Winfred Mueni (28) amefikishwa katika Mahakama ya Makadara jijini Nairobi, akishtakiwa kwa mauaji ya kutokusudia baada ya mpenzi wake Titus Njoroge Kimani (30), kufariki dunia wakati wa tendo la ndoa.
Tukio hilo linadaiwa kutokea nyumbani kwa marehemu katika Mtaa wa Baba Dogo, Ruaraka, jijini humo.
Mtandao wa Taifa leo umeripoti kuwa Mueni anashtakiwa kwa kufupisha maisha ya mpenzi wake Septemba 22, 2023, ambapo inadaiwa kuwa wakiwa katika tendo ndoa, na hasa wakati Kimani anafika kileleni, alipoteza fahamu na kuanguka.
Inadaiwa kuwa kuwa Winfred alijaribu kuokoa maisha ya mpenzi wake kwa kumpeleka hospitali, hata hivyo, baada ya kufika, alielezwa kuwa Kimani amekwishafariki.
Kwa mantiki hiyo, mahakama hiyo imeelezwa kuwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), inamshtaki Winfred, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni āmtu wa mwisho kuonekana na marehemuā kabla ya kifo chake.
View attachment 2813774