Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkazi wa Dar es salaam aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akituhumiwa kutapeli Wananchi wanaopata huduma akijifanya Daktari.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini Mtu huyo akiwa kwenye harakati za kuwatapeli Watu wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Tukio hili limemfanya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Muhimbili Aminiel Aligaesha kutoa rai kwa Watu wote wanaojihusisha na kutapeli Wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama. View attachment 2734208
Mawa katisha sana
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu Cyprian Kasuva kifungo cha miaka 80 jela kwa kosa la kukutwa na makosa matatu, kosa la kwanza kukutwa na nyara za Serikali (kichwa cha Tembo na meno yake), kosa la pili kukutwa na silaha (Magobole matatu) na kosa la tatu kukutwa na risasi 35.

Cyprian(44) Mkazi wa Kalenga Iringa Vijijini inadaiwa alitenda kosa hilo May 09, 2022 katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo akiwa anabanika nyama ya Tembo, Askari wa Wanyama Pori wakafanikiwa kumkamata.

Kosa la kukutwa na kichwa cha Tembo na meno yake hukumu yake ni kifungo cha miaka 30 au faini ya shilingi milioni 348, kosa la kukutwa silaha (Magobole matatu) hukumu yake ni kifungo miaka 25 na kukutwa na risasi 35 hukumu yake ni kifungo miaka 25 na hivyo kufanya jumla ya makosa yote kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 80 ( anaitumikia kwa pamoja )

Kesi hiyo imesomwa na Hakim Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa na ilikuwa na Mashahidi 6 huku ikisimamiwa na Mwendedha mashtaka wa Serikali Barton Mayage, Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Cyprian aliiomba kupunguziwa adhabu kwasababu ni kosa lake la Kwanza na ana Watoto watatu wanamtegemea lakini hata hivyo akahukumiwa miaka 80. View attachment 2734206
Pole yake.
Atakaa jela angalau miaka 10 kisha atapata msamaha wa rais.
Pole sana
 
Mkazi wa Dar es salaam aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akituhumiwa kutapeli Wananchi wanaopata huduma akijifanya Daktari.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini Mtu huyo akiwa kwenye harakati za kuwatapeli Watu wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Tukio hili limemfanya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Muhimbili Aminiel Aligaesha kutoa rai kwa Watu wote wanaojihusisha na kutapeli Wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama. View attachment 2734208
Kwa vyovyote alikuwa anashirikiana na baadhi ya watumishi wa Muhimbili.
 
Mchana mwema
Gulf_1693135377131.jpg
 
Vuguvugu la mapinduzi kwa nchi za Afrika zinazoongea Kifaransa linaendelea. Baada ya Burkina Faso, Mali, Niger, Chad na Guinea, sasa ni zamu ya Gabon. Jeshi la Gabon limetangaza kuifurusha serikali ya Rais Ali Bongo baada ya vurugu zilizotokana na matokeo ya uchaguzi.

Jana Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (CGE) ilitangaza Rais Ali Bongo anayegombea awamu ya 3 amepata kura 64.2% huku mpinzani wake mkuu Profesa Albert Ondo Ossa akipata 30.7%. Kufuatia matokeo hayo wananchi waliingia mtaani wakidai kumefanyika udanganyifu, hali iliyosababisha Jeshi kuingilia kati na kupindua serikali.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi kupitia kituo cha Televisheni cha Gabon 24 imeeleza kuwa Rais Ali Bongo yupo chini ya ulinzi na serikali imevunjwa. Jeshi pia limetangaza kuvunja bunge na Mahakama, na kuunda baraza la uongozi la mpito la kijeshi, litakaloongoza mpaka utakapopatikana utawala wa kiraia.

"Tumevunja bunge, serikali na mahakama. Hakuna mhimili wowote utakaofanya kazi kuanzia sasa. Jeshi litaongoza nchi kwa kipindi cha mpito hadi hali itakapotulia. Tumefanya hivi kulinda watu wetu na amani yetu" imeeleza taarifa ya Jeshi.

Kufurushwa kwa Rais Bongo kunahitimisha miaka 57 ya familia yake kuongoza taifa hilo. Baba yake Mzee Omari Bongo aliongoza Gabon kwa miaka 43 kuanzia mwaka 1966 hadi mwaka 2009 alipofariki. Baada ya kifo chake mwanae Ali Bongo alichukua madaraka na kuongoza kwa miaka 14 kutoka 2009 hadi leo alipopinduliwa.

Familia ya Bongo inashutumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma. Mwaka 2019 ndugu wa Rais Bongo, ambao ni Omar Denis Bongo na Paskalina Bongo walituhumiwa kupokea rushwa ya £85M sawa na TZS Bilioni 230 ili kuisaidia kampuni moja ya Ufaransa kuchimba mafuta nchini Gabon.

Pia Rais Bongo anatuhumiwa kwa "nepotism" na kujaza ndugu zake wengi katika nafasi za juu serikalini wakiwemo watoto wake Malika Bongo, Noureddin Bongo, Jalil Bongo, Bilal Bongo na Jean-Valentin Bongo.

Gabon ni nchi ya 6 barani Afrika kufanya mapinduzi hivi karibuni. Nchi nyingine mbili, Guinea-Bissau na São Tome &Principe pia zilifanya mapinduzi lakini yakazimwa. Nchi zote hizo ni makoloni ya zamani ya Ufaransa. Ufaransa inaishutumu Urusi kuwa nyuma ya mapinduzi hayo.!
Screenshot_20230831_175850_Instagram.jpg
 
Malisa gj

Mabegi yenye noti za Franga pamoja dola za Marekani yamekutwa katika Ikulu ya Rais wa zamani wa Gabon aliyefurushwa madarakani hapo jana, Ali Bongo.

Makachero wanaendelea kuzihesabu lakini bado hazijajulikana thamani yake kwa sababu kila wakikaribia kumaliza wanakutana na furushi jingine la noti. Hawa ndio viongozi wa Afrika wajiitao wazalendo. Halafu yakiwafika wanasema "please make noise" Kiboboru.!!
Screenshot_20230831_180019_Instagram.jpg
 
Moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katika Jiji la Johannesburg, Afrika Kusini limesababisha vifo vya zaidi ya Watu 70 hadi sasa huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la Jiji hilo kubwa la Johannesburg.

@DW_Kiswahili_ imeripoti kuwa Msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha Jiji la Johannesburg, Robert Mulaudzi, amesema moto huo umesababishapia Watu wengine takribani 52 kujeruhiwa huku idadi ya vifo ikihofiwa kuongezeka kwakuwa jitihada ya kutafuta miili ya Watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine zinaendelea.
Screenshot_20230831_180215_Instagram.jpg
 
Nchi ya Krygzstan imetangaza kufungia mtandao wa TikTok baada ya Taasisi moja isiyo ya Kiserikali kuwasilisha ombi kwamba mtandao huo unaathiri ukuaji wa Watoto na kuharibu maadili ya Jamii kwa ujumla.

Uamuzi wa kufungia mtandao huo umetangazwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sera za Vijana.
Screenshot_20230831_180311_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom