Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣...ndani ya mchuma wa mswidi kitu Scania, jiko ndani kitanda ndani na ka-tv ka kizushi kameunganishwa na satelite, mawimbi hayakosekani, barabarani unapata kipupwe cha bahari ya Hindi. Na umeshatembea masaa manane unastahili kupumzika kwa nusu saa, mpira umeisha na wamegongwa tena.
Goma unaliamsha tena maana wimbo wa Kasongo mbona yeyooo ndo unaanza hapa. Unapunguza mwendo kumpa high five traffic officer, mdada wa nguvu ambaye kakukumbusha tena msimu wa sikukuu anataka kuja Mtwara kuogelea ufukwe wa Shangani. Unatabasamu huku unaitafuta Mnazi Mmoja uingie zako Lindi maana hapo ndipo safari itakomea.
Karibuni Lindi msimu huu wa sikukuu