Makarani wa vyama vyote na wahudumu wa IEBC waanza kupitia fomu zote

Makarani wa vyama vyote na wahudumu wa IEBC waanza kupitia fomu zote

Duh maombi tu maana hawa jamaa ni kama wamejiandaa pachimbike, leo hii kuna maeneo ambayo ya mbali na pamoja na raslimali walizo nazo IEBC, makaratasi hayajafika yote, sasa hao NASA wameyakusanya kivipi aisei.
Cha ajabu wanasema wameona matokeo kwenye mtandao wa tume,kama hawajadukua wamepata wapi hayo matokeo.
Kila la heri mmalize salama,naanza kuogopa,lakini nimepata funzo kua katiba wala tume sio suluhisho
 
wanaosupport kuwa Kenya kuna Demokrasia zaidi ya Tanzania wanashangaza sana,Wakenya kila kitu cha msingi wanapata through Protesting watu lazima waumie kila siku,hii tume ya sasa imeweka through Protesting na bado ni mbovu kuliko halafu bado tunaiita hiyo ina Demokrasi??
Hiyo ndiyo tofauti kubwa sana
Misukule ya Tz haiwezi kusukuma agenda Mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Lowassa alivyopambana kulalamika kwamba kura zake zimeibiwa, akabeba ushahidi na kupeleka kwenye majengo ya tume, lakini alipuuziwa mbali na mshndi akatangazwa. Hilo tumewashinda kwa mbali maana kwetu sisi inabidi vyama vyote vihusishwe, hesabu zipigwe taratibu kiasi kwamba hakuna atakayebaki akilalamika.
Lakini sisi hatuchinjani wala kupigana na mitutu sisi maji ya kuwasha na Bomu za machozi tu siku moja yamekwisha
 
Niliona mtu Tviini kama John Kelly yule wa Obama au macho yangu tu
 
Kilichofanyika KE mpaka sasa imedhihirishia ulimwengu kuwa wako matured enough katika demokrasia
 
Roma ni bora angeacha mziki. Nimesikiliza huo wimbo haujanivutia kabisa. Binafsi nilikuwa shabiki wa Roma ila kama kwa sasa staili ndio hii, mimi sio shabiki wake atafute wengine
Unaweza kuwa sio mlengwa wa wimbo huo.
Ndio njia sahihi ya kuepuka ugomvi na kuhakikisha mshindi anakubalika, yaani fomu zote zimekusaywa na makarani wa vyama vyote wamealikwa kushirikiana kwa pamoja katika kupitia takwimu baada ya takwimu, herufi baada ya herufi na kukokotoa mahesabu yote kwa pamoja hadi kieleweke.
Walioshuku demokrasia yetu, muda muafaka ndio huu hapa wa majirani kujifunza kitu.
Unadhani mtamaliza ? Bila ugomvi hapo. Ninashaka sana
 
nasikia jecha na lubuva wapo Nai,muwe makini
BTW japo sio kwa 100% ila uchaguzi umeonekana standard kwa levo ya kiafrika mashariki
Mama yangu Jecha tena !!!!!!!!!!!
Duuu bado professor sasa !!!!!
tapatalk_1501353203041.jpeg
 
Hata marekani Warusi walifanya udukuzi kulingana na maneno ya Hilary na Obama.Trump akashinda maisha yanaendelea!
 
Hata marekani Warusi walifanya udukuzi kulingana na maneno ya Hilary na Obama.Trump akashinda maisha yanaendelea!

Waligundua baadae sana, uhuru kashikwa peupe, tulia watu wanahesabu kwa fomu shida yako kama ni maisha yapo tu hata baada ya kufa!!!! Tatizo linakuja aina ya maisha!!!!
 
Nakumbuka Lowassa alivyopambana kulalamika kwamba kura zake zimeibiwa, akabeba ushahidi na kupeleka kwenye majengo ya tume, lakini alipuuziwa mbali na mshndi akatangazwa. Hilo tumewashinda kwa mbali maana kwetu sisi inabidi vyama vyote vihusishwe, hesabu zipigwe taratibu kiasi kwamba hakuna atakayebaki akilalamika.
Akabeba ushahidi gani wewe MTU mzima mbona mwongo sana, unafaidika nini kudanganya. Sema huo ushahidi walioubeba, wakati replica ya docs za 34b ndio zilitumika kuwaprove kwamba wameshindwa. M
 
  • Thanks
Reactions: KGM
Cha ajabu wanasema wameona matokeo kwenye mtandao wa tume,kama hawajadukua wamepata wapi hayo matokeo.
Kila la heri mmalize salama,naanza kuogopa,lakini nimepata funzo kua katiba wala tume sio suluhisho
Hivi wewe mbona unaonyesha jinsi ulivyomweupe kichwani? Mtandao wa tume ya uchaguzi ya kenya ni Website ambayo wanaweka matokeo ya uchaguzi ili kila mtu aone. Sasa wewe ulitaka NASA wasiangalie kwenye hiyo Website? NASA Kujua kwamba servers za tume ya uchaguzi zimeingiliwa ni kutokana kutokana na baadhi ya matokeo yaliyokuwa yanawekwa kwenye hiyo Website kuwa tofauti na ilivyo kwenye Form za matokeo. Hivyo hicho pekee ni kuashiria kikubwa sana kwamba kuna either tatizo kwenye mfumo/servers au mkakati wa kupendelea upande mmoja!
Mama yangu Jecha tena !!!!!!!!!!!
Duuu bado professor sasa !!!!!View attachment 562931

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sisi Waafrika tulishazoea kuiba na fujo kwenye chaguzi. ndiyo maana ICC walikuwa wanajaa maviongozi ya Kiafrika na ndiyo maana hayaitaki mahakama ya icc kwa sababu bado hayaamini kwenye kushindwa kwenye chaguzi. Why only Afrika each and every time? We still have a long way to go as far as democracy and fair elections are concerned

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh maombi tu maana hawa jamaa ni kama wamejiandaa pachimbike, leo hii kuna maeneo ambayo ya mbali na pamoja na raslimali walizo nazo IEBC, makaratasi hayajafika yote, sasa hao NASA wameyakusanya kivipi aisei.
Kazi ipo nginjanginja hadi ikullu!
 
Waligundua baadae sana, uhuru kashikwa peupe, tulia watu wanahesabu kwa fomu shida yako kama ni maisha yapo tu hata baada ya kufa!!!! Tatizo linakuja aina ya maisha!!!!
Waluo a.k.a wasukuma mna matatizo sana.Kisa cha kutangaza matokea kabla ya tume ?Observers:EU,AU,CW,Hata John Kerry,alisema uchaguzi ulikuwa huru na uwazi.Hao wote wana imani na tume.Raila akubali matokeo akishindwa.Kuleta ubishi dunia nzima inamshangaa!
 
Safari hii mauaji yakitokea,ICC haiwezi muacha Raila salama.Manake anachochea vurugu!
 
NASA Kujua kwamba servers za tume ya uchaguzi zimeingiliwa ni kutokana kutokana na baadhi ya matokeo yaliyokuwa yanawekwa kwenye hiyo Website kuwa tofauti na ilivyo kwenye Form za matokeo. Hivyo hicho pekee ni kuashiria kikubwa sana kwamba kuna either tatizo kwenye mfumo/servers au mkakati wa kupendelea upande mmoja!
Mudavada alinukuliwa akisema kuna mtu ameingia kwa kutumia akaunti Msando,upo hapo hapo?walijuaje kama akaunti ya msando imekua logged in?
 
Faulo za uchaguzi zipo kila sehemu duniani ni ishu ya hesabu tu hata hao wakenya hizo karatasi za makarani zishachezeshwa tayari.
 
Back
Top Bottom