Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Polisi wa Cameroon wameripotiwa kufungua uchunguzi kuhusu madai mchezaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto’o alikuwa sehemu ya kashfa ya upangaji matokeo. Staa huyo mwenye umri wa miaka 42, alishutumiwa kupanga matokeo katika mechi ya daraja la pili la Cameroon baada ya sauti yake kusikika kudaiwa kuzungumza na Rais wa Victoria United, Valentine Nkwain.
.
Kulingana na mtandao wa Camfoot, Eto’o, ambaye amekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) tangu Disemba 2021, inadaiwa aliahidi kuipandisha daraja la pili klabu ya Victoria United.
.
Madai hayo yame-mkanushwa na Eto’o na Nkwain. Gazeti la The Guardian sasa limeripoti kuwa, kutokana na barua iliyoonekana kwao, polisi wa Cameroon wameanzisha uchunguzi kuhusu madai ya matumizi mabaya ya mamlaka na rushwa.
…………….