Makamba: Sisi tumeamua kuwa wakweli, bwawa la Nyerere linaisha Juni 2024. Adai tarehe ya mwanzo isingewezekana kwa namna yoyote

Makamba: Sisi tumeamua kuwa wakweli, bwawa la Nyerere linaisha Juni 2024. Adai tarehe ya mwanzo isingewezekana kwa namna yoyote

Kuna tofauti ya ufanyaji kazi. Miradi mingi ya Magufuli kazi zilifanyika usiku na mchana.

Nakumbuka ile SGR waziri Kamwele aliwahi kuvamia site usiku akakuta kazi inaendelea.

Sasa haya mambo January hawezi. Anataka kula bata tu huku akitembea na cheo cha uwaziri.
Usiku na Mchana lkn kwa miaka Miwili Unusu walijenga only 30%!
 


Hao ndio CCM uki fungua mlango jua unakaribisha nuksi.

Yaani mtu apambane na mabeberu waliotoka kuzuia mradi kwa madai ya mazingira. Achopoe hela za miradi mingine na kutumia hela za walipa kodi not budgeted for kwa mradi.

Halafu leo umwite muongo, sasa amuongopee nani wakati huo mradi kwa Magufuli ni mtoto wake. Kaubuni yeye na kauanzisha yeye, awamu ya sita imeukutia kati tu.
 
Haiwezekani au yeye ndio yupo busy na mitungi ya gesi.
 
Ah Makamba!!!eeh Ndugu yangu!!!

Kumbe SERIKALI iliyopita walikuwa waongo sio!!?

Nyie ndio wakweli!!

Hivi mnajua kuuendeleza kuponda awamu iliyopita itawafanya wenye DOLA kuwachukia Rasmi na kuwanyang'anya na kijiti akapewa MWINGINE!?

Watawauliza Kwamba wakati awamu iliyopita inadanganya wewe msaidizi wake ulikiwa WAPI kusema kweli!!?ina Maana uliapa kuilinda na kuitetea jamuhuri au kuiangamiza!!?kwanini useme mlidanganya na Sasa tuta aaminije kama hamtudanganyi wakati mlikuwepo NDANI ya utawala!!?

Mtajibu nini eeh makamba!!?

Mtamteteaje namba Moja hapo!!?

NIMEANDIKA tu,ili nichangie uchumi!!
 
Asante sana mheshimiwa waziri, Niko eneo la mradi, kwangu Mimi hii Ni habari njema zaidi, 600,000x24 Ni sawa na 14,400,000/=

Mungu Ni mwema, kuja kuisha mradi nitakuwa nimepata mtaji.

Sioni haja ya kuwa na haraka, kikubwa watanzania wajue kuwa mradi unaendelea na utakamilika tu.
 
Anasikiliza Bunge la Jamhuri ya Msoga!
Wamepanga kabisa January atakuwa Rais 2025 na Ridhiwan 2035. Ila Mama ajiangalie, maana amezungukwa na Mbwa mwitu,asipojipanga anaweza asifike 2025.

Wewe uliona wapi Duniani, Waziri hasikilizi Bunge! JK na Rostam ni watu hatari kwa usalama wa nchi.
Umenena kweli tupu kuhusu Jk.
 
Bora muendelee kuwa waongo lakini umeme uwake kuliko wakweli huku kitaa tupo gizani
 
January Makamba sasa ndiye waziri wa nishati na umeme, huku kusini wale KANGOMBA wanafanya shughuli zao.

Korosho inavunwa na kuuzwa bila kutumia JWTZ
afufuke sasa
Umesikia bei huko.? Wakulima wanalia. Ndio utajua JPM alikuwa mwanaume.
 
Kwa sasa wamegundua kuwa hawakuwa wakiwaambia wananchi ukweli. Ndani ya mwezi huu Tu taarifa kuhusu makinikia, uhalali wa vyama kufanya mikutano na hili la bwawa la umeme zimetuonesha kwamba kipindi chote kile tulikuwa tunafungwa kamba za chuma.
 
Akiwa Clouds TV, waziri wa nishati January Makamba amesema bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere linaisha mwezi Juni mwaka 2024 na wameamua kwenda na uhalisia na hawaoni aibu kusema litaenda miaka miwili mbele kuliko tarehe iliyotarajiwa kwani kwa namna yoyote isingewezekana ile tarehe ilitangazwa awali.

Awali Makamba amesema bwawa limeanza kujengwa Disemba 2018 na mpaka 2021(awamu ya tano) lilikuwa limejengwa kwa asilimia 37 kwa miaka miwili na nusu lakini mwaka mmoja(Awamu ya sita) limefika asilimia 74.

Makamba amesema wameongeza usimamizi na wamebadilisha 'Project Management' na wametumia pesa zaidi kupitia Tanesco kuhakikisha unakamilika kwa viwango na ubora.

Makamba pia amesema wameweka vichwa vyao pale na watapoinua uwe umeisha hivyo mambo ya Bungeni wao hawayasikilizi bali wanasimamia mradi vizuri na hali ilipo ni nzuri.

Awamu iliyopita ilidhamiria kumaliza bwawa la Nyerere Juni mwaka huu wa 2022.

Kuhusu hali ya umeme nchini, Makamba amesema umeme unaozalishwa nchini ni megawatts 1700 na mahitaji ya juu ni megawatts 1500 hivyo nchi inajitosheleza.


Ila kweli kabisa hawa jamaa kuwaamini inabidi mtu ujitoe sanaa.

Kila siku akihojiwa anabadiri asilimia ambazo awamu ya tano ilikuwa imejenga bwawa hilo.

Lakini cha ajabu zaidi, kama amelikuta 37%, wao wamefikisha 74%, hilo ni ongezeko la 37% zingine kwa mwaka mmoja...Bwawa hilo kwa sasa limebakiza 26% liweze kukamilika kwa 100%...lakini hizo 26% zilizobaki,zinahitaji miaka miwili kukamilika.

Yaani ni hivi..
37%=mwaka mmoja.

26%=miaka miwili

Ngoja aendelee kutolisikiliza Bunge kama alivohaidi
 
Back
Top Bottom