Makamba: Kurekebisha alichofanya Hayati Magufuli sio usaliti. Dalili nilizoanza kuziona si nzuri

Makamba: Kurekebisha alichofanya Hayati Magufuli sio usaliti. Dalili nilizoanza kuziona si nzuri

Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kifo cha Magufuli kimeleta kipindi cha mpito chenye wasiwasi ila Rais Samia Suluhu ameanza vizuri kuendeleza yale aliyoacha Rais na kufanya marekebisho na mashahihisho pale panapostahili

Makamba ameongea kauli za kutiliana shaka, utengano, kuhukumiana na tuhumiana hazijengi na zinawachanganya wananchi,

Kaendelea kusema pia mazuri aliyofanya rais Magufuli hayatapotea kwa kauli za kubeza lakini pia wanaotoa maoni ya kurekebisha mambo wasionekane ni wasaliti kwani ameanza kuona dalili ambazo sio nzuri

Zaidi msikilize hapa

Tatizo ni anayesema hayo ukimuangalia usoni unajiuliza hii kauli inatoka kweli kwake -kauli ya Mwl.

Na mwisho dhumuni la kufanya hayo Mabadiliko nini , icd, nasaco, ttcl, sgr vs mabus/ma lorry , vi tanesco, gas,
 
Kuna watu wana akili fupi sana!

Kuna wakati hata mimi niliambiwa eti natafuta uteuzi toka kwa Magufuli!

Kibinafsi sikumjua na yeye wala hakunijua.

Sasa ndo aje kuniteua mimi kwa kunisoma tu JF??

Akili za nyumbu bana...wanazijua wenyewe tu.

Yaani Magufuli akose wote anaowajua huko halafu aje JF na kusoma baadhi ya mabandiko ya Nyani Ngabu akimsifia, halafu eti amteue.

Kwanza anaanza anzaje? Ananitumia PM au?
Kwa akili za magufuli lolote lingewezekana especially km ungekuwa unatumia id yenye jina lako kamili

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ametolea mfano mambo gani ambaye Rais Samia anayarekebisha?
TAKUKURU kubambikiza watu kesi zisizo na ushahidi, TRA kupora wafanyabiashara fedha na kutishia kuwapa kesi za uhujumu uchumi, kugombana na mataifa ya nje kwa kuwaita mabeberu, kugombana na majirani n.k mpaka Makamba akutajie mzee?
 
Ushamfukuza jamvini
 
Masta mind wa hili ni PM wake na makamu wa Rais hawa ni wakufuza (PM)na makamu wa Rais ni kumblack mail,
Credebility ya PM imeshuka hadi sifuri tangu kudanganya umma wa watanzania afya ya rais ni imara, mbaya zaidi alikuwepo msikitini.
 
TAKUKURU kubambikiza watu kesi zisizo na ushahidi, TRA kupora wafanyabiashara fedha na kutishia kuwapa kesi za uhujumu uchumi, kugombana na mataifa ya nje kwa kuwaita mabeberu, kugombana na majirani n.k mpaka Makamba akutajie mzee?
Yeye ndio katia mifano hiyo au unawakilisha mawazo yake?
 
The guy is smart up stairs, ila wana filosofia walishakataa kwamba hakuna "mawazo huru/free philosophy". Huyu ndugu haoneshi kumponda Mwendazake, wala hamsifii. Yeye anajiweka katikati.
Napenda ajitambulishe tumjue na kumhukum kwayo.
Hatujasahau wakati ule alivotutumbukiza kwenye " cyber law " ambayo mpk leo imepelekea kuzikwa kwa Uhuru wa mawazo kwa jamii.
 
Kama Mtu Akifa anasifiwa kwa Mema yake Basi lazima Pia Alaumiwe kwa Ubaya wake ili iwe Funzo na kwa Wengini na Sio Kosa Msema aliyekufa iwe kwa Mazuri au Mabaya.
Hiyo ni enzi na enzi huwezi kuuvunja huo mwiko kwa chuki zako! Mpaka kushindana na marehemu. Itakusaidia nini au marehemu atajirekebishaje ukimshinda!
 
Na wewe umerudia upumbavu ule ule alioukataa Makamba!

Shida iliyopo sasa hivi ni kwamba kuna watu hasa wapinzani wanataka Samia aongoze kwa mawazo yao, yani utasikia toa yule weka yule, ukiuliza kwa sababu gani utaambiwa sababu aliteuliwa na magufuli!

Yani kisa eti kwakuwa mtu aliteuliwa na Magufuli basi asiwepo kwenye seilikali ya Rais Samia ambao wote ni ccm. Na nyuma ya hii hoja ya nyie wapumbavu ni kujaribu kuonesha kwamba Magufuli hakuna lolote jema alilofanya.

Hii nguvu mnayotumia sasa hivi kujaribu kupambana na marehemu mngeitumia kupigania ile mifumo mibovu mnayosemaga inawanyima kura. Lakini kwa kuwa nyie ni wajinga mtakumbuka hayo ikifika oktoba 2025.

Mwacheni Samia aongoze nchi kwa utashi atakaoshauriwa na washauri wake, ccm ni tasisi kubwa na Samia hataongoza kwa matakwa ya nyie wajinga wachache bali kwa mfumo unaotokana na chama chake.
Mnawasingizia wapinzani mbowe kaongea hajasema hill zote kachambo ripoti ya CAG hajasema hivyomtoa made no follower wa kigogo huyo ndiyo nimemsikia twitter,
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kifo cha Magufuli kimeleta kipindi cha mpito chenye wasiwasi ila Rais Samia Suluhu ameanza vizuri kuendeleza yale aliyoacha Rais na kufanya marekebisho na mashahihisho pale panapostahili

Makamba ameongea kauli za kutiliana shaka, utengano, kuhukumiana na tuhumiana hazijengi na zinawachanganya wananchi,

Kaendelea kusema pia mazuri aliyofanya rais Magufuli hayatapotea kwa kauli za kubeza lakini pia wanaotoa maoni ya kurekebisha mambo wasionekane ni wasaliti kwani ameanza kuona dalili ambazo sio nzuri

Zaidi msikilize hapa

DAlili gamni msituletee ujinga hapa. Mama Samia , Mh. Rais endelkeza ndoto za magufuli otherwise Mama yangu ukishindwa kuna wanaounyemelea urais. Work hard as you used to do. Utafanikiwa tu!
 
Magufuli alifanikiwa sana kuwafanya baadhi ya watanzania kumwona mungu. Asiyekosea
Yaani Ni Nabii tena Mafalme hasa. Na he hang on. Hajafariki yumo hai ndani ya Mioyo ya mamilioni ya watanzania. Sasa wewe Furuki=utia humuhumu mitandaoni usilogwe kuyasema mitaani unless hujitaki!
 
Back
Top Bottom