Makamba: Kurekebisha alichofanya Hayati Magufuli sio usaliti. Dalili nilizoanza kuziona si nzuri

Hakuna anayesema Magufuli alikuwa Malaika. Lakini kutumia mwanya wa kuondoka kwake kuturudisha kwenye corruption ya wazi; ukwepaji kodi; uwekezaji holela wa wazungu n.k sio sawa. Tumeishatoka uko. Tumkosoe kwa mambo ya msingi kama kuweka mazingira rafiki ya biashara, kuongeza ajira na kuongeza demokrasia n.k. bila kusahau lengo ni kupeleka nchi mbele.
 
Na wewe umerudia upumbavu ule ule alioukataa Makamba!

Shida iliyopo sasa hivi ni kwamba kuna watu hasa wapinzani wanataka Samia aongoze kwa mawazo yao, yani utasikia toa yule weka yule, ukiuliza kwa sababu gani utaambiwa sababu aliteuliwa na magufuli!

Yani kisa eti kwakuwa mtu aliteuliwa na Magufuli basi asiwepo kwenye seilikali ya Rais Samia ambao wote ni ccm. Na nyuma ya hii hoja ya nyie wapumbavu ni kujaribu kuonesha kwamba Magufuli hakuna lolote jema alilofanya.

Hii nguvu mnayotumia sasa hivi kujaribu kupambana na marehemu mngeitumia kupigania ile mifumo mibovu mnayosemaga inawanyima kura. Lakini kwa kuwa nyie ni wajinga mtakumbuka hayo ikifika oktoba 2025.

Mwacheni Samia aongoze nchi kwa utashi atakaoshauriwa na washauri wake, ccm ni tasisi kubwa na Samia hataongoza kwa matakwa ya nyie wajinga wachache bali kwa mfumo unaotokana na chama chake.
 
Makamba ni mmoja kati ya watanzania amesema alichojisikia kwa sababu zake ila na yeye mwenyewe anatakiwa kujisahihisha kwingi tuuu

Neno lake sio sheria sababu watanzania wengine pia wanasema wanachojisikia

Your browser is not able to display this video.



Kazi iendelee
 
Kama Mtu Akifa anasifiwa kwa Mema yake Basi lazima Pia Alaumiwe kwa Ubaya wake ili iwe Funzo na kwa Wengini na Sio Kosa Msema aliyekufa iwe kwa Mazuri au Mabaya
Kila mtu ana mabaya hata wewe. Lakini kwa mila zetu mtu akifa mabaya tunamwachia Mungu sisi tunachukua mazuri
 
CCM kimenuka
 
Watajuana hayatuhusu.
 
Kila mtu ana mabaya hata wewe. Lakini kwa mila zetu mtu akifa mabaya tunamwachia Mungu sisi tunachukua mazuri
hatusemi makosa ya maguful, tunasema makosa ya Rais. Tatizo Maguful alihodhi Urais na ndo maana makosa mengi (Kama si yote) yanamwangukia Maguful badala ya Rais.
 
Sukuma gang hadi walianzisha dini ya Magufulism
hatusemi makosa ya maguful, tunasema makosa ya Rais. Tatizo Maguful alihodhi Urais na ndo maana makosa mengi (Kama si yote) yanamwangukia Maguful badala ya Rais.
 
Kama Mtu Akifa anasifiwa kwa Mema yake Basi lazima Pia Alaumiwe kwa Ubaya wake ili iwe Funzo na kwa Wengini na Sio Kosa Msema aliyekufa iwe kwa Mazuri au Mabaya.
Ivi Ni kweli hairuhusiwi kumsema mtu kwa mabaya. Hasa kwa wenzetu waislamu, Kuna sehemu Quran imekataza.
 
umemaliza kabisa,
 
Bado tunamfikiria kumpa U-PM ...
Mheshimiwa Rais Samia ametuahidi kuwa atafuata nyayo za mtangulizi wake. Moja kati ya mambo ambayo Magufuli aliyoyaweka hadharani ni tahadhali aliyompa waziri mkuu kuwa asitegemee kuwa angeshika hicho cheo kwa miaka 10 kwani itategemea utendaji wake!! Sasa kama huyu waziri mkuu alikuwa katika kundi lililotaka kuvunja katiba baada ya kifo cha mwendazake, mama wala usiwe na kigugumizi kumtumbua!
 
Hakuna shujaa jizi la kura, labda shujaa wa watu wasiojulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…