Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Jaji Mkuu wa zamani nchini Liberia, Gloria Musu Scott pamoja na watu wengine watatu wa familia yake, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kutekeleza mauaji.
Tovuti ya RFI imeripoti kuwa, wanne hao walikamatwa na kufunguliwa mashtaka Juni mwaka jana kwa kuhusishwa na kifo cha Charlotte Musu, ambaye ni mpwa wa jaji huyo.
Charlotte aliuawa Februari mwaka jana, katika makazi ya Scott, mjini Brewerville, Kaskazini Magharibi wa Liberia.
Jaji Mkuu huyo wa zamani amekuwa akisisitiza kwamba watu wasiojulikana walivamia makazi yake ambapo walitekeleza mauaji ya mpwa wake.
Baada ya miezi minne ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Mahakamani katika mji mkuu wa Monrovia, mwezi uliopita walipatikana na kosa la kumuua Charlotte japo wamekuwa wakikana mashtaka hayo. Hata hivyo, mahakama imesema ilipata ushahidi wa kutosha.
Scott alihudumu katika nafasi ya Jaji Mkuu wa Liberia kati ya mwaka 1997 hadi 2003.