TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

Kila Mtu hupewa nafasi yake hapa Dunia..kuhudumu katika eneo flani kwa ruksa na Baraka zake Mungu.

Ndio maana ukimkuta rubani mzuri anajua namna ya kukwepa upepo mkali angani , kurusha ndege vizuri na hata kutua..

Dereva Mzuri anajua gear ya kilima kikali na hata tairi upepo anajua..Maalim alipewa Kibali tangu alipozaliwa Wete Pemba...Akawekewa haiba na Mvuto wa kipekee kabisa.

Hakika Watu Kama Maalim hawazaliwi kila mara na kama ingekua Rahisi hivyo basi tungeona wengi wamechipukia..Viomgozi wazuri huja na kupita Ni tangu enzi na enzi.

Maalim Alikua Mwamba, jabali kubwa lenye nguvu ya ushawishi isiyo na kifani, mwanaume wa shoka aliesimama imara hata asiyumbe katika miaka yake yote.

Angeweza kusema neno na likasambaa kama moto huyu alikua mtu Wa ajabu na wa kipekee sana.

eeh Mungu tunakushukuru kwa ajili ya mtu huyu...eehhh Mungu tunakushukuru kwa ajili ya tumbo alimolala mwanaume huyu
..eeeh Mungu asante kwa ajili ya maisha ya Maalim....


Maalim tunakuombea Allah Akupe kauli thabit...akupunguzie adhabu ya kaburi.....

Ulale ukijua wewe Ni Simba na Simba Hafi....Milele na Milele Maalimu wewe ni Mmoja tu na ndio wewe uliekufa leo.

Tutaonana asubuhi ile Njema..😪😪😪
 
Natazamma hapa TBC 1 leo ndio wanasema eti hayati Mwal.J.Nyerere alikuwa anamkubali sanaaaaaa hayaati Maalim Seif
Kweli siasa ni mchezo mchafu kumbe marehemu wa watu alikiwa ana historia nzuri nyuma ya siasa za vyama vingi

Kupitia siasa marehemu alionekana kama mchafuzi wa amaani kumbe alipigania maendeleo ya Zanzibar
 
Nimeumia Sana[emoji24]
Angefaidi japo miaka hii mitano jamani [emoji24]
Hakuna cha kufaidi Duniani.
Maalim hakuwa mgeni wa vyeo.
Alishakuwa Waziri Kiongozi, Makamu wa kwanza wa Rais awamu ya kwanza ya utawala Mohamed Shein

Aliyoyafanya yanatosha kama alimvyomkadiria Mwenyezi Mungu.
Apumzike kwa Amani[emoji120]
 
Innallillah..waina illayh..rajoun..M/Mungu amsameh ampumzishe kwa amani..

Tumefiwa!
 
Poleni Familia ya Hayati Maalim Seifu S. Hamad, Poleni watanzania wote na mimi nikiwemo kwa msiba huu mzito kwa taifa.

Hayati Maalim Seifu, ameondoka akiwa amekamilisha kazi yake sawa sawia, kaicha Zanzibar ikiwa moja na ya amani huku mashirikiano kati ya Watanzania waishio Zanzibar yakiwa yameimarika.Pia mashirikiano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar yakiwa bora kabisa katika masuala ya muungano ya pande mbili hizi za Jamhuri ya nchi hii.

Kwa kifupi Hayati Maalim Seifu ameondoka bila deni.

Hayati Maalim Seifu, Alale mahala pema peponi. Amina.
 
Ccm machinery wana PhD ya unafiki
Aisee ni kweli jamaa historia yake ni balaa, namsikiliza Abdulkarim Atik hapa TBC 1 anamuelezea Maalim hakika mimi mwenyewe najilaumu kwanini sikufatilia historia ya huyu jamaa

Mzee Atik anasema Maalim alikwenda Brunei akaonana na mfalme na alipewa dollar za kutosha lakini aliporudi Znz akakabidhi zile Pesa zote japo alikabidhiwa yeye kama yeye kwa matumizi yake binafsi.

Mzee Atik anasema kama ingekuwa ni Kenya bac Maalim angekuwa mwanasiasa Billionaire na kumbuka yy ndio muasisi wa baraza la wawakilishi in short kafanya mengi ndani ya Znz
 
Kila mtu atapeleka hesabu yake kwa muumba
Mungu ni wa kuogopwa sana
Ya Ulimwengu tuyapendayo tutayaacha
Tujiombee kifo Chema
Kifo ni cha kila mtu
Wote tutakufa lakini matendo yetu ndio hesabu tutakayoipeleka kwa Mola

Tuthamini Utu wa kila mtu kwani HUU USINGIZI WA MILELE NI WA KILA MMOJA
TUWE WANYENYEKEVU NA KUMUOGOPA MUNGU

Siasa kama siasa dah!
 
Back
Top Bottom