Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20240109_062458_Chrome.jpg
Screenshot_20240109_062519_Chrome.jpg
 
Mabingwa watetezi Mlandege FC wametinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitoa APR ya Rwanda kwa mikwaju ya penati 4-2.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa Uwanja wa News Amaan Complex leo Jumanne, Januari 9, 2024 ulimalizika dakika 90 kwa suluhu.

Mlandege inasubiri mshindi baina ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate utakaochezwa kesho uwanja huo huo.

FT: Mlandege FC 0-0 APR FC (Pen: 4-2)

Screenshot_20240110_063821_InstaPro%20.jpg
 
Mtu mmoja ambaye jina lake halijatajwa amefariki dunia na wengine 19 wanaendelea kutibiwa baada ya kugundulika kuugua ugonjwa wa kipindupindu ulioibuka mkoani Mwanza.

Taarifa hiyo inakuja zikiwa zimepita siku nne tangu watu watano waripotiwe kuugua ugonjwa huo uliolipuka katika eneo la mji mdogo wa Kagongwa mkoani Shinyanga huku 13 wakilazwa na 452 waliochangama nao wakifuatiliwa.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo, Jumanne Januari 9,2024, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Rachel Kasanda amesema aliyefariki ni mwanamme aliyetoka katika sherehe iliyofanyika kwa mmoja wa wake zake anayeishi Dutwa mkoani Simiyu.

Kasanda amesema marehemu baada ya kutoka Dutwa alirejea kwa mwanamke mwingine anayeishi wilayani Magu akiwa na dalili za kuharisha na kutapika na hali yake ilipobadilika alipelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani humo kisha kufariki akiwa mapokezi.

Kuhusu Nyamagana na Ilemela, Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk Pima Sebastian amesema watu saba wamethibitika kuugua ugonjwa huo huku 18 wakiwemo ndugu na waliokutana nao wakifanyiwa ufuatiliaji.

Amesema wagonjwa wawili tayari wameruhusiwa, baada ya kupatiwa matibabu na hali zao za afya kuimarika huku akitahadharisha watu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Screenshot_20240110_063925_InstaPro%20.jpg
 
Mabingwa watetezi Mlandege FC wametinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitoa APR ya Rwanda kwa mikwaju ya penati 4-2.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa Uwanja wa News Amaan Complex leo Jumanne, Januari 9, 2024 ulimalizika dakika 90 kwa suluhu.

Mlandege inasubiri mshindi baina ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate utakaochezwa kesho uwanja huo huo.

FT: Mlandege FC 0-0 APR FC (Pen: 4-2)

View attachment 2867019
Dah wajomba zangu ,wametolewa kumbe
 
Back
Top Bottom