Makamba: Sisi tumeamua kuwa wakweli, bwawa la Nyerere linaisha Juni 2024. Adai tarehe ya mwanzo isingewezekana kwa namna yoyote

Makamba: Sisi tumeamua kuwa wakweli, bwawa la Nyerere linaisha Juni 2024. Adai tarehe ya mwanzo isingewezekana kwa namna yoyote

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Akiwa Clouds TV, waziri wa nishati January Makamba amesema bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere linaisha mwezi Juni mwaka 2024 na wameamua kwenda na uhalisia na hawaoni aibu kusema litaenda miaka miwili mbele kuliko tarehe iliyotarajiwa kwani kwa namna yoyote isingewezekana ile tarehe ilitangazwa awali.

Awali Makamba amesema bwawa limeanza kujengwa Disemba 2018 na mpaka 2021(awamu ya tano) lilikuwa limejengwa kwa asilimia 37 kwa miaka miwili na nusu lakini mwaka mmoja(Awamu ya sita) limefika asilimia 74.

Makamba amesema wameongeza usimamizi na wamebadilisha 'Project Management' na wametumia pesa zaidi kupitia Tanesco kuhakikisha unakamilika kwa viwango na ubora.

Makamba pia amesema wameweka vichwa vyao pale na watapoinua uwe umeisha hivyo mambo ya Bungeni wao hawayasikilizi bali wanasimamia mradi vizuri na hali ilipo ni nzuri.

Awamu iliyopita ilidhamiria kumaliza bwawa la Nyerere Juni mwaka huu wa 2022.

Kuhusu hali ya umeme nchini, Makamba amesema umeme unaozalishwa nchini ni megawatts 1700 na mahitaji ya juu ni megawatts 1500 hivyo nchi inajitosheleza.



PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA


HISTORIA

 
Kwa hivyo kama hawalisikilizi Bunge ambalo ndiyo wawakilishi wa wananchi maana yake hakuna sababu ya kuwepo kwa Bunge??

Mkuu CCM walianza kama utani wakahakikisha Serekali inakuwa na nguvu kuliko bunge, maana walikuwa wanaona wapinzani wanapata nguvu kupitia bunge. Matokeo yake ndio haya, bunge limekuwa kibogoyo hadi akina Makamba wanasema hawalisikilizi bunge, maana kwa sasa bunge limegeuka sehemu ya kujengea kambi za makundi ndani ya CCM.
 
Hili Bwawa linaweza kukamilika 2030.

Halafu hiyo dharau kwa Bunge, ni matokeo ya Bunge lenyewe kuwa dhaifu na wabunge wala wasilalamike.
 
Hata ndege na flyover mlisema haiwezekani lakini leo tunaziona
January Makamba sasa ndiye waziri wa nishati na umeme, huku kusini wale KANGOMBA wanafanya shughuli zao.

Korosho inavunwa na kuuzwa bila kutumia JWTZ
afufuke sasa
 
Anasikiliza Bunge la Jamhuri ya Msoga!

Wamepanga kabisa January atakuwa Rais 2025 na Ridhiwan 2035. Ila Mama ajiangalie, maana amezungukwa na Mbwa mwitu, asipojipanga anaweza asifike 2025.

Wewe uliona wapi Duniani, Waziri hasikilizi Bunge! JK na Rostam ni watu hatari kwa usalama wa nchi.
 
Nakubaliana na usemi wa Makamba.
Tusisahau fiksi nyingi tulizolishwa Awamu ya Mwendazake, ingawaze Mwendazake ata enziwa kwa kuanza ujenzi wa huu mradi.
Kuna tofauti ya ufanyaji kazi. Miradi mingi ya Magufuli kazi zilifanyika usiku na mchana.

Nakumbuka ile SGR waziri Kamwele aliwahi kuvamia site usiku akakuta kazi inaendelea.

Sasa haya mambo January hawezi. Anataka kula bata tu huku akitembea na cheo cha uwaziri.
 
Back
Top Bottom