali: Vyanzo ...

28 Ago 2023 - Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Najla al-Mangoush, alikosolewa kwa kukutana na mwenzake wa Israeli, amefutwa kazi kwa kwenda kinyume na destruri, mazoea ya diplomasia ya Libya inayoona si sawa kukutana na viongozi wa Israeli.....
 
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu hivyo tunatakiwa kuacha siasa hasa kuhusu ziara zake nje ya nchi kwani zimeleta manufaa makubwa kwa nchi.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Zaidi sikiliza hii link mpaka mwisho

This is bullshit aise. Kwaiyo hata kama unayoenda kufanya huko nje kwa kutuwakilisha sisi ni yale tunayoona hayafai tukukalie kimya eti kwamba tukungoje urudi ndio tukuseme/kukushauri.


Sijui hii ngozi nyeusi ina nn.
 
Back
Top Bottom