TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

Inna Lilah Wainna Ilayh Rajiun

Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko sana hii taarifa ya kifo cha Mwanasiasa huyu Mahiri sana TANZANIA Maalim Seif. Alikuwa mtu aliyeweza kuwaunganisha Wazanzibar.

Sijawahi kumlaumu hata kidogo kutokana na msimamo wake kwenye nyanja ya siasa.

Allah amlaze mahala pema. Wanapolazwa wema.

Ameen
 
Ni mtikisiko mkubwa Zanzibar, Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa ni siasa za Zanzibar na siasa za Zanzibar zilikuwa ni Maalim Seif kwa hakika.

Tuna msiba mkubwa lakini pia tuna mengi ya kusherehekea na kujifunza kutokana na ushawishi na umaarufu wa Maalim Seif. Ninayo mengi ya kusema lakini nashindwa nianzie wapi!

Kwa sasa itoshe kusema pole familia yake, pole Wazanzibari na pole Watanzania wote.
 
Halafu shida zaid kwa maalim sio umri pekee nadhani afya pia ilikua ishamsaliti vya kutosha, hili dubwana hata likitembea na Lowassa hakuna namna linapita naye mazima (kumradhi kwa watakaokwazika kwa hili)
 
Mimi nachosikitika walimu expose mzee wa watu katika ziara ya mwisho aliyofanya Mwanza na Chato. Serikali ilikuwa kwenye kukana ugonjwa na kumfanya watu kuogopa kujikinga kuvaa barakoa au kuwa distance na mzee ali act kama hakuna kitu. Haikuwa ziara ya lazima labda mzee angeambiwa stay safe home hali sio nzuri lakini too much political pressure haya ndiyo matokeo.

Sitaki kukufuru wala kulaumu kifo ila haya mambo yanazuilika halafu mengine Mungu ndio anajuwa. Kuna watu watasema siku yake imefika hapana mtu anayejinyonga na kamba huwezi kusema siku yake imefika. Mungu katupa akili ukiumwa nenda katibiwe huwezi kukaa home ukasema kama siku imefika basi.

Serikali please fungeni mashule mzuie mikusanyiko isiyo ya lazima na shughuli za kiuchumi zitaendelea kwa tahadhari, mnawakosea watu wenu, au nyinyi mna chanjo tayari mnaingiza watu wengine mkenge.
 
Back
Top Bottom