Makanisa Nchini Mjitafakari

Mleta mada ameshauri fungu la kumi na shukurani zetu tuzipeleke moja kwa moja kwa wasio jiweza. Kanisani zinawanufaisha wenye uwezo kwa kufungua miradi isiyo na msaada kwa wenye uhitaji...

#tuamkekanisanitunapigwanakitukizitodeile
Jisaidieni Wenyewe kwa Wenyewe acheni kupeleka vitu Vinavyoenda Nufaisha Watu. Mtu kakutendea mema mpelekee huyo mtu zawadi na Mshukuru. Pesa zenu Zipelekeni kwa Wahitaji maana Wao ndio wanaona Kweli nimepewa na Mtu

Haya makanisa Hata Leo ukienda Huko kwa Wahitaji na Masikini hawajui wamepewa lini misaada zaidi ya Waumini hao hao ndio tena Wawasaidie masikini wenzao

Hatujawahi kuwaona Hao wachungaji wala mapadri wakipanga Foleni Kwenye mahospitali makitoa Misaada zaidi ya Kujilimbikizia mali na Kwenda kuanzisha Miradi mikubwa mikubwa ili Taasisi zao ziendelee kuwa Hai. Hata Siku mkiwakimbja Watabaki na Miradi mikubwa mikubwa bila Shida ya Chakula ndani na Watoto wao
 
Bwana hapokei kitu maana Hana Mikono na Wala Mungu haitaji hayo wanayofanya. Wameandika hivyo ili Ukapigwe vizuri huko

Mungu haitaji Shule
Mungu haitaji Chuo
Mungu haitaji Benki
Mungu haitaji Majengo

Hayo yote Ni mahitaji yako wewe binadamu sasa Akuombea Sadaka yako ya Nini wakati hana Mahitaji ya Kibinadamu wanayofanya hao Wachungaji na Mapadri huko

Sasa Hizo sadaka Wanazosema Za Mingu ila Tunaona Zinafanya Mahitaji ya Kibinadamu
 
Kupitia binadamu unamuona Mungu.
Asamsaidiae mhitaji umkopesha Mungu nae atamlipa mara nyingi yake.
Hii kanuni wanaijua wazungu thus kadri wanavyotupa misaada zaidi ndivyo wao wanavyotajirika zaidi.
 
Nijitolea kwa hali na mali kujenga shule moja ya kanisa mkoa fulani,Cha kushangaza nilimaliza chuo nilienda kuomba kazi pale NIKAKOSA nafasi walipewa Ndugu,na watoto wa wachungaji.Niliumia sana mpka leo nishabadili mfumo.
Hayo ni madhaifu ya wanadamu
 
DAAH!!
FIRST WE MUST COLONIZED OUR MIND ,
ukweli mchungu aisee...
Ngoja nijitafakari na nichukue hatua....
Mkuu hii comment ndio imenileta wala sijasoma tittle. Kweli tupambane wanetu wasome hizo shule za gharama tunazojenga kwa michango
 
Hali hiyo unayoisemea kama iko makanisani peke yake ila kwenye misikiti na mahekalu waumini wakitoa sadaka zinawarudia swala ni dogo tu ni kuachana na makanisa unajiunga huko kwingine ambapo ukitoa sadaka zitakuwa zinakurudia.
 
Unaonesha unaposali wewe ndio pana majanga usijumlishe makanisa yote ndugu, hama ukiona uoni faida ya sadaka yako au amia kabisa din nyingine ambayo hawatoi sadaka
 
Hali hiyo unayoisemea kama iko makanisani peke yake ila kwenye misikiti na mahekalu waumini wakitoa sadaka zinawarudia swala ni dogo tu ni kuachana na makanisa unajiunga huko kwingine ambapo ukitoa sadaka zitakuwa zinakurudia.
Ungeweka Zinavyorudi ungesaidia
 
Ukiona mtu anasononeka kama wewe ujue maisha yako ni magumu sana, usilalamikie kanisa lalamikia serikali kupandisha bei vitu, ndio jibu lako msisingizie makanisa coz miaka na miaka yapo hivyo hivyo wewe nani umezaliwa juzi tu eti unaliwa??!! Unajitafutia laana ungehama tu amia din nyingine ambayo haitoi sadaka
 
Maisha yakiwapiga msikimbilie kusema makanisa, huo ni mfumuko wa bei shughulikeni na serikali zenu, au hamia din nyingine ambayo hawatoi sadaka
 
Badala mpambane na serikali zinazopandisha bei kila kitu eti mnapambana na kanisa ni dhambi yaani maisha yawachape eti sadaka tunaliwa??!!makanisa yapo miaka na miaka leo wewe umezaliwa juzi unatoa maneno kama hayo🙄🙄🙄 pambaneni na serikal zinazoongeza matozo hizo ndio zinafanya muone kanisa linakula hela mnatia aibu na umasikini wenu visadaka vyenu vitawapeleka wapi ??! Badilika wewe ni aibu hama amia fin ambayo haitoi sadaka usilalame tuu
 
Hiki kiingereza chako dada kimefanana sana na cha yule the dedi "ankali" wa chattle.
Mwenyewe hiki kiingereza changu sikielewi ...
Yaani hata cjui nimeamdika nini [emoji848][emoji23][emoji23][emoji28][emoji23][emoji23]
NB: Nimesomea shule ya kanisa na msikiti.

Au cjasoma. Au .......
 
Nyie bado mmepumbazwa. Hiyo serikali ingekuwa inakukata Kodi Halafu haijengi Barabara na Kukuwekea Huduma za Afya nahisi akili yako ingekaa sawa. Usisingizie watu wana Maisha magumu kwa Kuhisi hisi kwenye mada Hatujaweka Akaunti zetu za Benki na miradi ungeona Nani ni Masikini na Mwenye maisha Magumu.

Kinachoongelewa hapa Kikae Akilini mwako ujue Unaibiwa kwa Kupumbazwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…