Makapuku Forum

Polisi wa Cameroon wameripotiwa kufungua uchunguzi kuhusu madai mchezaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto’o alikuwa sehemu ya kashfa ya upangaji matokeo. Staa huyo mwenye umri wa miaka 42, alishutumiwa kupanga matokeo katika mechi ya daraja la pili la Cameroon baada ya sauti yake kusikika kudaiwa kuzungumza na Rais wa Victoria United, Valentine Nkwain.
.
Kulingana na mtandao wa Camfoot, Eto’o, ambaye amekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) tangu Disemba 2021, inadaiwa aliahidi kuipandisha daraja la pili klabu ya Victoria United.
.
Madai hayo yame-mkanushwa na Eto’o na Nkwain. Gazeti la The Guardian sasa limeripoti kuwa, kutokana na barua iliyoonekana kwao, polisi wa Cameroon wameanzisha uchunguzi kuhusu madai ya matumizi mabaya ya mamlaka na rushwa.

…………….
 
DUH! HAYO MASHARTI YA ZIDANE USIPIME
.
Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ameripotiwa alikubali kurejea katika kazi ya ukocha lakini kwa sharti moja tu. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ana ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa soka akiwa kama kocha licha ya kustaafu, alionyesha nia ya kuinoa moja ya timu kutoka Ufaransa.
.
Zidane aliiongoza Madrid kunyakua mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa akiwa kama kocha mkuu, pia aliipa UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la klabu la FIFA mara mbili, pamoja na taji la La Liga na Supercopa. Hata hivyo, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 51 hajawahi kufundisha nje ya Hispania na nafasi yake ya mwisho akiwa kocha wa Madrid ilikuwa kuanzia mwaka 2019 hadi 2021. Sasa iliripotiwa Mfaransa huyo aliamua kurudi upya huku akihusishwa na klabu ya Olympique de Marseille ya Ufaransa.
.
Ripoti hiyo inasema Zidane alikubali kuwa kocha wa Marseille hata hivyo, kuna sharti moja ambalo lazima litimizwe endapo angeteuliwa. Inasemekana alikubali kuwa meneja mpya wa Marseille endapo klabu hiyo itauzwa kwa mwekezaji kutoka Saudi Arabia.

Lakini sharti la Zidane lingekuwa gumu kutimizwa kwani mmiliki wa sasa Frank McCourt, ambaye alinunua klabu hiyo miaka saba tu iliyopita, alisisitiza katika miezi ya hivi karibuni kwamba hana mpango wa kuipiga bei.

 
[emoji599] PYRAMIDS WANATINGA MAKUNDI
.
18’—[emoji460]️ Mustafa Fathi
56’—[emoji460]️ Mustafa Fathi
61’—[emoji460]️ Mustafa Fathi
82’—[emoji460]️ Mustafa Fathi
.
FT: [emoji1093] PYRAMIDS 6-1 APR [emoji1206]
 
Miamba ya Morocco, FAR Rabat inayonolewa na aliyekuwa kocha wa Yanga SC, Nasreddine Nabi imeaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla cha 3-1 dhidi ya Etoile Sahel ya Tunisia.

FT: FAR Rabat [emoji1173] 1-2 [emoji1249] Etoile Sahel (Agg. 1-3)
🟥 Marour18'
[emoji460] Zouhzouh 90+4'

[emoji460] Naouali 20'
[emoji460] Aouani 64'

Winga wa zamani wa Yanga SC na Simba SC Bernard Morrison alianza kwenye mchezo huo.

Nabi ameaga mashindano ya CAFCL kikatili baada ya mchezaji wake Zouhair Marour kula umeme dakika ya 18 tu.
 
HISTORIA imeandikwa! Hatimaye mwiko wa kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika umevunjwa, Yanga imetinga makundi ya CAFCL kwa mara ya kwanza tangu 1998.

FT: YANGA SC [emoji1241] 1-0 [emoji1232] AL MERREIKH (Agg. 3-0)

Yanga inakuwa timu ya 6 kutinga hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika baada ya:-

• Al Ahly [emoji1093]
• Pyramids [emoji1093]
• Jwaneng Galaxy [emoji1052]
• TP Mazembe [emoji1078]
• Petro Luanda [emoji1029]
• Young Africans SC [emoji1241]

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…