Makapuku Forum

Makapuku Forum

AL AHLY MSHINDI WATATU KLABU BINGWA DUNIA
.
FT: URAWA REDS [emoji627] 2-4 AL AHLY [emoji1093]
19’—[emoji460]️ Yasser
25’—[emoji460]️ Tau
43’—[emoji460]️ Kante
54’—[emoji460]️ Scholz (pen)
60’—[emoji460]️ Koizumi (og)
90’—[emoji460]️ Maaloul

Screenshot_20231222_195922_Instagram.jpg
 
Unaambiwa yule Benchikha hacheki kabisa na nyani pale ‘Simba’ inaelezwa jamaa ni noma kwenye kusimamia masuala ya nidhamu! Kwa kifupi ni kwamba mwamba kanyooka hana konakona.
.
Picha linaanza kawaambia wachezaji wote ni sawa, hakuna star, mchezaji mzawa au mgeni wala mchezaji mkongwe. Hakuna aliyejuu ya mwingine wala mwenye haki zaidi kwenye timu.Nimeambiwa kuelekea mechi dhidi ya Kagera Sugar, kuna siku Jean Baleke alichelewa mazoezini, Benchikha akamzuia kuingia uwanjani kuungana na wachezaji waliowahi mapema uwanja wa mazoezi.
.
Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Baleke akatupwa benchi halafu fresh tu. No kelele wala maswali.Kawaambia wachezaji hakuna mtu atacheza kutokana na jina wala mazoea, kila mmoja anapaswa kuonesha uwezo mazoezini na kutekeleza maelekezo. Kwa hiyo wanasimba jiandaeni kwa surprises nyingi sana kutoka kwa Benchikha.
Screenshot_20231222_200148_Instagram.jpg
 
EDO KUMWEMBE: Kuhusu Chama vs Simba?
.
[emoji187] Tatizo la Chama na Simba ni ushahidi halisi wa namna Simba walivyokosea katika madirisha mengi ya usajili kwa miaka mitatu iliyopita....hawakuwahi kuondoa umuhimu wake uliopitiliza klabuni. Alipokuwepo hapo awali,, alipokwenda Morocco, na aliporudi nyayo zake zilisimama juu ya utosi wa Simba.
.
Mwanzoni tu mwa msimu alienda mazoezini, alipoona hakuna maajabu akagoma kwenda Uturuki.

Ameichukua klabu mateka kwa muda mrefu. Usajili bora ungemfanya awe bora lakini ungeondoa umuhimu uliopitiliza.

Kule upande wa pili wameondoka Fei, Mayele na Nabi, wakaondolewa Morrison, Djuma na Bangala lakini bado mwendo mdundo...mpuuzi mmoja aliwahi kusema

‘Mwanamke anaringa zaidi akigundua hauna wanawake wazuri zaidi yake’...huku Afrika hakuna nidhamu kama wewe unajihisi ni ‘Mungu mtu’ klabuni. Uprefesheno tuwaachie akina Messi huko Ulaya ambapo kila mtu anajua yupo chini ya taasisi.“
.
Screenshot_20231222_200251_Instagram.jpg
 
RAIS WA KLABU YA WYDAD ATHLETIC AMEKAMATWA.

Rais Said Naciri wa Wydad Casablanca amekamatwa na mamlaka nchini Morocco kwa makosa kadhaa ikiwemo biashara haramu za dawa za kulevya na utakatishaji fedha, ikumbukwe pia anatuhumiwa kujitwalia mali kwa namna ya unyang’anyi kutokana na madaraka yake kama Mbunge kwenye Baraza la Wawakilishi akiwakilisha jimbo la Casablanca-Anfa.

Ikumbukwe pia alikuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa Wanachama (Ultras) ambao walikuwa wanahitaji ajiuzulu tangu mwezi Novemba, mpaka hivi sasa Mashabiki na Wanachama wengi wameisusia timu yao, wakiwa pia na rungu la FIFA kutofanya usajili.

Huenda baada ya sekeseke hili kundi la Ultra Winners wataanza kuiunga mkono timu yao huku pia mambo mengi yakirejea kwenye hali ya kawaida, Naciri hivi sasa anakumbana na mkono wa sheria.

Taarifa kwa msaada wa mtandao.
Screenshot_20231222_200542_Instagram.jpg
 
Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kenneth Boymanda amesema wamepokea kauli iliyotolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda kuhusu Shirika hilo na tayari wameanza kuyafanyia kazi kikamilifu maelekezo yaliyotolewa.

Akiongea na @AyoTV_, Boymanda amesema “Ndani ya Shirika tunayo sera ya upimaji ufanisi wa kazi kwa Watendaji na kama kuna changamoto za kiutendaji kwa Watumishi wa Shirika hilo, hatua stahiki zinachukuliwa kwa wote ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na ubora unaotakiwa”

“Niwaombe sana Wananchi watuvumilie kwenye kipindi hiki ambacho uzalishaji haukidhi mahitaji, Shirika linafanya kila jitihada kuhakikisha kipindi hiki tunakipita salama wakati tukisubiria mashine ya kwanza katika mradi wa Bwawa la Nyerere”

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam jana pamoja na mambo mengine Makonda alinukuliwa akiwaambia TANESCO “Je maumivu, mzigo na shauku anayoibeba Rais Samia ndio hayohayo Watendaji wa Tanesco wanayabeba ama wanamuachia Mwenyekiti wetu peke yake ? ukiona hadi Rais anavunja bodi maana yake hili suala halivumiliki, tunawauliza Watendaji wa Tanesco mnajiona mnastahili kweli kumuwakilisha Rais Samia ama mnasubiri tenda, anavunja bodi, atengue, ateue....... huku hamumtendei haki Rais Samia, kuna vingine ni uzembe tu, unapokaa ofisini na kutoa maelezo ofisini bila kwenda site mnatengeneza picha tofauti”
Screenshot_20231222_200746_Instagram.jpg
 
Wanandoa 61 wamepeleka maombi ya talaka kwa ajili kuvunja ndoa zao katika Baraza la Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe kwa kipindi cha mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia November hadi December 20 mwaka huu.

@AyoTV_ imezungumza na Mwenyekiti wa Baraza hilo Muhimba Payovela aliyethibitisha kupokea migogoro mingi ya Wanandoa kuliko ya ardhi huku akieleza kuwa sababu kubwa ya Wanandoa wengi kudaiana talaka ni kutoaminiana na wengine kuendekeza tamaa.

“Ndoa 61 kila mmoja anataka kuvunja ndoa yake hakuna anayekuja kusema anataka kusuluhisha bali kila mmoja anasema sitaki tena ndoa” ——— Payovela

Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Makambako wamesema maombi ya talaka kwa Wanandoa yanachangiwa na wengi wao kutoridhika na walichonacho na baadhi ya Wanawake kutaka usawa ndani ya ndoa zao huku wengine wakitaka kuzivunja kutokana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.
Screenshot_20231222_200846_Instagram.jpg
 
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Fransisko ametangaza eneo la Mafinga mkoani Iringa kuwa Jimbo Jipya Katoliki na kumteua Padri Vincent Mwagala wa Jimbo Katoliki la Iringa kuwa askofu wa kwanza wa jimbo hilo jipya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) iliyosainiwa na katibu wake mkuu, Padri Charles Kitima, leo Desemba 22, 2023, uteuzi huo unaanza leo huku jimbo hilo likipewa jina katika lugha ya kilatini ‘Mafingens’.

Askofu Mteule Mwagala amezaliwa Desemba 11, 1973 huko Makungu Wilaya ya Mufindi, Jimbo Katoliki la Iringa.

Baada ya masomo ya upadri, alipewa daraja takatifu la upadri Julai 11, 2007 jimboni Iringa na kuhudumu katika nafasi tofauti za utume nchini Italia na jimboni Iringa.

Screenshot_20231222_201011_Instagram.jpg
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limelazimika kutumia mabasi kuwasafirisha abiria zaidi ya 200 waliokwama jijini Arusha kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye kichwa cha treni.

Abiria hao waliokuwa wasafiri jana kwenda Dar es Salaam, wamesafirishwa kwa mabasi leo hadi kituo cha treni cha Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa abiria waliokwama Moshi ambao walikuwa wakienda Arusha wamesafirishwa kwa mabasi madogo ya kukodi.

Abiria waliokuwa wamekwama Arusha walilazimika kulala stesheni.

Screenshot_20231222_201129_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom