Makanisa Nchini Mjitafakari

Makanisa Nchini Mjitafakari

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
1,486
Reaction score
1,874
Sasa Hivi Wasomi wanazidi kuwa Wengi wajinga Wanapungua Kwa Kasi na Serikali ndio hiyo Inazidi kujenga Madarasa hata Kama Haijui Itawapeleka wapi hao wasomi inaowajengea madarasa

Waumini wenu wanaokuja Makanisani (wale wenye Akili Timamu) Wanaona Jinsi gani Mnavyoyaendesha Makanisa Bila Wao Kufaidia Directly na hizo pesa Mnazosema Mnampelekea Mungu wakati ukweli ni Kwamba Hazifiki kwa Mungu bali mnazipigia Bajeti zenu za Kujinufaisha Au Kutengeneza Future Za Maisha Na Makanisa Yenu na Kuanzisha Miradi ambayo haimnufaishi Muumini Directly

Hakuna Siri kwamba Makanisa Hapa Nchini yamekuwa yakikusanya Michango.. Sadaka.. Shukrani..Harambee...Bahasha...Michango ya Redio...n.k Milioni na Bilioni kwa Mwaka Zinakusanywa Katika Makanisa. ila Msaada kwa Waumini kama Waumini husika haiendi Directly Kitu ambacho Kinasababisha hata Watu kuona Wanachotwa Mifukoni kwa Kisingizio cha Watabarikiwa au Wanamtolea Mungu

Mfano 1: Leo hii Muumini Apate Ugonjwa au Kuzeeka Asijiweze. Kanisa Linakaa Pembeni waumini ndio wachange Tena Pesa katika Jumuiya zao Na Pengine Asipoudhuria Misa au Jumuiya ingawa Ni Muumini Aliyekuwa Anachangia Anapotezewa kama Vile ni Mpagani tu

Katika Vikundi mbalimbali hapa Nchini Watu wanachanga Pesa Na wanauliza Zitawanufaisha Vipi wao kama Wao either wakiwa Wameugua Au Wakiwa Na Sherehe au Kifo. Kitu Ambacho waumini Ambao wamepumbazwa Wanashindwa Kuulizia Sadaka na Michango yao Kanisani itawasaidia nini Katika maisha Mmoja Mmoja.

Wameambiwa Sadaka Ni Za Mungu wakati Wakishazitoa Wanaona Majengo, viwanja, Mashule na Mahospitali yanajengwa bila Wao kuwapewa hata Asilimia moja Ya Mapato kutoka Katika Vyanzo hivyo.

Na Wakijaribu Kupeleka Watoto au Wao wenyewe wanakutana Na Bei ambayo hata Asiyemuumini Anatozwa hiyo hiyo Pesa haijalishi.

Fungukeni Macho Mnapigwa kwa Kivuli cha Mnamtolea Mungu. Hii Siri Baada ya Wengine Kuijua Wameamua na Wao kufungua makanisa kwa Kasi na Wanaendelea Kupiga Pesa maana Waumini akili timamu Hazipo Zimeshafubazwa kwa Kuambiwa Mungu ndie Anayetolewa

Wakati Huyo Mungu kwanza Haitaji kitu chochote kile Kutoka Kwako maana Hana Mapungufu kama Wewe ulivyo. Yeye kakamilika Haitaji sadaka wala Dhabihu wala Kitu Chochote kutoka Kwako maana Huwezi Mlipa Chochote.

Umekuwa Muumini Wa Muda Mrefu mpaka Unazeeka Hapo. Kanisa Lako halina hata Account ya Kusaidia Waumini wake wanapopatwa na Matatizo. Hivi hamuoni Mmechanganyikiwa na Mnaendeshwa Kunufaisha Watu. Kazi yako ni Kupeleka Fungu la Kumi kanisani ambalo wenye Nalo wanaenda Kuweka Mabati kwenye Miradi ya Kanisa

Jisaidieni Nyie kwa Nyie. Pelekeni Fungu la Kumi mnalotoa huko Kanisani kwa Watu wenye Mahitaji maana Mungu ndio kawaumba Hivyo ,msaidianeni Nyie kwa Nyie si kumpelekea Binadamu mwenzako Pesa Halafu Yeye anakuhadaa eti Unampa Mungu.

Chukueni Pesa zenu Pelekeni wagonjwa..Pelekeeni Watoto Yatima Wanautunzwa Na Watu..wasaidieni wazee walio majumbani Hawana Uwezo wa Kujipatia Vyakula Wakat kanisa lako hilo Likisubiri Afe ili Lije Limpe Upako Tu na Kumzika na likimkuta Haudhulii Misa Linamuacha

Mtu anapata Ajali ya Gari tena Unakuta ni Mahala pa Kijijini anaokolewa na Mwanakijiji hapo anamuwahisha Hospitali anapatiwa matibabu. Halafu kwa Sababu Akili timamu hana anachukua Pesa anaenda Kutoa Shukurani kwa Mchungaji au anapeleka Sadaka Ya Shukurani kanisani. Aliyemuokoa Kule Kijijini na Hospitali waliomtibu hawakumbuki

Hivi wewe unategemea utabarikiwa wewe. Au ndio mabalaa ya Maisha Yatakuandama. Yaani Yule Mwanakijiji aliyekutoa Kwenye Gari na Kukuokoa Hana Maana Na Sometimes alikuwa anajipitia Tu ..kwanini Usiende Kumpa Yule na Hao wa Hospitali waliokusaidia Ukapona Wangekuacha Je Huyo mungu wa Huko Kanisani na Kwa Mchungaji wako angekuja Kukupeleka hospitali. Tujitambue Wana Ndugu tumepotoshwa sana na Tumepotoka Kweli kweli

Tutumie Akili Timamu na Tumwabudu Mungu asiyetaka Vitu bali Aliyeumba Vitu vyote bila Yeye Kukutaka Kitu Chochote kile kutoka Kwako. Huyo ndio Mungu wa Kweli hana Mapungufu ya Kutaka Taka Vitu. Si Kama ukimnyima Anakuchukia na Kukupa Mabalaa hapa Duniani hakuna Mungu wa Hivyo


Asanteni
 
Ni Lini Watoto Wa Waumini wa Kanisa Walio Vijijini watasoma Katika Hizo Shule Zenu zinazofaulisha Division 1?

Wakati wakiwa Wanatoa Sadaka na Michango ya Shukurani, Na Harambee na Michango Mingine ya Kutegemeza Sijui nini wanaambiwa Inapelekwa Jimboni sijui inaenda Wapi. Sasa Mbona Mkishaanzisa Hizo shule Zenu mnakaribisha Matajiri na Wenye Pesa Ndio wakasome humo wakati waumini wenu Watoto wao Hawajiwezi na Wamekaa Bila Elimu Bora!
 
Ni Kama kuna ujumbe fulani Unataka kuufikisha lakini kwa andiko hili wengi watapoteza mwelekeo!

Mungu Katika Biblia ameagiza 'Nitoleeni Fungu la Kumi sababu hiyo ni haki yangu, na akaongeza nijaribuni Kwa njia hiyo Muone kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni.

Kuna sehemu ameagiza 'pandeni juu milimani mkalete miti mnijengee Kanisa.

Yote hayo ili Jina Lake Litukuzwe.

Ukitafakari Hayo Utagundua Michango na Sadaka kwa Mungu siyo Hiari ni Lazima.

Nafikiri shida yako mtoa Mada ni Baadhi wa wanaokusanya hiyo michango na Sadaka Hawatumii kwa Malengo Yaliyokusudiwa.

Ushauri : Wewe Hapo Ulipo Ukiona Sadaka zako Zinapigwa. Hama tu.
 
Viongozi wengi wa makanisa wanaishi maisha bombastic sana huku waumini wao, waleta sadaka, ni chokest mbaya sana.
Ndio mnatakiwa mjiulize kama Waumini mmepumbazwa vya Kutosha Maana Mlikuwa hamna Cha Kusimamia wala Kuhoji. Na Waliwaambia Ukihoji unamkufuru Mungu na Utalaaniwa wakijua Ndio Njia Nzuri ya Kuwateka Watu

Ni mipango yao Ili wamiliki hii Dunia ila Mungu wa Kweli atawaumbua Vibaya sana maana Watu wenye Akili timamu watakuja Kuwaumbua sana
 
Mengine yanafungua mabenki ya kibiashara, viongozi wa haya makanisa wamekuwa hawana aibu kubebesha waumini wao mizigo mizito wasiyoweza kubeba wao wenyewe, wanajenga mashule, vyuo na mahospitali ambayo waumini wao hawanufaiki kwa kutoa michango yao
 
Mtoa mada hama kanisa ulilomo.
Kumbukumbu la torati
Maagizo kuhusu fungu la kumi
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; 25ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; 26na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la mavuno yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; 29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
 
Ni Kama Kuna ujumbe fulani Unataka kuufikisha lakini kwa andiko hili wengi watapoteza mwelekeo..!
Mungu Katika Biblia ameagiza 'Nitoleeni Fungu la Kumi sababu hiyo ni haki yangu, na akaongeza nijaribuni Kwa njia hiyo Muone kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni.!
Kuna sehemu ameagiza 'pandeni juu milimani mkalete miti mnijengee Kanisa...!
Yote hayo ili Jina Lake Litukuzwe.
Ukitafakari Hayo Utagundua Michango na Sadaka kwa Mungu siyo Hiari ni Lazima...!
Nafikiri shida yako mtoa Mada ni Baadhi wa wanaokusanya hiyo michango na Sadaka Hawatumii kwa Malengo Yaliyokusudiwa...!
Ushauri : Wewe Hapo Ulipo Ukiona Sadaka zako Zinapigwa ...Hama tu.
Mleta mada ameshauri fungu la kumi na shukurani zetu tuzipeleke moja kwa moja kwa wasio jiweza. Kanisani zinawanufaisha wenye uwezo kwa kufungua miradi isiyo na msaada kwa wenye uhitaji...

#tuamkekanisanitunapigwanakitukizitodeile
 
Nikawaza sana eti nitoe elfu 20 ya sadaka kanisani wakati ndugu yangu kule kijijini hali yake ngumu wengine wanasoma kwa tabu, nikasema alie juu anaona mpaka moyoni mwangu , basi nikatuma 18 kijijini elfu 2 ibaki kanisani na hii policy ni mpaka kesho nasaidia wenye uhitaji kwa hali na mali, Kanisani tupo wengi nisipotoa mimi atatoa mwingine.
 
Kama jehanamu ipo kweli ! Walio na Makanisa wataungua sanaaaaa. Makanisa ni Biashara za watu wenye kuwatumia maskini na matajiri kujiongezea kipato. Yapo Makanisa machache sana viongozi wao wataiona mbingu. Haya ya walokole hakuna hata moja litasalia yataungua kama mti mkavu.. kwani ni wachafu kuliko mnyama....hawana tofauti na waganga wa kienyeji..
 
Tukirudi kwenye fikira dini zote tulizo nazo ni dini za mchongo tuu ni vile tuu tumezaliwa na kukuta wakubwa wetu wanaabudu.

Fikiri kabla ya biashara ya utumwa watu walikua hawajui uislam africa.

Fikiri kabla ya kuja wazungu watu walikua hawajui ukristo africa.

Je walioishi kabla hukumu zao zikoje.

Jambo tafakarishi tunaomba kwa pamoja juu ya kinga fulani ila hilo hilo jambo lina kwenda tupata, mfano ufaulu, nafuu ya mgonjwa, ajari.

Kikubwa tuishi kwa kuwajari wenzetu, tutende yaliyo mema.
 
Kumbukumbu la torati
Maagizo kuhusu fungu la kumi
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; 25ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako; 26na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la mavuno yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; 29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Kaa chini na Akili yako Mwenyewe Jiulize aliyeandika Hayo ni Nani! Kama Yameandikwa na Binadamu mwenzako basi Jua Umepigwa.

Na ukisoma.Mstari mpaka Mstari utajua Ni maandiko ya Kibinadamu mwenye Tamaa ya Mali mpaka anasema Mwenyewe kabisa huyo Mwandishi Kwamba hizo Sadaka kama Ni Nzito Basi Zibadili ziwe Pesa halafu zipeleke na Ukishazipeleka Yeye atatumia Kama Roho yake inavyo penda


Mungu hajawahi andika chochote kile wala Kumwambia Mtu aandike Kitu
 
Huu ujumbe uwafikie kina mwa. Nimewahi uliza hili vipi muumini masikini ananufaika vipi kiuchumi akijiunga na dhehubu lake. Inatakiwa madhehebu yaanzishe vyuo vya ujuzi kupitia sadaka na michango ya waumini kisha waumini masikini wasome wapate ujuzi Ili wazalishe kisha watoe sadaka. Nyumba za ibada zichunge watu kiroho na kiuchumi. Hata maandiko usema usiende nyumbani mwa Bwana mikono mitupu.
 
Back
Top Bottom