Makamba: Kurekebisha alichofanya Hayati Magufuli sio usaliti. Dalili nilizoanza kuziona si nzuri

Makamba: Kurekebisha alichofanya Hayati Magufuli sio usaliti. Dalili nilizoanza kuziona si nzuri

Makamba haaminiki tena na raia sijui afanyaje aeleweke na wananchi wa kawaida.

Kwanza akwenda mzika Magufuli na pia alikuwa ameanzisha vuguvugu la kumsaliti pindi akiwa hai.
Raia gani hao wasiomwamini?mbona wengine tunamwamini sana tu
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kifo cha Magufuli kimeleta kipindi cha mpito chenye wasiwasi ila Rais Samia Suluhu ameanza vizuri kuendeleza yale aliyoacha Rais na kufanya marekebisho na mashahihisho pale panapostahili

Makamba ameongea kauli za kutiliana shaka, utengano, kuhukumiana na tuhumiana hazijengi na zinawachanganya wananchi,

Kaendelea kusema pia mazuri aliyofanya rais Magufuli hayatapotea kwa kauli za kubeza lakini pia wanaotoa maoni ya kurekebisha mambo wasionekane ni wasaliti kwani ameanza kuona dalili ambazo sio nzuri

Zaidi msikilize hapa


Magufuli kuna mengi mazuri kayafanya na ya kuendelezwa, lakini kuna mengi abaya ya kukemewa na kutoyafanya, mfano JPM alikubali kuwa hashauriki-hiyo ni handicap.

Mwalimu Nyerere vile vle kuna mengi aliyafanya-kujenga utaifa, lakini kuna mengi vile vile alifanya-forced villagisation.

Mwinyi kuna Mengi tu aliyafanya-Ruksa na kulegeza masharti ya biashara na uchumi, lakini vile vile kuna mengi naye alifanya-matapeli toka nje waliingia nchini.

Mkapa kuna mengi aliyafanya, kuisuka na kuitengeneza TRA, na TANROADS, lakini kuna mengi mabaya aliyafanya -kuuza mashirika kiholela, kuuza nyumba za serikali

Kikwete kuna mengi tu aliyafanya, kukaribisha wawekezaji wengi kama kina Dangote, Gas, Kinyerezi I,II . Lakini kuna mengi tu alikosea, kusafiri sana kama Sindbad na kutosimamia vizuri serikali yake.

Sasa najiuliza Magufuli kwani ni malaika, hadi asikosolewe?
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kifo cha Magufuli kimeleta kipindi cha mpito chenye wasiwasi ila Rais Samia Suluhu ameanza vizuri kuendeleza yale aliyoacha Rais na kufanya marekebisho na mashahihisho pale panapostahili

Makamba ameongea kauli za kutiliana shaka, utengano, kuhukumiana na tuhumiana hazijengi na zinawachanganya wananchi,

Kaendelea kusema pia mazuri aliyofanya rais Magufuli hayatapotea kwa kauli za kubeza lakini pia wanaotoa maoni ya kurekebisha mambo wasionekane ni wasaliti kwani ameanza kuona dalili ambazo sio nzuri

Zaidi msikilize hapa


Huyu msaliti utaona anamchomekea maneno samia. Ni mnafiki tu anawakilisha wapigaji.
 
downloadfile.gif

Tuwaangalie tu Mbiti watifuane Wenyewe
 
Nadhani kuna kikundi ni kama wanampigia kampeni marehemu hata hujui nia yao ni nini? Mtu amefariki nikumuombea tu haya ya duniani watafanya walioko wala sio lazima kila mtu aje afanye kama marehemu. mwacheni Mama atawale kivyake kama humkubali subiri uchaguzi piga kura basi.
 
Wale wezi wana taka Mama aendelee kuwafunga watu, kuwaibia watu, kuwapa watu kesi za kugushi. Maana walisha kula mbwa wanataka wamlishe na mama.

Tumeona Mama kaagiza kesi zisizonna ushahidi zifutwe, ila mwezi sasa Dpp yuko kimya. Mama kaahiza vyombo vya habari vifunguliwe, kanuni zifuatwr, waziri ana itisha vikao kujadiliana, yani hakuna nidhamu kwenye huu utawala.

Bado wanafikiribMagu yuko hai. Sasa tumuombe Mama awashughulikie hawa wote wanao pandisha mabega...
Mama kajichanganya mwenyewe, watu walishauri avunje Baraza lote la mawaziri.
Aanze upya,sijui kakutana na Nini huyu mama.
Kosa hili litamgharimu Sana.

Mwisho wa siku naiona aibu ikimpata
 
Maneno mazuri sana January kaongea

Kushindana kuonyesha nani ni mnazi zaidi wa rais Magufuli is useless, this man is dead na harudi tena.

Na kushibdana kuonyesha nani ni mnazi zaidi wa rais Samia ni kupoteza muda, kwa sababu Samia keshasoma gemu lote anajua nini maana ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!

Cha msingi ni kuwa turudi kujenga nchi kwa kutumia watu waliotosha kwa vigezo na siyo wanaojua sana kushangilia, kusifu na kujipendekeza.

Samia ana kazi kubwa ya kutengeneza serikali inayoendana na yeye na vision yake kwa nchi, hana budi kuondoa wale wote walioingia kwenye serikali kwa kununuliwa, kujipendekeza, uzandiki na fitna.

Aweke wataalamu huko kwenye kurugenzi za halmashauri na aachane na ukada
Well said Missile of the Nation
 
Mchango uliotolewa leo na mbunge wa Bumbuli mheshimiwa kijana January Makamba umeonyesha kuwa pamoja na CCM pakacha lao kujaa viongozi uchwara kumbe wapo (yupo) walao wenye akili.

Kama CCM ingekuwa na hata nusu ya viongozi wenye akili kama huyu hakika kingekuwa chama cha kuheshimika sana.

Hapa hata ukiwachanganya Majaliwa, Ndugai, Tulia, Mwigulu, Lusinde na Jenister combined hawafikii akili ya Makamba. Hii ni aibu kwa hata Naibu Spika kumkatiza hotuba yake Makamba

 
Kama Mtu Akifa anasifiwa kwa Mema yake Basi lazima Pia Alaumiwe kwa Ubaya wake ili iwe Funzo na kwa Wengini na Sio Kosa Msema aliyekufa iwe kwa Mazuri au Mabaya.
Unamlaumu vipi marehemu? Ili upate nini? Na nani ajibu malalamiko yako?
 
Back
Top Bottom