Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwili wa mtoto Salehe Zuberi (5) aliyefariki dunia alfajiri ya Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu, umezikwa leo Jumamosi wilayani Handeni.

Akizungumza baada ya maziko hayo, babu wa marehemu, Salimu Kivumbi amewashukuru viongozi waliojitokeza na kusaidia mwili wa mjukuu wake kufika Handeni.

Novemba 16, 2023, Mwananchi Digital iliripoti taarifa ya mwili wa Salehe kushikiliwa Muhimbili baada ya kudaiwa deni la Sh2.4 milioni lililotokana gharama za matibabu huku familia yake, ikiomba wasamaria wema kujitokeza kuwasaidia waupate mwili wa mtoto wao kwa ajili ya maziko.

Mmoja wa wananchi aleshiriki maziko hayo, Nicholas Kusaka amesema imefika wakati sasa kwa Serikali kuangalia njia mbadala ya kutatua changamoto hii ambayo huwakumbana Watanzania wengi wenye uwezo wa chini.

Naye Diwani wa Vibaoni, Marry Mntambo amewapongeza wananchi wake kwa kujitokeza kuchangisha fedha mtaani kwa ajili ya kuukomboa mwili huo licha ya Mbunge wa Handeni Mjini, Reuben Kwagilwa kuahidi kulishughulikia tatizo hilo pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda aliyechangia Sh3 milioni.
Screenshot_20231119_072547_Instagram.jpg
 
Baada ya Everton kupokonywa alama 10, taarifa zinadai kwamba mabosi wa timu za Manchester City na Chelsea wako matumbo ni joto wakihofia kunyang’anywa alama zitakazozishusha kwenye nafasi za sasa.
.
Everton imepokonywa alama hizo baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka sheria ya usawa wa matumizi ya pesa na sasa ipo kwenye hali mbaya zaidi baada ya Leeds, Leicester City, Southampton, Nottingham Forest na Burnley kuidai fidia.
.
Wataalamu wa masuala ya kisheria wameionya Man City, ambayo Januari, mwaka huu ilituhumiwa kwa makosa 115 ya kukiuka sheria hiyo sambamba na Chelsea ambayo ipo chini ya uchunguzi ikidaiwa kukiuka sheria hiyo enzi za umiliki wa Roman Abramovic.
.
Kwa mujibu wa mmoja kati ya wanasheria mahiri wa masuala ya michezo nchini England, Stefan Borson ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya kifedha wa Manchester City ni kwamba, kama Man City au Chelsea zitakutwa na hatia, basi zinaweza kushushwa daraja.
.
Borson alidai adhabu iliyopewa Everton ni ndogo kwa kosa ililofanya na mambo yanaweza kubadilika kwa Man City na Chelsea ambazo huenda zikakumbana na adhabu kali ya kuzishusha daraja.
.
Hata hivyo, Man City ilikana tuhuma za kukiuka sheria na ikaajiri mwanasheria NGULI kutoka kampuni ya KC Lord Pannick kwa ajili ya kuitetea kwenye kesi hiyo.
.
Everton ilikutwa na hatia ya kuzidisha matumizi ya Pauni 19.5 milioni kutoka Pauni 105 milioni ilizotakiwa kutumia ikifanya hivyo kwa miaka mitatu. Lakini, kwa upande wa Chelsea na Man City inaonekana kwamba zitapata adhabu kubwa zaidi kwa sababu zimekuwa zikihusishwa kukiuka sheria kwa muda mrefu, hivyo hata adhabu itakuwa kubwa tofauti na Everton.

…………..
Screenshot_20231119_072708_Instagram.jpg
 
REECE AMETEMBELEA SHABIKI ALIYEZIMIA
.
Shabiki wa Chelsea, Reece James ametuma ujumbe wenye hisia kupitia akaunti ya Instagram baada ya kumtembelea hospitali shabiki aliyepatwa na mshtuko wa moyo. Tukio la shabiki huyo aliyezimia kwa dakika 20 kutokana na mshtuko wa moyo lilitokea wakati wa mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea na Manchester City kabla ya mapumziko ya kimaitaifa timu hizo zikitoka sare ya mabao 4-4.
.
Hata hivyo, wakati mechi inaendelea shabiki huyo wa Chelsea alipatwa na mshtuko akiwa jukwaani uwanjani Stamford Bridge na kuzua taharuki. Shabiki huyo alidondoka na kuzimia kwa dakika 20 wengi wakiamini kwamba huenda amefariki, lakini baada ya kufanyiwa matibabu alizinduka. Kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini na wiki hii alitembelewa na nahodha huyo wa Chelsea ili kumsaidia na kumpa moyo kufuatia mshtuko huo.
.
Beki huyo aliandika ujumbe wa maneno kupitia akaunti yake yenye wafuasi milio 3.1 akisema: “Nilitembelea hospitali jioni ya leo kumona shabiki wa Chelsea ambaye alipata mshtuko wa moyo kwenye mchezo wetu dhidi ya Man City. ‘Alifariki’ kwa dakika 20 na madaktari walifanikiwa kuokoa maisha yake. Alionekana mwenye nguvu . Nina furaha sana kwamba amepona.”
.
James aliendelea kusema: “Maisha ni ya thamani sana na hayatabiriki. Kila kitu kinaweza kutokea wakati wowote. Kwa hiyo furahia maisha hata kama wakati mwingine mambo yanakuwa magumu.”
Screenshot_20231119_072932_Instagram.jpg
 
Huenda ukawa umeshtushwa na upungufu wa dagaa unaojitokeza kwenye baadhi ya masoko jijini Dar es Salaam.

Mwananchi jana iliweka kambi katika katika Soko la Kimataifa la Samaki Ferry na kubaini ndoo moja ya lita 20 ya dagaa mchele imepanda kutoka wastani wa Sh40,000 hadi Sh70,000 ndani ya wiki mbili zilizopita.

Kutokana na mazingira hayo, wafanyabiashara wa dagaa wa kukaanga katika magenge jijini hapa wamesema bei ya fungu la Sh1,000 haitabadilika, isipokuwa wamelazimika kupunguza wingi wake.

View attachment 2817753
Mwanza wanatabia ya kufunga ziwa week nzima kupisha dagaa kukua nadhani hili ndo chanzo
 
Farhan Kihamu

MBWANA SAMATTA, sikuwa busy sana na Wachezaji Vijana kwenye mchezo wa leo! Wala sikuwa busy sana na uwezo wa ukuta wa Taifa Stars namna umetulia na venye walimlinda vyema Aishi Manula ambaye alikuwa kwenye ile hadhi yake ya siku zote, the real Tanzania One.

Nilikuwa busy sana kumtazama Tanzania Football Poster Boy @samagoal77 na usinga wake umekaa vyema begani anakuja chini anakaba na kuchukua mali kisha anapanda nazo, sahau kuhusu assist na namna amevuja jasho, nilivutiwa na namna alivyoliongoza jeshi lake mbali na nyumbani.

Sahau kuhusu flights nyingi za usiku kurejea Terminal Three pale Airport kwa Babu yake Mwalimu wa Butiama, sahau namna ratiba inavyombana kutoka ardhi ya Bongo Movie mpaka Ugiriki kwa Spartacus na Pythagorus! Heshimu kipaji chake na jitihada kwa taifa lake ambalo wengi wamekuwa wakimbeza sana.

CAPTAIN! Take a bow @samagoal77 ipo siku tutaliandika jina lako kwa damu kwenye mapango ya Mahenge, Morogoro! Tutaliandika tena jina lako kwa upendo kwenye Mwendokasi za Mbagala kwakuwa YOU ARE ONE OF US, ONE OF OUR OWN.

Screenshot_20231119_073128_Instagram.jpg
 
Wanafunzi 88 waliojiunga na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) mkoani Arusha, wameshindwa kumaliza mafunzo kwa sababu mbalimbali ambapo kati yao, 14 wadaiwa kuyakimbia ambapo mhitimu hutunukiwa “Shahada ya Kijeshi.”

Hayo yamebainishwa katika mahafali ya leo Jumamosi Novemba 18, 2023 ambapo maofisa wanafunzi 575, wametunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan na hivyo kuvishwa vyeo vya Luteni Usu.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mkuu wa chuo hicho, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kulikuwa na makundi mawili wa wanafunzi ambapo katika kundi la 04/20 la maofisa wa wanafunzi wa shahada ya Sayansi ya Kijeshi, waliojiunga na chuo walikuwa 73 huku 62 ndiyo walifanikiwa kuhitimu.

View attachment 2818406
🤣🤣🤣🤣 hao hata vita watakimbia hao.
 
Back
Top Bottom