Poleni Familia ya Hayati Maalim Seifu S. Hamad, Poleni watanzania wote na mimi nikiwemo kwa msiba huu mzito kwa taifa.
Hayati Maalim Seifu, ameondoka akiwa amekamilisha kazi yake sawa sawia, kaicha Zanzibar ikiwa moja na ya amani huku mashirikiano kati ya Watanzania waishio Zanzibar yakiwa yameimarika.Pia mashirikiano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar yakiwa bora kabisa katika masuala ya muungano ya pande mbili hizi za Jamhuri ya nchi hii.
Kwa kifupi Hayati Maalim Seifu ameondoka bila deni.
Hayati Maalim Seifu, Alale mahala pema peponi. Amina.