Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Mwili wa mtoto Salehe Zuberi (5) aliyefariki dunia alfajiri ya Novemba 15 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu, umezikwa leo Jumamosi wilayani Handeni.
Akizungumza baada ya maziko hayo, babu wa marehemu, Salimu Kivumbi amewashukuru viongozi waliojitokeza na kusaidia mwili wa mjukuu wake kufika Handeni.
Novemba 16, 2023, Mwananchi Digital iliripoti taarifa ya mwili wa Salehe kushikiliwa Muhimbili baada ya kudaiwa deni la Sh2.4 milioni lililotokana gharama za matibabu huku familia yake, ikiomba wasamaria wema kujitokeza kuwasaidia waupate mwili wa mtoto wao kwa ajili ya maziko.
Mmoja wa wananchi aleshiriki maziko hayo, Nicholas Kusaka amesema imefika wakati sasa kwa Serikali kuangalia njia mbadala ya kutatua changamoto hii ambayo huwakumbana Watanzania wengi wenye uwezo wa chini.
Naye Diwani wa Vibaoni, Marry Mntambo amewapongeza wananchi wake kwa kujitokeza kuchangisha fedha mtaani kwa ajili ya kuukomboa mwili huo licha ya Mbunge wa Handeni Mjini, Reuben Kwagilwa kuahidi kulishughulikia tatizo hilo pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda aliyechangia Sh3 milioni.