new forest
Member
- Mar 28, 2024
- 35
- 97
Habari Wana JF?. Hii ni true story kabisa. Kuna familia ya jirani yangu imesambaratika sababu ya MAKANISA ya KILOKOLE japo kisa kilianzia mbali sana. Mume mtu alikuwa anamtuhumu mkewe kuwa kwenye ukoo wao kuna mkosi WA wanawake kufiwa na waume zao.
Katika familia ya huyo mke mtu, kuna wanawake sita na wanne kati Yao walishafiwa na waume zao kasoro huyo mke mtu ninayemzungumzia na mdogo wake WA mwisho tu, ila dada zao wote waume zao walishafariki Kwa sababu mbalimbali wengine Ajali, magonjwa nk.
Sasa mume mtu alipoona Hilo swala akaingia na wasiwasi akamuuliza mkewe mbona kwenu kuna kasumba ya wanawake kufiwa na waume zao isije ikawa Mimi ndo nafwata coz ikumbukwe katika familia ya mke mtu walikuwa wamebaki wawili tu ambao sio wajane.
Mume mtu akamuomba mkewe waende Kwa mganga au wakafanye Mila kijijini Ili kama kuna mkosi kwenye familia Yao wamtafute suluhisho.
Lakini mke mtu sababu ni mlokole na amshika dini kupita maelezo, akakataa katakata kutafuta suluhisho la tatizo Hilo Kwa waganga au kufanya Mila. Kwanza akamwambia mumewe kuwa yeye anaamini kwao hakuna mikosi yoyoye na hata hao dada zake wajane , waume zao walikufa vifo vya kawaida kama wanadamu wengine tu.
Jambo hili lilimkasirisha sana mume mtu, na akaona mkewe kama anachukulia poa suala la kifo sabubu tu kashika dini kupita kiasi.
Isitoshe mke alishahama kanisa katoliki walilokuwa wanasali, na kahamisha watoto wote kwenda hilo kanisa la KILOKOLE japo watoto ni wakatoliki pia, walibatizwa, walipata komunio na kipaimara. Jambo hili lilimkasirisha sana mume mtu baye ni mkatoliki mzuri na kiongozi kwenye jumuiya.
Hivi sasa ninavyozungumza ndoa hiyo imekufa.
MAKANISA ya KILOKOLE ni HATARI sana hasa Kwa akina mama na watu ambao hawana elimu ya kutosha kuchanganua mambo Kwa jicho la tatu.