Ni mtikisiko mkubwa Zanzibar, Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa ni siasa za Zanzibar na siasa za Zanzibar zilikuwa ni Maalim Seif kwa hakika.
Tuna msiba mkubwa lakini pia tuna mengi ya kusherehekea na kujifunza kutokana na ushawishi na umaarufu wa Maalim Seif. Ninayo mengi ya kusema lakini nashindwa nianzie wapi!
Kwa sasa itoshe kusema pole familia yake, pole Wazanzibari na pole Watanzania wote.