Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huenda ukawa umeshtushwa na upungufu wa dagaa unaojitokeza kwenye baadhi ya masoko jijini Dar es Salaam.

Mwananchi jana iliweka kambi katika katika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry na kubaini ndoo moja ya lita 20 ya dagaa mchele imepanda kutoka wastani wa Sh40,000 hadi Sh70,000 ndani ya wiki mbili zilizopita.

Kutokana na mazingira hayo, wafanyabiashara wa dagaa wa kukaanga katika magenge jijini hapa wamesema bei ya fungu la Sh1,000 haitabadilika, isipokuwa wamelazimika kupunguza wingi wake.

Screenshot_20231118_144336_Instagram.jpg
 
Ni mtaa wenye pilikapilika, pikipiki zilizopakia watu wenye nguo zilizochafuka ‘grisi’ zinaingia na kutoka. Kuna biashara za vipuri vilivyotumika vya magari sambamba na vyuma chakavu na bei zake zinatajwa kuwa rafiki.

Hapa ni Tandale, jijini Dar es Salaam, lakini hali kama hii utaishuhudia pia katika mitaa mingi kama Manzese, Tabata Dampo, Temeke na kwingineko, vivyo hivyo eneo la Wakereketwa - Unga Limited jijini Arusha.

Mbali na biashara hii kushamiri, yapo maneno kuwa baadhi ya watu wanaofanya biashara hizi wanahusika pia katika wizi wa vipuri na magari, jambo linaloamsha shauku ya kuchunguza undani wa biashara hii.

James Muhinga, mkazi wa Msasani jijini Dar es Salaam anasimulia tukio lililomkuta la kuibiwa vioo vya pembeni (side mirror) za gari lake kisha baada ya miezi kadhaa alimkuta nazo mtu mwingine ambaye alidai amevinunua Manzese.

“Mwaka jana (2022) niliibiwa ‘side mirrors’ za gari langu na baada ya miezi kama minne hivi nilizikuta kwenye gari la mtu mwingine aliyedai amenunua Manzese,” anasema.

Kufuatia maelezo hayo, mwandishi wa Mwananchi aliamua kuweka kambi katika maeneo zinakofanyika biashara hizo jijini Dar es Salaam akichunguza namna zinavyofanyika na ikabainika kuwa wateja wengi hufuata bei ya chini ya vifaa hivyo.

Screenshot_20231118_144450_Instagram.jpg
 
Aliyekuwa Rais wa Liberia, George Weah amepoteza kiti cha urais mbele ya kiongozi wa upinzani, Joseph Boakai ambaye amefanikiwa kufikisha asilimia 51 ya kura zote zilizopigwa ambapo kisheria utamfanya kuwa mshindi.

Akizungumzia mwelekeo wa kazi ya kuhesabu kura katika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Liberia, Weah jana alisema kuwa ataachia nafasi hiyo kwa amani huku akiwataka wafuasi wake wakubaliane na matokeo ya ushindi wa Boakai ambaye alimshinda katika uchaguzi uliomweka madarakani mwaka 2017.

"Muda mfupi uliopita nimezungumza na Rais aliyechaguliwa Joseph Boakai na kumpongeza kwa ushindi.

"Nawaomba wote kufuata mfano wangu na kukubaliana na matokeo ya uchaguzi," amesema Weah.

Licha ya Boakai kushinda katika uchaguzi wa awali, hakufikisha asilimia 51 ambazo kisheria ndizo zinahitajika ili mgombea atangazwe kuwa mshindi jambo lililopelekea zoezi la upigaji kura kurudiwa.

Screenshot_20231118_144553_Instagram.jpg
 
Maandalizi ya Mazishi ya mtoto Salehe Zuberi aliyefariki dunia alfajiri ya Novemba 15 Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu, yamekamilika na anatarajiwa kuzikwa mchana leo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 18, 2023, mjomba wa marehemu, Ibrahimu Kivumbi amesema mwili uliwasili nyumbani hapo jana usiku.

Amesema mpaka sasa hakuna changamoto yoyote kuhusu maandalizi ya mazishi, kinachosubiriwa na muda uliopangwa wa kwenda kuuhifadhi mwili huo.

"Tunawashukuru viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wenzetu wa Vibaoni kwa michango yao na kufanikisha mwili kufika Handeni, kwa kweli tulikuwa kwenye wakati mgumu," amesema.

Mwananchi Digital Novemba 16, 2023 iliripoti taarifa ya mwili wa marehemu Salehe kushikiliwa Muhimbili huku babu wa yake Salim Kivumbi, akiomba uongozi wa Muhimbili na wasamariawema kumsaidia apate mwili wa mjukuu wake kwa ajili ya mazishi.

Viongozi mbalimbali walijitokeza kuisaidia familia hiyo kukomboa mwili wa marehemu uliokuwa ukishikiliwa kwa deni la Sh2.4 milioni zikiwa ni gharama za matibabu kabla ya mauti kumkuta.

Screenshot_20231118_144801_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Kipalestina (Unrwa), Juliette Touma amesema ili waweze kutoa misaada ya kiutu katika ukanda wa Gaza, lita 120,000 za mafuta zinahitajika kila siku.

Shirikia na Reuters limeripoti kuwa Israel limeidhinisha malori ya mafuta hasa yanayotoka Misri kuingi ukanda wa Gaza kwenda kutoa msaada kutokana na uhaba wa nishati hiyo.

Touma amesema ukosefu wa nishati hiyo pamoja na kukatika kwa mawasiliano, kunaitatiza Unrwa kutoa misaada ya kibinadamu Gaza kutokana na uharibifu wa miundombinu iliyopo.

Amesema mpaka jana, hapakuwa na mafuta yaliyofikishwa Gaza japo inadaiwa kuwa Baraza la Mawaziri la Israel linaloshughulika na vita hivyo, limeidhinisha malori mawili ya mafuta kuingia Gaza yakitokea Misri kila siku.

Kwa upande mwingine, kampuni za mawasiliano ya simu za Paltel na Jawwal zimesema kuwa huduma za simu na intanet zimerejeshwa kwa sehemu katika Ukanda wa Gaza.

Screenshot_20231118_144927_Instagram.jpg
 
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wananchi wanaowahudumia wanawezeshwa kupata huduma ya majisafi kwa kupewa utaratibu wa kulipa kidogokidogo kwa mkopo.

Ametoa kauli hiyo jana Novemba 17, 2023 kwenye hafla ya utiaji saini na kumkabidhi mkandarasi M/S SinoHydro kutoka China eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa sio wananchi wote wana uwezo wa kulipia gharama ya maunganisho mapya kwa wakati kulingana na utofauti wa kipato, hivyo kwa wale ambao hawawezi wapewe utaratibu wa kulipa kwa njia ya mkopo ili wote wanufaike na huduma ya majisafi.

Screenshot_20231118_145023_Instagram.jpg
 
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, imetaja visababishi vikuu vya wanawake kujifungua watoto kabla ya wakati (njiti) kuwa ni pamoja na maambukizi ya bakteria, UTI na malaria kwa mjamzito.

Sababu nyinyine ni mwanamke kushika ujauzito wa watoto mapacha, presha ya mimba (kifafa cha mimba), upungufu wa damu na kupata ajali wakati wa ujauzito.

Sababu hizo zimebainishwa leo Ijumaa Novemba 17, 2023, kwenye maadhimisho ya siku ya watoto njiti duniani yaliyofanyika kikanda katika hospitali hiyo, jijini Mwanza, huku Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk Neema Kayange akisema kila mwezi, wastani wa watoto njiti 130, huzaliwa hospitalini hapo.

“Tunaiasa jamii kuhudhuria kliniki kuanzia mimba ikiwa changa kabisa, mjamzito kupata lishe kamili na kupatiwa dawa za kuongeza damu (Folic acid), na kufanya ufuatiliaji wa makuzi ya mtoto akiwa tumbaoni,” amesema Dk Kayange.

Screenshot_20231118_145409_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyofanya kikao chake mkoani Njombe imemhukumu Joel Nziku kunyongwa hadi kufa, kwa kosa la kuwaua watoto watatu wa baba yake mdogo.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Aboubakar Mrisha amesema mshitakiwa huyo alitekeleza mauaji hayo mwezi Januari mwaka 2019 katika Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

Jaji Mrisha amesema mshitakiwa huyo alikwenda nyumbani kwa baba yake mdogo na kuwachukua watoto watatu ambao aliwapakia kwenye lori na baadae aliwaua kwa kuwapiga na kitu kizito na kisha kuitelekeza miili katika maeneo tofauti.

Amesema pamoja na mshtakiwa kukana kuhusika na mauaji pamoja na kukana kutowafahamu watoto waliouawa, mahakama imesema kupitia vielelezo na mashahidi tisa walioapa na kutoa ushahidi mahakamani hapo, mahakama hiyo imemkuta mshitakiwa na hatia ya mauaji.
Screenshot_20231118_145507_Instagram.jpg
 
Chai ya Tanzania imetajwa kuwa ni ya kipekee na kwamba hauwezi kuilinganisha na chai yoyote duniani huku upekee wake ukitokana na rangi yake asilia ambayo huwezi kuilinganisha na chai yoyote Duniani na hivyo masoko ya nje yanahitaji chai ya Tanzania ili wachanganye na chai nyingine na wapate rangi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula amesema hayo wakati wa mnada wa kwanza wa Kimataifa wa chai ambao umefanyika kwa mara ya kwanza nchini ukilenga kuongeza thamani ya zao la chai ili kuchangia pato la Taifa, kabla ya hapo mnada huo ulikuwa unafanywa Kenya “Lazima tuilinde chai yetu na tujipongeze kuwa tuna chai nzuri”

Tani 560 sawa na 48% ya chai iliyopelekwa mnadani, imeuzwa kwa wastani wa USD cent 77 kwa kilo ambapo Mgeni rasmi wa mnada ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Dkt. Hussein Omar.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TBT, Mary Kipeja amesema faida za mnada huo ni kuongeza uwazi kwenye soko la chai, kuongeza kipato cha wakulima wa chai ambapo pia Serikali itapata mapato zaidi kupitia bandari za Tanga na Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa Wananchi kama wakulima na wanufaika wa mnyororo wa thamani
Screenshot_20231118_145633_Instagram.jpg
 
Mkazi wa Kijiji cha Mkangwe Kata ya Malangali Wilaya ya Mufindi Emmanuel Kikoti (66) amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na kosa la ubakaji kwa kufanya mapenzi na binti mwenye tatizo la akili mwenye umri wa miaka 14 wakati Binti huyo akichunga ng'ombe na Kaka yake.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Sekela Kyungu amesema November 1,2023 huko katika Kijiji cha Mkongwe kata ya Malangali Wilayani Mufindi Mshtakiwa alifanya mapenzi na Muhanga huyo huku akijua kwamba Binti huyo ana tatizo la akili, Kyungu amesema Muhanga huyo alikuwa porini akichunga ng'ombe na Kaka yake na Wakati wakiwa wanachunga ng'ombe Kaka wa Muhanga huyo alitoka kidogo ndipo Mshtakiwa alipopita na kumkuta Binti akiwa pekee yake kisha akamuuita na kumpeleka korongoni na akatekeleza kitendo hicho.

Baada ya Kaka wa Muhanga huyo kurudi katika sehemu ambayo alimuacha muhanga na kutomkuta alianza kumtafuta na kumkuta kwenye korongo hilo akiwa na Emmanuel na baada ya kuona tukio hilo Kaka wa Muhanga huyo aliondoka na kwenda kumuita Dada yake hadi kwenye eneo hilo na kumkuta Mshtakiwa bado anaendelea kufanya kitendo hicho.

Mahakama hiyo imemtia hatiani Mshtakiwa huyo kwa mujibu wa kifungu namba 228 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 rejeo la Mwaka 2022; na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela chini ya kifungu namba 137 cha kanuni ya adhabu sura 16 rejeo la mwaka 2022.

Hata hivyo Hakimu amefafanua kuwa adhabu ya kosa kama hilo ni kifungo chake miaka 14 Jela ila kutokana na maombi ambayo Mshtakiwa Emmanuel ameyatoa na ukizingatia ndio kosa lake la kwanza, umri wake wa miaka 66 huku akiwa ni Mgane na ana Familia ambayo inamtegemea ndipo Mahakama ikatoa adhabu hiyo.
Screenshot_20231118_145732_Instagram.jpg
 
Huenda ukawa umeshtushwa na upungufu wa dagaa unaojitokeza kwenye baadhi ya masoko jijini Dar es Salaam.

Mwananchi jana iliweka kambi katika katika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry na kubaini ndoo moja ya lita 20 ya dagaa mchele imepanda kutoka wastani wa Sh40,000 hadi Sh70,000 ndani ya wiki mbili zilizopita.

Kutokana na mazingira hayo, wafanyabiashara wa dagaa wa kukaanga katika magenge jijini hapa wamesema bei ya fungu la Sh1,000 haitabadilika, isipokuwa wamelazimika kupunguza wingi wake.

View attachment 2817753
Chakula changu pendwa😭😭
 
Back
Top Bottom