3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 5,350
- 15,426
Bwana alitoa na Bwana ametwa jina la Bwana lihimidiwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naikumbuka hiyoApumzike kwa amani mzee wetu na alipost kwenye twitter yake kuwa ana Corona Inalilah wainayilah rajoon
RIP Maalim usingekubali kushirikiana na MACCM huenda mpaka leo tungekuwa tunakula ugali, wapemba waliumia mno hawakujali maisha yao, mali zao walisimama haki ipatikane, wewe na mnafiki zito mkakubali maridhiano ya kugawana vyeo, hicho cheo hata hujakifaidi
Siasa za zanzibar zimezikwa rasm. Na Mwinyi ni mrith wa mzee baba bara 2025.Kufa kufaana, kuna watu wengine wanachekelea tumboni kwamba afadhali ili sasa walau wapumue pumue na siasa za Zanzibar.
nimehuzunika sana siku ya leo mwili wote umesisimuka baada ya kusikia kifo chake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kaingia mwenyewe kwenye mitq 18, unadhani jiwe afanyeje?. (Kajiinguza mwenyewe kwenye nyavu kwanini asivuliww?)
Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Maalim Seif amefariki ktk Hospitali ya Muhimbili. Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza siku 7 za maombolezo ya Kitaifa
Kupitia ukurasa wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atoa salamu za rambirambi
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina"
View attachment 1704550
Maalim Seif alizaliwa kutokana na familia ya wakulima wa kijiji cha Mtambwe, nje kidogo ya mji wa Wete, Pemba, katika Oktoba 22, 1943, Maalim Seif alivuka bahari ya mkondo wa Pemba kuja Zanzibar kuendelea na masomo ya sekondari kutoka 1958 hadi 1963.
Hakuweza kuendelea na masomo ya chuo kikuu pale alipotakiwa aende kusomesha katika shule za sekondari ili kujaza mapengo yaliowachwa na walimu wengi wa Kiingereza na wachache wa kizalendo baada ya Mapinduzi ya 1964. Wakati ule siasa kali za utawala wa mkono wa chuma ulishuhudia serikali ikitaifisha vikataa vidogo vya mashamba na nyumba za makazi za watu walioonekana maadui wa Mapinduzi ziliipelekea Zanzibar kuelezwa na nchi za Magharibi kama Cuba ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo, alifanikiwa kuchukua shahada ya kwanza ya Elimu, Sayansi ya Kisiasa na Uhusiano wa Kimataifa´kutoka mwaka 1972 hadi 1975 na aliporudi Zanzibar alichaguliwa msaidizi maalum wa Rais wa Zanzibar mpaka mwaka 1977 alipochaguliwa Waziri wa Elimu.
Katika medani ya siasa Maalim Seif alichaguliwa mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo aliitumikia kwa miaka 11. Katika mwaka 1984 kufuatia kile kilichojulikana kama kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Visiwani kulikoshuhudia kulazimishwa kustaafu kwa aliyekuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe, Maalim Seif alichaguliwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Lakini kauli zake za uwazi za mara kwa mara za kuonyesha hafurahishwi na mwenendo mzima wa Muungano na kueleza Zanzibar haitendewi haki kwa baadhi ya mambo ndani ya Mungano kuliepelea kutimuliwa katika chama na pia kupoteza wadhifa wa Waziri Kiongozi kufuatia hatuahio ya chama.
Tokea wakati huo aliandamwa kwa kuonekana tishio la kisiasa na mwaka 1989 alifunguliwa mashitaka bandia ya kupatikana na nyaraka za siri za serikali. Alikaa miaka miwili gerezani, baadhi ya wakati katika chumba akiwa peke yake kwa muda unaoweza kufikia wiki mbili mpaka alipoachiwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa kuwa hakuwa na kesi ya kujibu.
Tanzania ilipofungua milango yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Maalim Seif na baadhi ya wenzake aliofukuzwa nao Halmashauri Kuu ya CCM walikuwa miongoni ma walioanzisha Chama chaWananchi (CUF) na kuwa Makamo Mwenyekiti wake wa kwanza
Aligombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, mwaka 2000, 2005, 2010,2015 na 2020, Alishindwa kwa kura chache, lakini mwenyewe amekuwa akiamini alishinda chaguzi zote hizo na aliporwa ushindi kwa sababu Tanzania na hasa Zanzibar haijakuwa tayari kupokea mfumo wa demokrasia kwa moyo safi.