Sasa Hivi Wasomi wanazidi kuwa Wengi wajinga Wanapungua Kwa Kasi na Serikali ndio hiyo Inazidi kujenga Madarasa hata Kama Haijui Itawapeleka wapi hao wasomi inaowajengea madarasa
Waumini wenu wanaokuja Makanisani (wale wenye Akili Timamu) Wanaona Jinsi gani Mnavyoyaendesha Makanisa Bila Wao Kufaidia Directly na hizo pesa Mnazosema Mnampelekea Mungu wakati ukweli ni Kwamba Hazifiki kwa Mungu bali mnazipigia Bajeti zenu za Kujinufaisha Au Kutengeneza Future Za Maisha Na Makanisa Yenu na Kuanzisha Miradi ambayo haimnufaishi Muumini Directly
Hakuna Siri kwamba Makanisa Hapa Nchini yamekuwa yakikusanya Michango.. Sadaka.. Shukrani..Harambee...Bahasha...Michango ya Redio...n.k Milioni na Bilioni kwa Mwaka Zinakusanywa Katika Makanisa. ila Msaada kwa Waumini kama Waumini husika haiendi Directly Kitu ambacho Kinasababisha hata Watu kuona Wanachotwa Mifukoni kwa Kisingizio cha Watabarikiwa au Wanamtolea Mungu
Mfano 1: Leo hii Muumini Apate Ugonjwa au Kuzeeka Asijiweze. Kanisa Linakaa Pembeni waumini ndio wachange Tena Pesa katika Jumuiya zao Na Pengine Asipoudhuria Misa au Jumuiya ingawa Ni Muumini Aliyekuwa Anachangia Anapotezewa kama Vile ni Mpagani tu
Katika Vikundi mbalimbali hapa Nchini Watu wanachanga Pesa Na wanauliza Zitawanufaisha Vipi wao kama Wao either wakiwa Wameugua Au Wakiwa Na Sherehe au Kifo. Kitu Ambacho waumini Ambao wamepumbazwa Wanashindwa Kuulizia Sadaka na Michango yao Kanisani itawasaidia nini Katika maisha Mmoja Mmoja.
Wameambiwa Sadaka Ni Za Mungu wakati Wakishazitoa Wanaona Majengo, viwanja, Mashule na Mahospitali yanajengwa bila Wao kuwapewa hata Asilimia moja Ya Mapato kutoka Katika Vyanzo hivyo.
Na Wakijaribu Kupeleka Watoto au Wao wenyewe wanakutana Na Bei ambayo hata Asiyemuumini Anatozwa hiyo hiyo Pesa haijalishi.
Fungukeni Macho Mnapigwa kwa Kivuli cha Mnamtolea Mungu. Hii Siri Baada ya Wengine Kuijua Wameamua na Wao kufungua makanisa kwa Kasi na Wanaendelea Kupiga Pesa maana Waumini akili timamu Hazipo Zimeshafubazwa kwa Kuambiwa Mungu ndie Anayetolewa
Wakati Huyo Mungu kwanza Haitaji kitu chochote kile Kutoka Kwako maana Hana Mapungufu kama Wewe ulivyo. Yeye kakamilika Haitaji sadaka wala Dhabihu wala Kitu Chochote kutoka Kwako maana Huwezi Mlipa Chochote.
Umekuwa Muumini Wa Muda Mrefu mpaka Unazeeka Hapo. Kanisa Lako halina hata Account ya Kusaidia Waumini wake wanapopatwa na Matatizo. Hivi hamuoni Mmechanganyikiwa na Mnaendeshwa Kunufaisha Watu. Kazi yako ni Kupeleka Fungu la Kumi kanisani ambalo wenye Nalo wanaenda Kuweka Mabati kwenye Miradi ya Kanisa
Jisaidieni Nyie kwa Nyie. Pelekeni Fungu la Kumi mnalotoa huko Kanisani kwa Watu wenye Mahitaji maana Mungu ndio kawaumba Hivyo ,msaidianeni Nyie kwa Nyie si kumpelekea Binadamu mwenzako Pesa Halafu Yeye anakuhadaa eti Unampa Mungu.
Chukueni Pesa zenu Pelekeni wagonjwa..Pelekeeni Watoto Yatima Wanautunzwa Na Watu..wasaidieni wazee walio majumbani Hawana Uwezo wa Kujipatia Vyakula Wakat kanisa lako hilo Likisubiri Afe ili Lije Limpe Upako Tu na Kumzika na likimkuta Haudhulii Misa Linamuacha
Mtu anapata Ajali ya Gari tena Unakuta ni Mahala pa Kijijini anaokolewa na Mwanakijiji hapo anamuwahisha Hospitali anapatiwa matibabu. Halafu kwa Sababu Akili timamu hana anachukua Pesa anaenda Kutoa Shukurani kwa Mchungaji au anapeleka Sadaka Ya Shukurani kanisani. Aliyemuokoa Kule Kijijini na Hospitali waliomtibu hawakumbuki
Hivi wewe unategemea utabarikiwa wewe. Au ndio mabalaa ya Maisha Yatakuandama. Yaani Yule Mwanakijiji aliyekutoa Kwenye Gari na Kukuokoa Hana Maana Na Sometimes alikuwa anajipitia Tu ..kwanini Usiende Kumpa Yule na Hao wa Hospitali waliokusaidia Ukapona Wangekuacha Je Huyo mungu wa Huko Kanisani na Kwa Mchungaji wako angekuja Kukupeleka hospitali. Tujitambue Wana Ndugu tumepotoshwa sana na Tumepotoka Kweli kweli
Tutumie Akili Timamu na Tumwabudu Mungu asiyetaka Vitu bali Aliyeumba Vitu vyote bila Yeye Kukutaka Kitu Chochote kile kutoka Kwako. Huyo ndio Mungu wa Kweli hana Mapungufu ya Kutaka Taka Vitu. Si Kama ukimnyima Anakuchukia na Kukupa Mabalaa hapa Duniani hakuna Mungu wa Hivyo
Asanteni