TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

hiyo ishu mbona maalim aliizungumzia kwenye kitabu chake
Ana kitabu aalitoa? Mbona mzee Atik hapa anasema alimwambia Maalim aandike kitabu lakini marehemu alikataa

In other word marehemu ameondoka na siri zake
 
Pole kwa waliofikwa na msiba, familia, ACT, CUF, CCM, Wazanzibari na watanzania wote kwa ujumla.
 
Siku moja watoto walienda mtoni kuchota majio, kufika mtoni wakamuona chura yuko kwenye maji, wakaanza kushindana kumrushia mawe wakitaka kujua nani mwenye shabaha zaidi....kwa huzuni yule chura akapaza sauti ya upole "Mchezo wenu ni mauti yangu".
 
Kweli corona ipo ila nilichogundua ikikupata usikimbilie hospital we kaa kwako upige nyungu za kutosha kama alivyofanya jiwe
 
Mwenyezi Mungu ndio anajua hatima ya mtu kufa/uhai, serikali hatuwalaumu kwa hili... hii ya kutokutangaza na kutilia mkazo hapa tutawalaumu, tuliona meya wa moshi akizuia watu kuingia mkutanoni na barakoa ...na hii taarifa nayo hamjaweka wazi nikipi kimemchokua ndugu yetu, mbaya zaidi tukiongea mwatuona wachochezi
 
Inna lillah wa inna ilayh rajiuun: Mwenyeezi mungu aiweke roho yako pahala pema peponi.

Kwanza pole ziende kwa Familia, ndugu, jamaa, Wazanzibari wote na wana ACT. Nimepokea taarifa kwa masikitiko makubwa sana, ila kwa kuelewa uwezo wa Maulana nimezikubali taarifa na kuzikumbatia huku nikijua leo Maalim katangulia na kwa kuwa KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI, yeye katangulia nasi tupo nyuma yake.

Maalim umeacha pengo kubwa si kwa Wazanzibari tu bali ni kwa Tanzania nzima na Afrika. Pengo kubwa linatokana sifa moja kubwa uliyokuwa nayo ya kutokuwa mchumia tumbo. Ulipigania haki za Watanzania bila kujali pesa, kwani kama vyeo ulishavipata na ungepata hata hicho cha urais Zanzibar kama ungewasahau wananchi. Hivyo sifa zako kubwa ni Tatu: Haki kwa wote, Demokrasia ya kweli na upendo katika kudumisha amani. Ulipambana lakini kikomo chako ni pale ulipoona amani inataka kupotea, uliwatuliza wananchi na kutafuta njia mbadala, ukijua kuwa mabadiliko bila vita yanawezekana.

Ulizungumza hata na adui yako aliyekutesa na kutesa wananchi kama kufanya hivyo kutaleta unafuu wa maisha kwa watu wako. Hukujali kuchekwa wala kubezwa kwa lile uliloliamini. Umefanya hivyo miaka nenda rudi, wakati mwingine ulifanikiwa lakini wakati mwingine ilionekana kama umedanganywa lakini yote uliyafanya kwa nia njema tu.

Kubwa kabisa ni kuwa umeonyesha njia, njia ya kule ulipotaka tufike, nayo ni IDIOLOJIA thabiti ya kuamini katika utu wa Mtanzania, Kuleta demokrasia ya kweli, Kujenga uchumi imara na kuondokana na siasa za kibaguzi. Hapa umetuachia urithi dhabiti na imara, na kubwa zaidi umefanya kazi kwa karibu sana na vijana ambao wameiva na wako tayari kuvaa viatu vyako. Kwa hayo Jina lako ndani ya mioyo ya watanzania litaishi mkilele, kwa vile tutayaishi maisha yako. Wazanzibari wataendelea kula na kufaidi matunda uliyoyaacha kama vile ni mti wa idiolojia unaomwagiliwa maji usiku na mchana.

Namalizia kwa kusema Kila nafsi itaonja umauti, Inna Lillah wa inna ilayh rajiuun. Maalim kwaheri, Mwenyeezi Mungu aipumzishe roho yako pahala pema peponi. Amen.
 
Pole kwa familia, ndugu na Jamaa, hakika kaacha pengo kubwa katika siasa za Tanzania.
 
R.I.P mzee wetu Maalim Seif. Ulipambana kudai haki ya wazanzibar. Mungu akupumzishe mahali pema peponi, Amin
 
Inna lillah wainna illaih rajiuun. Kapumzike Maalim, umetenda kadri ya uwezo wako. Mungu akupe kauli thabit.
 
Huu uzi acha tu nipite kimya nisicomment chochote maana...
Yote tumwachie Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, mwenye haki.
R.I.P maalim Seif mpambanaji uliyevuja jasho na damu kupambania haki ya Wazanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…