MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Ni dhahiri kwenye hili la corona, Tanzania imeamua kutoendana na mataifa mengine duniani, yenyewe imeamua kupuuza hiki kirusi na kuendelea na maisha kama kawaida, bado wanasongamana kwenye vilabu vya pombe, kwa hili hakuna taifa lenye uhuru wa kuingilia maamuzi yao Watanzania maana wenyewe ni taifa huru. Hivyo hata wakijifia huko watajua wenyewe na kuzikana. Lakini changamoto inaibuka pale kwamba Tanzania sio kisiwa, ni taifa lenye ujirani na mataifa mengine, linachangia hata baadhi ya makabila kwenye mipaka yake.
Kwa hiyo, ina maana kwa namna moja au nyingine lazima raia wake wataingia na kutoka kwenye baadhi ya haya mataifa ambayo yameizunguka, hususan madereva wanaofanya kazi za usafirishaji wa mizigo. Lakini changamoto inakuja pale, kila mojawapo wa haya mataifa wameweka bayana lazima yeyote anayeingia apimwe, hamna njia ya mkato kwa hili., iwe kule SADC au EAC, lazima upimwe, na imetokea kwamba madereva wengi wa Tanzania wanagunduliwa kuwa na kirusi, kitu ambacho kinasababisha aibu kwa uongozi wa Tanzania maana huko kwao walishaaminisha raia wao hamna kitu kama corona.
Viongozi wao waliomba Kenya isiwe ikitaja uraia wa madereva wao kila inapowagundua na kirusi, Kenya ilizingatia hili na kuweka siri, kila ikipima na kumgundua muathirika wa Tanzania, imekua inampokeza kwenye mamlaka husika kimya kimya. Kingine walichokubaliana ni kwamba madereva wawe wanapimwa kwenye taifa wanakotokea na kupewa vyeti, ili ipunguze msongamano pale mpakani, kwamba akiibuka na cheti, hana haja ya kupimwa tena, anapita tu, ila wakakubaliana hata hawa wenye vyeti watakua wanapitiwa mara moja moja (random tests), sio wote ila anaibukiwa mmoja kati ya kama kumi vile na kupimwa.
Hii hapa ndio imeibua changamoto, maana madereva wanaibuka na vyeti, wengi wanaoshtukizwa na kupimwa wanakutwa na kirusi ilhali wana vyeti, sasa hapo inabidi wapimwe wote, hata kama una cheti chenye mihuri ya hadi ikulu, lazima upimwe tena, na ndio wanakutwa na kirusi balaa.
Rais wetu Uhuru ana jukumu la kuhakikisha usalama wa afya ya Wakenya, haijalishi nini wala nini, Tanzania wanune, walipuke, wabwatuke, wang'ake ukweli utabaki pale pale, lazima tuhakikishiwe usalama wetu, wao wafanye yao huko watakavyo, lakini kila anayeng'ang'ania kuvuka mpaka kuja Kenya lazima afuate sheria zetu na masharti.
Sasa sielewi makampuni yao ya usafirishaji yanakwama wapi, mbona wasiajiri madereva pande zote mbili, gari linafika na kupokezwa kwa dereva wa nchi ya pili, wanatupiana funguo, linapulizwa madawa na kila hatua zinachukuliwa. Hapo mbona tutaendelea kuheshimiana tu. Ni bayana Kenya ndiye jirani muhimu sana kwa Tanzania, ukipitia takwimu zao za biashara baina yao na majirani wote, utakuta Kenya ndiko wanauza mazao yao mengi, na ndio maana wao hupiga makelele sana kila pakiibuka mzozo, maana hata ukiangalia leo hii Uganda bado wanataja madereva wa Tanzania wanaogunduliwa na kirusi, ila hautaskia Watanzania wakililia Uganda, wanawaacha waendelee kutaja, ila kwetu wanalia sana.
Njia itafutwe ya kumaliza hii issue kabisa, aidha tuwekeane bandari kavu mipakani kila mtu abaki kwao, au madereva waajiriwe kwenye kila taifa la pili, lakini ukweli utabaki pale pale, lazima upimwe upimwe upimwe, hapiti mtu...kwa cheti au makaratasi ya kariokoo lazima upimwe.