Makapuku Forum

Makapuku Forum

.
 

Attachments

  • IMG_6199.jpeg
    IMG_6199.jpeg
    1.2 MB · Views: 2
Juma la kwanza katika mwezi wa mwisho wa 2024. Siku zimekimbia na kwa baadhi yetu tunaopata likizo kipindi cha June, tunaona ni kama jana tu tulikuwa likizo, na hatujajipanga kwa ajili ya likizo nyingine ya 2025, Mungu tupe maisha. Naam, ndugu yenu ni kama mwanafunzi au mwalimu, likizo zangu ni pale shule zinapokuwa zimefungwa (shule za wengi).

Kwa wadau wenye vibarua/kazi tunajua tunafanya kazi na watu wa silika tofauti na hapa leo nataka kukuonesha tabia ambazo huoneshwa na mtu/watu ambao hujiona wa muhimu kuliko uhalisia. Mtu wa namna hii huonesha tabia kadhaa bila yeye kujijua na hivyo huathiri mahusiano yake na watu wengine.
Kumbuka, kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha kiburi na kujiamini, thamani yako halisi na kujipandisha mabega na hapa ndipo hoja ya mmoja kusisitiza mafanikio binafsi hata pasipotakikana. Hakuna ubaya kueleza mafanikio yako, lakini haileti maana na ni kiburi kukaa unayaelezea kila siku kwa watu wale wale kwenye matukio yaleyale. Muhimu, hatuwezi kuishi kwenye jamii ambayo mmoja ni kujisifu tu bila kutambua mafanikio ya wengine.

Jipe nafasi ya kusikiliza zaidi msimu huu wa sikukuu kuliko kusikilizwa.

Nitaandika tena maana sijachoka kukutakia wakati mzuri katika msimu huu wa sikukuu.

MALCOM LUMUMBA kitambo sana mdau, kila wakati ni furaha kukuona wewe na wadau wote humu Jukwaani
 
Back
Top Bottom