Makampuni ya simu yadharau agizo la Serikali (TCRA)

Makampuni yamefuata agizo la Waziri Ndugulile kuwa Mb1 iwe tshs 1. Najua alikalishwa chini na kushauriwa kuwepo na ongezeko la bando na akalitekeleza.

Huu mtego amenasa na utamgharimu maisha yake yote ya kisiasa.

Nimelisema wazi hili ili wanasiasa wetu wajifunze kuwa siyo kika ushauri ni wa kukurupukia wanapaswa wajitafakari kabla ya maamuzi yeyote
 
Ndio umeongea nini sasa
Haujaelewa nini ?

Kwa kuweka hizo bei bado mitandao ipo within bei elekezi za bundle..., hizo bei nyingine tofauti, tofauti ilikuwa ni offers, Je unaweza kumlazimisha mtoa huduma atoe offer ?

Walikuwa wanatoa offer kuvutia wateja..., sasa kama pote ni level playing field kuna incentive gani ya kutoa offer ?

TCRA wakae tena na wadau kurekebisha upuuzi waliofanya
 

SWALI NI KWA NINI TCRA WALIKUBALIANA MAKAMPUNI YA SIMU KUIDHINISHA BEI ZA AJABU AJABU ⁉️
OMBI LANGU BODI YA TCRA IVUNJWE NA MENEJIMENTI KUPIGWA CHINI MARA MOJA.
 
Habari ya asubuhi wadau wote

Nawasalimia kwa Jina LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA[emoji1241]
 
Route za xvideos zitapungua. Waminye zaidi kubet online kuwe kugumu
 
Kwanini tusiwekeze kwenye Ttcl yetu bhanaa tuiudumie kupitia budget yaetu ya serikali tutimue ma kampun yote haya kichef chef
 
Haya mambo tujifunze kotoka kwenye sukari , sement, mafuta ya kula kwa mara zote bei zinapopanda serikali hutoa matamko yasiyo na msaada wowote kwa wananchi, n kama ili mradi ionekane wameongea ila matamko yao huwa hayana utekelezaji.
 
Hzo ni programming kijana , sio issue ya overnight, mpo fixed Sana na siasa hata kwenye mambo ya kitaalam Zaid
Programming gani zipo slow hivyo Mkuu ina maana tupo nyuma kiasi hicho daah...
 
Kwanini tusiwekeze kwenye Ttcl yetu bhanaa tuiudumie kupitia budget yaetu ya serikali tutimue ma kampun yote haya kichef chef
Monopoly na mawazo ya siasa za ujamaa kwa serikali yoyote huwa mwishoni hazileti tija na maendeleo. Mifumo, sheria thabiti, na regulatory entities makini ni moja ya vitu vitavyotusaidia kupiga hatua mbele zaidi, badala ya kuendelea kukumbatia mawazo, na siasa za ujamaa zilizoshindwa kitambo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…