Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ametolea ufafanuzi kuhusiana na kile kilichojadiliwa na Watu wengi mitandaoni kuhusu Bernard Kamungo kuitwa Timu ya Taifa ya Marekani U-23 kuelekea michezo ya Olympic.
Msigwa amejibu suala hilo katika post ya Mwandishi John Jackson @johnjackson_jj anayeishi Ujerumani baada ya kuandika kuwa Tanzania imeshindwa kumpa Uraia Kamungo.
“Tanzania inazidi kupoteza Wachezaji wenye pontential nasikia mlimnyima passport, sasa anaenda kuichezea USA @gersonmsigwa kaka inabidi hawa Watu tuwe tunawazingatia mapema kabla hawajachukuliwa na Mataifa wanayoishi, huyu jamaa ni World Class Player @bernardk17” - John Jackson
Baada ya post hiyo Msigwa alijibu kwenye comment na kuandika kuwa “Hajawahi kunyimwa passport ya Tanzania, suala hili linafanyiwa kazi tuvute subra”
Kamungo alizaliwa katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu Kigoma Tanzania January 1 2002 na aliondoka Tanzania kwenda Marekani 2016 na familia yake kama Wakimbizi walioomba hifadhi nchini Marekani, kwa mujibu wa sheria ana haki ya kupata Uraia wa Tanzania kutokana na kuzaliwa nchini.