Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea
Dalili dhahiri bila chenga kwenye screen ya televisheni tunaona na kusikia kuwa ndani ya chama dola kongwe CCM kuna mtafaruku uliozua nyufa katika chama, kugawanyika mitizamo, makundi kuwepo na mayowe ya wengi kutomkubali kiongozi wao athibitisha balozi namba mbili (balozi namba moja ni rais) waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Januari Yusuf Makamba.
Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri wa Muungano Tanzania kauli zake huchukuliwa kwa uzito ndani hadi mataifa ya nje ikiwemo JF ya watu makini great thinkers.
Tukirejea historia ya mawaziri wa mambo ya nje Tanzania baadaye waliteuliwa kuwa mawaziri wakuu hata marais.
Mawaziri wa mambo ya nje waliokuwa marais baadaye ni Jakaya Kikwete, Benjamin Mkapa. Waliokuwa mawaziri wakuu intaneti inatupa majina ya John Malecela, Salim Ahmed Salim, waliowania urais Bernard Membe, Oscar Kambona n.k mtandao wa intanet na google search inaonesha
Picha maktaba: Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje yaani balozi namba mbili kwa uzito Tanzania akikutana na Fidel Castro kiongozi wa Cuba. Source : salimAhmedSalim.com
Kauli hii ya January au Januari kama mzee Makamba anavyomuita ni kauli nzito za ndani kabisa ya hali ya kisiasa ilivyo katika dhoruba la makundi kupingana kuhusu kiongozi wao mkuu kama anatosha au la.
Nchi zingine kauli tata za waziri wa mambo ya nje huweza kuleta mtafaruku na pia kumpunguzia uzito ktk ushawishi kisiasa boss wake machoni mwa jumuiya ya kimataifa mbali na umma wa ndani ya nchi ya asili.
Vyombo makini vya nje, na balozi za kigeni nchini watakuwa wamenukuu kauli hii nzito ya balozi namba mbili wa Tanzania kuhusu kinachoendelea ndani ya taasisi kubwa ya chama dola kongwe upinzani wa ndani ya chama cha mapinduzi kwa bosi wake na kuitia taarifa hii katika mizania ya mahusiano ya kimataifa