Makapuku Forum

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei ameapa kujibu shambulio la bomu lililosababisha vifo vya watu 84 waliokuwa wakiadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani lililofanywa na Marekani.

Shambulio hilo la Kerman kusini mwa Iran limetokea Jumatano, Januari 3, 2024 na kusababisha vifo vya watu 84 na wengine wengi kujeruhiwa.
Bado hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.

"Wahalifu wakatili lazima wajue watakabiliwa vikali kuanzia sasa na bila shaka kutakuwa na jibu kali," amesema Khamenei katika taarifa yake kwa umma.

 
Jambo jema sana kwasie watumiaji wa NHIF
 
KAMATI hiyo imejumuisha wajumbe 16, wakiwamo vigogo wa Simba na Yanga, Injinia Hersi Said na Salim Abdallah ‘Try Again’ na wachambuzi wa soka kama Jemedari Said, Oscar Oscar. Pia kuna Baba Levo, Joti, Mwijaku, Bongo Zozo, Seven, Prisca Kishamba, Beatrice Singano, Michale Nchimbi, Hamis Ali, Paulo Makanza, Mohamed Soloka na Hassan Raza.
.
Katika taarifa yake, Wizara inasema kamati hiyo ina lengo la kuhamasisha mashabiki na wapenzi wa michezo wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kuzishangilia na kuziunga mkono timu hizo pamoja na kuratibu hafla maalumu ya harambee na kuichangia itakayofanyika Januari 10, jijini Dar es Salaam.
.
Arena kama wadau wakubwa wa michezo hususani soka, tunadhani serikali inarudia kosa lilelile ambalo limewahi kutokea siku za nyuma kwa kuunda kamati hizi za kisiasa badala ya kuwekeza zaidi kuwa na timu bora zinazowahamasisha mashabiki na wapenzi kwenda wenyewe viwanjani.
.
Inawezekana serikali ina lengo zuri la kutaka kuona mashabiki na wapenzi wanaziunga mkono timu zao kwenye michuano zinayoshiriki, lakini kwa bahati mbaya ni kamati hizi hizi zimekuwa tatizo la kuzikwamisha timu hizo hata pale wanapokuwa wamebakiza hatua chache wafuzu michuano shiriki.
.
Zimekuwa zikivuruga saikolojia za wachezaji na kibaya zaidi zinaundwa na baadhi ya watu wasiojua mchezo wenyewe na wala hawana maajabu ya kusaidia kuhamasisha timu zifanye vizuri kwa sababu watu kwenda viwanjani au kuziunga mkono timu hizo haiwezi kuwa kitu kama timu haifanyi vyema.
.
Tunaamini serikali na hasa Wizara ya Michezo, ingekuwa ikiunda kamati kwa kushirikisha nyota wa zamani wenye rekodi zao ambao hata wakienda katika kambi ya timu hizo za taifa na kuzungumza na wachezaji zinaweza kuwaongezea nguvu ya kupambana viwanjani kuzibeba timu hizo kama ambavyo England wanafanya kuwahusisha kina David Beckham.
.
Mwaka 2019, iliundwa kamati kama hiyo na kupelekwa Misri kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) na kipi kilichoiletea mafanikio Stars zaidi ya kumaliza michuano bila pointi hata moja, lakini malalamiko yakiwa mengi kutokana na aina ya watu waliotumia fedha za serikali kwenda kwenye fainali hizo.
 
Winga mpya wa Yanga, Augustine Okrah mwenye umri wa miaka 30 jana alipata jeraha la kichwa dakika tatu baada ya kuingia uwanjani na hivyo alishindwa kuendelea na mchezo.
.
Taarifa kutoka Yanga zinaeleza kuwa Okrah anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya kitabibu zaidi kuhakikisha afya yake inakaa sawa.
 
Hahahaha
 
Msemaji Mkuu wa Serikali amesema Serikali ya Tanzania imeanza utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwajengea Waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope Wilayani Hanang Mkoani Manyara jumla ya nyumba 101.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo January 05,2024, Matinyi amesema “Nyumba hizi zinajumuisha nyumba 89 zilizothibitika kupotea baada ya maafa haya ya tarehe 3 Desemba, 2023, pamoja na nyumba 12 ambazo Wataalamu wa Serikali wameshauri zibomolewe na eneo lake lisitumike kwa ajili ya makazi ama shughuli zozote za kiuchumi na kijamii.

“Serikali imetenga ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa makazi mbadala ya kudumu katika shamba la Waret lililopo kwenye eneo la Jeshi la Magereza, kwenye kijiji cha Gidagamowd, kata ya Mogitu, wilayani Hanang. Eneo hilo lipo umbali wa km 4.5 kutoka barabara kuu ya Babati-Singida, na km 21.2 kutoka mji mdogo wa Katesh kuelekea Singida”

“Kazi zilizokamilika hadi sasa ni upimaji wa viwanja na usajili wa ramani ya eneo la ujenzi. Kuna jumla ya viwanja 269 vilivyopimwa ambapo viwanja 226 ni makazi pekee, viwanja 26 ni makazi na biashara na viwanja 17 ni maeneo ya huduma za kijamii kama zahanati 1, eneo la kuzikia 1, kiwanja cha michezo 1, eneo la wazi 1, viwanja vya maeneo ya ibada 3, ofisi ya kitongoji 1, soko 1 na Shule ya Msingi 1”

“Hatua inayofuata ni umilikishaji wa viwanja kwa Waathirika, ukamilishaji wa ubunifu wa ramani za nyumba, gharama na zijengwe na nani lakini mpango ni kufanya kazi kwa mtindo wa operesheni kwa muda wa miezi mitatu”
 
Mbwa aitwaye Cecil anayemilikiwa na Clayton Law na Mkewe Carrie Law ambao ni Wakazi wa Pittsburgh nchini Marekani ameibua gumzo baada ya kuichanachana bahasha iliyokuwa na dola elfu nne za Kimarekani ( USD 4000 ) na kuzitafuna pesa zote.

Wanandoa hao licha ya kupata hasira na hasara ambayo inafikia milioni 10 kwa pesa za Kitanzania, wameendelea kumsifu mbwa huyo kuwa ni mpole na hii ndio mara yake ya kwanza kutafuna pesa zao, kuzichanachana huku wakiamini amemeza zaidi ya dola elfu mbili.

“Cecil alikuwa mbwa mbaya siku ya kwanza tulichukia lakini kwa sasa tunacheka tu tukiwaza hili tukio, zimepita wiki nne tangu tukio litokee na tunashukuru mbwa wetu anaendelea vizuri hajaugua na ameendelea kuwa mbwa mzuri kwetu” ——— wamesema Wanandoa hao.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Immaculate Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu; Zuhra Yunus, imesema kabla ya uteuzi huo, Dk Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu.

“Kwa uteuzo huo, Dk Semesi na anachukua nafasi ya Dk Samuel Mafwenga ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi huu unaanza Januari 5, 2024,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mbali na wadhifa huo, Semesi amewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kipindi kimoja cha mwaka 2015 /2020.

Semesi ni miongoni mwa wabunge waliokuwa na michango mizuri Bungeni na pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya kuchunguza masuala ya kiuchumi na kisheria kuhusu usafirishaji wa makinikia iliyoendeshwa na Mwenyekiti wake Profesa Nehemiah Osoro.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…