Makao makuu ya wilaya ya Iramba, Mwigulu anahusika

Makao makuu ya wilaya ya Iramba, Mwigulu anahusika

TAMISEMI ikatae huo ujinga! Kwani majengo yakiwa ya serikali kuu yana shida gani? Hayo watakayojenga hapo Misigiri wameshindwa nini kuyajenga huko huko Kiomboi?
Wenye akili kama hizi wako tu huku Nangunde?
 
Kwani Shida nini? Mfano Mbona Makao
Makuu ya Nchi yemehamishiwa Dodoma lakini Mji wa dar unaendelea ku shine na Vilevile Mji wa Dodoma unaendelea Kushine nakuifanya Miji yote kuwa Bambam. Kukuza Miji Midogo siyo hasara ila ni faida kwa Halmashauri na Mkoa Husika.
Hizi Hisia za Kwamba Mji unahamishwa hakuna kinachohishwa ila Majengo ya Ofisi ndo yanahamia huko.
Hata majengo ya ofisi pia hayahami bali ofisi (watu, documents na mafile)ndiyo huhama.
Wanakohamia ndiyo hujengwa majengo mapya ya ofisi ama kupanga.
 
Sasa hapo kiomboi pana nini cha maana si afadhali ya misigiri nyie wanyira vipii
 
Hoja sio kuchangamka bali kutoshirikishwa wananchi.
Siyo kila jambo la serikali ni kushirikisha wananchi mambo mengine yanahitaji maamuzi tu faida mtakuja kuiona huko mbeleni. Mambo ya kuchelewesha maendeleo hayana mjadala.
 
Kuna sababu nyingi za maana kuhamisha makao makuu ya wilaya kutoka kiomboi kwenda misigiri! ni mwenye nia ovu na iramba tu ndiye atakayepinga wazo hili!
 
Back
Top Bottom