Akiwa Clouds TV, waziri wa nishati January Makamba amesema bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere linaisha mwezi Juni mwaka 2024 na wameamua kwenda na uhalisia na hawaoni aibu kusema litaenda miaka miwili mbele kuliko tarehe iliyotarajiwa kwani kwa namna yoyote isingewezekana ile tarehe ilitangazwa awali.
Awali Makamba amesema bwawa limeanza kujengwa Disemba 2018 na mpaka 2021(awamu ya tano) lilikuwa limejengwa kwa asilimia 37 kwa miaka miwili na nusu lakini mwaka mmoja(Awamu ya sita) limefika asilimia 74.
Makamba amesema wameongeza usimamizi na wamebadilisha 'Project Management' na wametumia pesa zaidi kupitia Tanesco kuhakikisha unakamilika kwa viwango na ubora.
Makamba pia amesema wameweka vichwa vyao pale na watapoinua uwe umeisha hivyo mambo ya Bungeni wao hawayasikilizi bali wanasimamia mradi vizuri na hali ilipo ni nzuri.
Awamu iliyopita ilidhamiria kumaliza bwawa la Nyerere Juni mwaka huu wa 2022.
Kuhusu hali ya umeme nchini, Makamba amesema umeme unaozalishwa nchini ni megawatts 1700 na mahitaji ya juu ni megawatts 1500 hivyo nchi inajitosheleza.