Makapuku Forum

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi kuhusiana na kile kilichojadiliwa na Watu wengi mitandaoni kuhusu Bernard Kamungo kuitwa Timu ya Taifa ya Marekani U-23 kuelekea michezo ya Olympic.

Msigwa amejibu suala hilo katika post ya Mwandishi John Jackson @johnjackson_jj anayeishi Ujerumani baada ya kuandika kuwa Tanzania imeshindwa kumpa Uraia Kamungo.

“Tanzania inazidi kupoteza Wachezaji wenye pontential nasikia mlimnyima passport, sasa anaenda kuichezea USA @gersonmsigwa kaka inabidi hawa Watu tuwe tunawazingatia mapema kabla hawajachukuliwa na Mataifa wanayoishi, huyu jamaa ni World Class Player @bernardk17” - John Jackson

Baada ya post hiyo Msigwa alijibu kwenye comment na kuandika kuwa “Hajawahi kunyimwa passport ya Tanzania, suala hili linafanyiwa kazi tuvute subra”

Kamungo alizaliwa katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu Kigoma Tanzania January 1 2002 na aliondoka Tanzania kwenda Marekani 2016 na familia yake kama Wakimbizi walioomba hifadhi nchini Marekani, kwa mujibu wa sheria ana haki ya kupata Uraia wa Tanzania kutokana na kuzaliwa nchini.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo October 12,2023 amepokea ripoti ya Kamati ya Kutathmini Ufanisi na Utendaji wa Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengini Kamati hiyo imesema suala la uraia pacha linahitaji mjadala wa Kitaifa ili kupata maoni ya Wananchi wote.

“Kwakuwa Serikali iliahidi kukamilisha mchakato wa hadhi maalum ili kukidhi shauku ya Diaspora Tanzania Kamati inashauri jambo hilo likamilishwe, hadhi maalum itatoa fursa kwa Diapora kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa na kupata haki ya kushiriki katika masuala ya kiuchumi na Kijamii katika Nchi yao ya asili na Serikali iandae utaratibu wa kuelimisha Umma kuhusu hadhi maalum na faida zake”

“Kuhusu suala la uraia pacha maoni ya Kamati ni kwamba jambo hili linahitaji mjadala wa Kitaifa ili kupata maoni ya Wananchi wote”
 
Moja ya habari kubwa iliyotufungulia mwezi huu wa October ni hii ya kuongezeka kwa wastani wa kipato cha kila Mtanzania kwa mwaka ambapo umeongezeka kwa asilimia 5 ikichangiwa na kukua kwa uchumi wa Kanda tatu za Dar es Salaam, Kanda ziwa na Kanda ya Kaskazini, kipato cha Mtanzania kimeongezeka kutoka wastani wa Tsh milioni 2.70 hadi Tsh Mil 2.84

Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya ufanisi wa uchumi katika kila Kanda iliyotolewa Oktober 5, 2023 inaonesha kwa ujumla inaonesha ukuaji wa Pato la Taifa ambalo limefikia Tsh trilioni 170.25 likiongezeka kutoka Tsh trilioni 156.37.

Ongezekao hilo linatajwa kuchangiwa zaidi na sekta ya kilimo, ujenzi, madini, viwanda na biashara.
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ameelezea mafanikio ya ziara ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India, wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Ikulu Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema katika ziara hiyo, Tanzania imefanikiwa kupata uhakika wa soko la mbaazi na Rais Samia ameomba kupatiwa soko la mgawo wa uhakika wa tani laki mbili kwakuwa India ni Mtumiaji mkubwa wa mbaazi duniani.

“Nchi ambazo zimepata fursa ya mgao kama huo ni Malawi na Msumbiji kutoka India, hivyo sisi ni watatu kutoka Afrika, katika hatua nyingine Serikali ya Tanzania imewasilisha mahitaji kwenye Serikali ya India, kwa ajili ya mradi mkubwa wa umwagiliaji kutoka Ziwa Victoria, mahitaji hayo ni takriban dola Bilioni moja ambao mradi huo utatekelezwa mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Dodoma, Kagera na Mara”

“Pia Serikali ya Tanzania ina mpango wa kununua jumla ya trekta elfu 10 na kujenga vituo maalum vya vifaa vya kilimo (mechanization), Serikali imekubaliana na makampuni makubwa mawili duniani ya matrekta, Mahindra na John Deer kuweka katika kipindi cha miezi 12 viwanda vya kuunganisha matrekta na kutengeneza vipuri ndani ya Tanzania”

“Tukizungumzia Sekta ya Ulinzi, Nchi hizi mbili zinatambua umuhimu wa kushirikiana kwenye teknolojia (technology transfer), kujengeana uwezo, mafunzo ya jeshi kwa pamoja na kubadilishana utaalamu na uzoefu”
 
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso @jumaa_aweso amesema suala la Wananchi kubambikiwa bili za maji halikubaliki na linakwenda kumalizika hivi karibuni ambapo Tanzania imekubaliana na India kutafuta Wadau ambao watawekeza kwenye mita za maji ambazo zitamwezesha Mtumiaji kununua maji kwa kiwango anachotaka kabla ya kuanza kuyatumia na yakiisha ananunua mengine kama ilivyo kwa umeme wa luku.

Akiongea Ikulu Dar es salaam leo wakati akielezea mafanikio ya ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Qatar na India kwa upande wa Sekta ya Maji, Aweso amesema “Kuna suala la mageuzi katika Sekta ya Maji, Wizara ya Maji pamoja na jukumu la kuwapa Wananchi maji maelelezo ya Rais ni kwamba tutumie teknolojia kufanya mageuzi kwenye Sekta ya Maji, kwa mfano hatuwezi kukubali kwamba Mwananchi kubambikiwa bili ya maji iwe ni suala la kawaida haiwezekani, haiwezekani suala hili liwe tatizo sugu ambalo limekosa mwarobaini, Mh. Rais katika ziara yake na sisi kama Wizara ya Maji wenzetu wa India kwenye teknolojia wapo vizuri kwamba tushirikiane nao kutafuta Wadau ambao watawekeza hasa kwenye pre paid meter kwamba Mwananchi atumie maji alipe bili ya maji kutokana na kile alichotumia, kama umeme anatumia maji ya elfu kumi ikisha ananunua mengine”

“Wakati mwingine unapita mtaani maji yanapotea, Mwananchi anatuma meseji kwa Mamlaka kwamba hapa panavuja lakini response inakuwa ndogo lazima tuwe na teknolojia ambayo itadetect kwamba hapa panavuja na Timu ikafika kwa haraka kufanya marekebisho, sio busara kuona maji yanavuja sehemu na Mwananchi hana maji”
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu @ummymwalimu amesema kufuatia kumpata Mwekezaji Esther Pharmaceutics ambaye atazalisha dawa hapa nchini, itasaidia kudhibiti bei za dawa kwasababu hivi sasa 80% ya dawa zinatoka nje ya Nchi na 60% kati ya hizo zinatoka India, hivyo Mwekezaji huyo atasaidia kushusha gharama za dawa na zitapatikana kwa wakati ambapo hivi sasa inachukua mpaka miezi tisa kuzipata kutokana na sababu mbalimbali.

Akiongea Ikulu Dar es salaam leo wakati akielezea mafanikio ya ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Qatar na India kwa upande wa Sekta ya Afya, Ummy amesema “Tumepata Mwekezaji ambaye yupo tayari na ameshacommit fedha za kuzalisha dawa Tanzania, kwa sasa 80% ya dawa zote zinazoingia nchini zinatoka nje ya Nchi na katika hiyo 60% ya dawa zinatoka India, kwahiyo sisi kama Sekta ya Afya tumerudi na mafanikio makubwa kupata Mtu ambaye sasa atawekeza katika uzalishaji wa ndani wa dawa”

“Dawa zikizalishwa ndani itasaidia kushusha gharama ya dawa kwasababu tutapunguza logistics cost za usafiri, uhifadhi n.k, pia dawa zitapatikana kwa wakati, sasa hivi inatuchukua mpaka miezi tisa kupata dawa kutoka nje ya Nchi hususani baada ya mlipuko wa Covid 19”

“Waziri Mkuu wa India amekubali ombi la Tanzania kuanzisha kituo cha tiba asilia ambapo tumenunua shamba ekari 100 Mkuranga kwa ajili ya kupanda miti dawa ambayo tunaijua ili kuweza kutengeneza dawa, hata hivyo tiba asili tayari imeanzishwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa saba na tunawaomba Madaktari waweze kushauriana na Wagonjwa ili kujadili tiba gani iweze kutumika katika matibabu”
 
Rekodi ya Brazil ya kushinda mechi 15 za kufuzu kombe la Dunia walizocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani imefikia ukomo asubuhi hii baada ya kutoka sare ya 1-1 na Venezuela.

[emoji2522]FT; ARGENTINA 1-0 PARAGUAY
[emoji460]️Otamendi

[emoji2522]FT; BRAZIL 1-1 VENEZUELA
[emoji460]️Magalhaes

[emoji460]️Bello

[emoji2522]FT; SPAIN 2-0 SCOTLAND
[emoji460]️Morata
[emoji460]️Sancet

[emoji2522]FT ;CROATIA 0-1 TURKEY
[emoji460]️Yilmaz

[emoji2522]FT; BOLIVIA 1-2 ECUADOR
[emoji460]️Romallo

[emoji460]️Paez
[emoji460]️Rodriguez

[emoji2522]FT; CHILE 2-0 PERU
[emoji460]️ Valdes
[emoji460]️ Lopez
 
Kocha wa Real Madrid Don Carlo Ancelotti baada ya kutunukiwa udaktari wa heshima katika Chuo Kikuu cha Parma amesema anataka aanze kuitwa Daktari !

“Nitawaambia wachezaji wangu waanze kuniita daktari”
 
Harry Maguire amesema licha ya ufinyu wa nafasi chini ya Ten Hag bado amekuwa na kiwango bora hasa anapopata nafasi kwani akianza uwezekano wa kushinda huwa ni mkubwa

“Rekodi yangu chini ya meneja huyu inajieleza yenyewe,Sijaanza michezo mingi kama nipendavyo lakini asilimia yangu ya ushindi wakati nimecheza ni ya juu sana.”

Mnasemaje tiba ni Maguire kuanza ____??
 
[emoji599] KIKOSI cha Timu ya Taifa, Taifa Stars [emoji1241] kinaendelea kujifua kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan itakayopigwa Saudi Arabia, huku kocha wa timu hiyo, Adel Amrouche akimuacha tena kiungo wa Azam FC, mwenye mabao manne katika Ligi Kuu hadi sasa, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
.
Hii ni mara ya pili kwa Fei kutoitwa Stars kwani Amrouche alimtema wakati Stars ilipovaana na Niger na Algeria zilizoipa timu hiyo tiketi ya fainali za Kombe la Afrika (Afcon 2023) zitakazofanyika mwakani Ivory Coast ambapo droo zake zilitarajiwa kupangwa usiku wa jana nchini humo Tanzania ikiwa chungu cha nne.
.
Mbali na Fei kiungo mwengine wa Yanga Jonas Mkude naye ni kati ya waliotemwa kwenye kikosi hicho cha Stars.
 
Legend wa Arsenal, Ian Wright amesema timu hiyo itashindana na Manchester City katika mbio za ubingwa endapo itamsajili straika wa Brentford, Ivan Toney katika dirisha dogo la usajili la Januari. Arsenal ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England tofauti ya pointi mbili dhidi ya Man City baada ya kuifunga wikiendi iliyopita.
.
Hiyo ni hatua nzuri kwa Kocha Mikel Arteta kutokana na ushindi huo wa kwanza Ligi Kuu England dhidi ya Man City tangu mwaka 2015. Lakini mkongwe huyo amedai Arsenal inatakiwa kufanya usajili wa straika mpya ambaye ataongeza nguvu katika kikosi na kumpendekeza Toney.
.
Aliongeza Arsenal haitafika mbali ikiendelea kumtegemea Eddie Nketiah na Gabriel Jesus ambao sio hatari zaidi wanapokuwa eneo la hatari. “Tulipoteza mabao mengi na ikatuweka katika nafasi fulani. Nadhani Toney atafaa zaidi kwa sababu ni mchezaji anayejua kufunga. Ukiwazungumzia Nketiah na Jesus utarudi nyuma katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham, Jesus alikosa mabao mengi sana, kwa mchezaji mwenye uwezo kama wake maeneo kama yale jitihada inahitajika zaidi.”
.
Toney ambaye amehusishwa na Arsenal alifungia Brentford mabao 20 msimu wa 2022-23 lakini anakibiliwa na adhabu ya kufungiwa miezi minane baada ya kukiri kuwa anabeti. Straika huyo wa kimataifa wa England atarejea Januari kuendelea na maisha yake ya soka.

 
AFCON 2023 [emoji471]

GROUP A
1. Ivory Coast [emoji1081]
2. Nigeria [emoji1184]
3. EQ Guinea [emoji1119]
4. Guinea Bissau

GROUP B
1. Egypt [emoji1093]
2. Ghana [emoji1110]
3. Cape Verde [emoji1065]
4. Mozambique [emoji1174]

GROUP C
1. Senegal [emoji1211]
2. Cameroon [emoji1062]
3. Guinea [emoji1119]
4. Gambia [emoji1108]

GROUP D
1. Algeria [emoji1026]
2. Burkina Faso [emoji1059]
3. Mauritania [emoji1163]
4. Angola [emoji1029]

GROUP E
1. Tunisia
2. Mali [emoji1159]
3. South Africa [emoji1221]
4. Namibia [emoji1176]

GROUP F
1. Morocco [emoji1173]
2. DR Congo [emoji1078]
3. Zambia [emoji1268]
4. TANZANIA [emoji1241]

 
Magazeti ya leo October 17, 2023.
 

Attachments

  • Screenshot_20231017_063643_Opera Mini.jpg
    182.6 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…