Makapuku Forum

[emoji599] Azizi KI gari imewaka, ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kuwa kwenye kiwango kikubwa ambapo kwenye mchezo wa KMC ndiye aliyewafanya viungo na mabeki wa KMC kupoteana kwa kazi yake ya kutawanya mipira na hata kasi yake kuelekea lango la wapinzani akishirikiana na Pacome, ambaye tachi zake zilikuwa ni za ‘mwana ukome’.
 
Kitu ambacho Yanga iliwapa shida wageni wao KMC ni mfumo wao wa kukaba kwa nguvu na kunyang’anya kwa haraka mpira kutoka kwa wapinzani wakihakikisha wapinzani wao hawasogei kwenye eneo lao la hatari.
.
Hatua hiyo iliwapelekea KMC muda mrefu kushindwa kutoka katika nusu uwanja yao na walipojaribu kuvuka kwenda nusu ya Yanga walipoteza mpira kwa haraka. KMC ilionekana kupata shida katika dakika 30 za kwanza ambapo hawakufanikiwa kufika eneo la hatari la Yanga kwa shambulizi lolote.
.
Wageni hao walifika kwa mara ya kwanza eneo la hatari dakika ya 31 kwa krosi ya beki wao wa kushoto Rahim Shomari akimtafuta mshambuliaji wake Sadala Lipangile lakini hata hivyo beki Dickson Job aliidhibiti kirahisi.
 
[emoji408] VIDUME WATATU

3/2—NI makocha watatu tu ndio walioshinda mechi zao zote mbili za ufunguzi wa msimu huu wa Ligi Kuu England.
.
[emoji736] Pep Guardiola (Manchester City)
[emoji736] Mikel Arteta (Arsenal)
[emoji736] Roberto De Zerbi (Brighton)

 
[emoji599] Kylian Mbappe amepigwa chini na wachezaji wenzake kwenye mchakato wa upigaji kura kuchagua nahodha mpya wa mabingwa hao wa Ufaransa, Paris Saint-Germain. Kocha wa miamba hiyo, Luis Enrique aliwaambia wachezaji wake anahitaji nahodha mpya wa kikosi chake kwa ajili ya msimu huu na kuwataka wachezaji hao kupiga kura kwa siri kumchagua anayefaa na hapo ndipo jina la Mbappe lilipokatwa, wakilitupa mbali kabisa.
.
Na kwenye mchakato huo, Mbappe aliishia kushika namba nne kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la RMC Sport. Katika kura za kumsaka nahodha, Marquinhos ametajwa kuwa namba moja, akifuatiwa na Danilo Pereira na namba tatu ni Presnel Kimpembe.
 
[emoji599] KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amefanyiwa upasuaji wa dharura kutokana na maumivu makali ya mgongo na atakosa mechi mbili za Ligi Kuu England. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alifanyiwa upasuaji na daktari Mireia Illueca, ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa uti wa mgongo mjini Barcelona na atabaki huko hadi atakapopata nafuu.
.
Guardiola amekuwa akisumbuliwa na mgongo kwa muda mrefu na alipanga kufanyiwa upasuaji, hivyo timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Juanma Lillo. Lillo ataiandaa timu kuelekea mechi mbili za ligi dhidi ya Sheffield United na Fulham zitakazopigwa kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi ujao.
.
Pia, Guardiola atakosa utambul-isho wa winga mpya Jeremy Doku aliyesajiliwa kutoka Rennes kwa Pauni 55 milioni, huku akiendelea kusaka kiungo mwingine wa kati.
 

Ulipe deni langu [mention]Phiri [/mention]
 
[emoji408] 13—LIONEL Messi sasa amehusika moja kwa moja kwenye mabao 13 katika mechi 8 alizocheza akiwa na klabu ya Inter Miami. Tangu ameanza kuitumikia klabu hiyo, Miami imeshinda mechi nane mfululizo huku akifunga katika kila mechi, imetwaa taji moja na tayari imeingia fainali ya michuano mingine ya US Open. [emoji238]
 
[emoji599] RASMUS Hojlund anatarajiwa kurejea wikiendi hii katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Nottingham Forest baada ya kukosa michezo miwili iliyopita. Mshambuliaji huyo anatarajiwa kurudi na kuleta nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Erik ten Hag na taarifa zimeripoti atafanya mazoezi na kikosi kamili kuelekea mchezo huo.
.
Man United ilianza kususua na katika mechi mbili walizocheza walifunga bao moja tu lililowekwa kimiani na beki wa kati Raphael Varane huku safu yao ya ushambuliaji ikionekana butu. Naye Ten Hag anaamini straika huyo mwenye umri wa miaka 20 atakuwa fiti asilimia 100 na huenda akawepo benchi kesho dhidi ya Nottingham Forest.
.
Chanzo cha habari kimeripoti kuna matarajio makubwa ya kuwepo kikosini kwa straika huyo, ambaye alitajwa na Ten Hag kama ni mshambuliaji wa aina ya kipekee. Kauli hiyo aliisema baada ya kumfuatilia straika huyo kipindi anakipiga Atalanta katika msimu wake wa kwanza Serie A ambako alifunga mabao tisa.
 
[emoji599] Winga mpya aliyesajiliwa Manchester City, Jeremy Doku, amefunguka kuwa angekuwa na maisha tofauti isingekuwa ushauri wa nyota wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane.
.
Winga huyo alifikiria kujiunga na Liverpool miaka mitano iliyopita wakati anakipiga Anderlecht mwaka 2018, lakini kauli ya Mane ilimkatisha tamaa. Doku, 21, aliweka wazi kwamba aliwahi kupewa jezi ya Mohamed Salah kama zawadi na endapo dili hilo lingekamilika Liverpool ingelazimika kulipa Pauni 500,000 ukilinganilisha na Pauni 55 milioni ambazo Man City imetoa kumnasa.
.
Lakini uhamisho huo haukufanyika na ametoboa siri kwamba alizungumza na Mane aliyemwambia muda wa kufanya uamuzi mkubwa katika historia ya soka lake ulikuwa bado. Akizungumza na mwaandishi wa habari wa Ouest France kuhusu mipango ya kuhamia Liverpool mwaka 2018 alisema:
.
“Nilikuwa bado mdogo nilikuwa na umri wa miaka 16, timu nyingi zilikuja na kuonyesha nia ya kunisajili, Liverpool ndio walivutiwa zaidi, Arsenal na Chelsea zilikuwepo pia.

Nakumbuka nilienda kufanya ziara Liverpool na wazazi wangu, tulionyeshwa maeneo ya uwanja wa Anfield, pia walinipa jezi ya Salah iliyosainiwa na nikakutana na wachezaji.

Niliongea na wachezaji wengi kama Simon Mignolet kwa sababu alikuwa Mbelgiji, Georginio Wijnaldum kutoka Uholanzi. Pia nilizungumza sana na Mane lakini hatukuzungumza kuhusu soka tulizungumza mambo tofauti.

Aliniambia nilikuwa mdogo bado ni muda mwingi na hakunishawishi kujiunga na Liverpool aliniambia tu utafanikiwa siku moja.”
 
[emoji599] JUST IN: Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele na beki kitasa wa Simba, Henock Inonga wamechaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo [emoji1078] kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Sudan.
.
Kiwango kizuri kilichoonyeshwa na nyota hao hasa katika mashindano ya CAF msimu uliopita bila ya shaka kimechangia kuitwa kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…