Makapuku Forum

Makapuku Forum

FB_IMG_1703995800616.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Zambia imesema jana Alhamisi kuwa imeahirisha kuanza kwa muhula mpya ya masomo kwa wiki tatu zaidi kutokana mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeshaua watu 150 tangu Oktoba, 2023.

Waziri wa Elimu, Douglas Syakalima amesema shule nchini humo zilipaswa kufunguliwa Januari 8, 2024 lakini sasa zitafunguliwa Januari 29, 2024,

Zaidi ya watu 4,000 wameugua kipindupindu na vifo 150 vimeripotiwa, takwimu za hivi karibuni za Serikali zinaonyesha kiwango cha vifo ni asilimia 3.7.

Pia wagonjwa wapya 342 wameripotiwa katika saa 24 zilizopita, huku vifo 23 vikiripotiwa.

"Serikali ina wasiwasi kuhusu athari za mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika sekta ya elimu, hivyo hatua hiyo imechukuliwa ili kulinda afya za wanafunzi," amesema Syakalima.

Desemba, 2023 Zambia iliendesha kampeni ya kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na usambazaji dawa ya klorini ili kuua wadudu kwenye maji machafu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kote ulimwenguni katika miaka ya hivi karibuni, huku Afrika ikiwa na hali mbaya.

Screenshot_20240105_144927_Instagram.jpg
 
Ulimwengu wa wapenda michezo baadaye leo utashuhudia tukio la kuachiwa huru kutoka gerezani mwanariadha wa zamani wa mbio fupi, Oscar Pistorious, raia wa Afrika Kusini.

Nyota huyu anaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo kwa miaka isiyopungua tisa, na sasa ataenda kutumikia kifungo cha nje hadi mwaka 2029.

Oscar (37), alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi mara nne.

Alimuua Reeva aliyekuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo wakati Oscar akiwa bafuni. Katika utetezi wake, nyota huyo alisema alifyatua risasi ikiwa ni sehemu ya kujihami kwani alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake.

Oscar amekuwa na maadui wengi tangu afanye tukio la mauaji na kupelekwa mahakamani, baadhi walijionyesha hadharani wakati kesi yake inasikilizwa kwenye mahakama ya North Gauteng High Court mwaka 2014.

Screenshot_20240105_145115_Instagram.jpg
 
Serikali ya Tanzania imesitisha bei mpya za kitita cha matibabu kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) huku ikitangaza kuunda kamati huru itakayofanya mapitio ya maboresho yaliyofanyika.

Bei hizo mpya zilizopangwa kuanza kutumika kuanzia Januari mosi, 2024 zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena.

Hatua hiyo inatokana na tishio la hospitali binafsi kusitisha huduma za matibabu kwa wenye kadi za NHIF na hivyo kulazimu mazungumzo ya mezani na waziri mwenye dhamana ya afya, Ummy Mwalimu.

Desemba 18, 2023 NHIF ilifanya mapitio ya kitita cha mafao kwa mwaka 2023, ambayo kwa mujibu wao yalilenga kuongeza au kupunguza gharama katika baadhi ya huduma, ili kuendana na bei halisi ya soko.

Kutokana na mabadiliko hayo, iliibuka sintofahamu baada ya madaktari bobezi kuyalalamikia wakidai kutoshirikishwa huku wamiliki wa hospitali binafsi wakieleza kutoyaafiki.

Uamuzi huo umefikiwa jana Alhamisi, Januari 4, 2024 baada ya mkutano wa ndani kati ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na wawakilishi wa wamiliki wa hospitali binafsi wakiwamo Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Chama cha Wamiliki wa Vituo vya Aafya Binafsi Tanzania (APHFTA) na Bakwata.

Screenshot_20240105_145234_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya afya nchini Rwanda imerejesha dawa za kuzuia fangasi (antifungal) zilizotengenezwa nchini Kenya kutokana na masuala ya usalama.

Katika taarifa yake, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (RFDA) imewaagiza waagizaji kurudisha tembe zote za fluconazole zenye miligramu 200 zinazotengenezwa na Univeral Corporation, kampuni ya Kenya.

Pia imeagiza wauzaji wa rejareja na vituo vya afya kusitisha usambazaji wa dawa hizo na kuzirejesha kwa wasambazaji.

Hii imekuja baada ya taarifa ya awali kutoka kwa mamlaka, ambayo imetahadharisha mtengenezaji huyo wa Kenya kuhusu kubadilika rangi kwenye tembe.

Kulingana na RFDA, vifurushi vinne vya jumla vya tembe za fluconazole 200mg zilizoingizwa nchini humo vimebadilika rangi na kuwa nyeupe baada ya kukaa kwa muda mfupi kwenye kabati.

Shirika hilo limesema baadhi ya tembe hizo zilizobadilika rangi tayari zimeingia kwenye soko la Rwanda.

Screenshot_20240105_145415_Android%20System.jpg
 
Back
Top Bottom