Makarani wa vyama vyote na wahudumu wa IEBC waanza kupitia fomu zote

Makarani wa vyama vyote na wahudumu wa IEBC waanza kupitia fomu zote

Ndio njia sahihi ya kuepuka ugomvi na kuhakikisha mshindi anakubalika, yaani fomu zote zimekusaywa na makarani wa vyama vyote wamealikwa kushirikiana kwa pamoja katika kupitia takwimu baada ya takwimu, herufi baada ya herufi na kukokotoa mahesabu yote kwa pamoja hadi kieleweke.
Walioshuku demokrasia yetu, muda muafaka ndio huu hapa wa majirani kujifunza kitu.
Siutilii shaka kamwe uzalendo wa Wafula na IECB, kwa kweli ktk hiki IECB ni mfano wa kuigwa. Wengine huku kwenye Tume zetu wanalazimisha tu mambo, hakuna uwazi wa aina ya IECB ambao wanaonyesha sio tu kutenda haki bali kuionyesha dunia kuwa uchaguzi umeefanyika kwa uhuru na mshindi atapatikana kwa haki.

Vv
 
Lakini sisi hatuchinjani wala kupigana na mitutu sisi maji ya kuwasha na Bomu za machozi tu siku moja yamekwisha
Hayo yote yanatokea kwa Kuwa TZ ni nchi ya 9 duniani kwa watu wake kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri (Low IQ) hivyo chochote kinachofanyika wao ni sawa tu kwani ubongo auna uwezo wa kujitambua.
 
Mudavada alinukuliwa akisema kuna mtu ameingia kwa kutumia akaunti Msando,upo hapo hapo?walijuaje kama akaunti ya msando imekua logged in?
Katika masuala ya IT kujua hilo sio tatizo ni kitu ambacho ni cha kawaida, isipokuwa hauwezi kuingia kuvuruga tamwimu kwani inakuwa protected.
 
Hata marekani Warusi walifanya udukuzi kulingana na maneno ya Hilary na Obama.Trump akashinda maisha yanaendelea!
Eti Maisha yanaendelea haufuatilii habari kujua Trump anavyochunguzwa?
 
Tanzania hata mtu anayejumlisha kura zake anakamatwa
 
Nadhani tume ya uchaguzi ya Marekani itakuja kujifunza jinsi Tume huru inavyopaswa kuwa
 
Akabeba ushahidi gani wewe MTU mzima mbona mwongo sana, unafaidika nini kudanganya. Sema huo ushahidi walioubeba, wakati replica ya docs za 34b ndio zilitumika kuwaprove kwamba wameshindwa. M

Mbona povu wakati sote tulikua tunaona matukio, hukumbuki Lowassa akizuiwa kuingia kwenye ofisi za NEC, alipojaribu kwenda plae kuzuia upeperushaji wa matokeo akisema ana ushahidi aliotaka kuwaonysha.
Anyway, tubaki kwenye hoja ya uzi huu, hatuongelei vya Tanzania.

Kenya washika dau wote wamealikwa, mawakala wa upinzani, wana habari, wachunguzi wa kimataifa n.k. Wapitie fomu zote moja baada ya nyingine. Binafsi ningependa Uhuru ashinde, lakini ushindi wake usiwe wa uchakachuaji ambao utatuletea matatizo, aisei nina biashara zangu na familia, hivyo urais wowote ule usiwe sababu ya kupoteza haya yote niliyoyafanyia kazi.

Kama ikitokea Raila ndiye mshindi, haya basi itabidi nimpokee kama rais wangu japo nitaumia komoyo moyo lakini ndio maisha yalivyo. Cha msingi yeye ni Mkenya na nina uhakika hana nia mbaya na nchi na atatutawala ipasavyo.
 
Back
Top Bottom