Naomba utaje nini hicho mumetuzidi overall, kumbuka nyie hata pale Zanzibar ilibidi mtishiwe kunyimwa misaada. Kwetu kila kitu kinafanywa above board and as per the rule of law. Kwa kifupi demikrasia ni mnyama asiyeeleweka, unaweza ukatutuhumu kwamba tunapiga kura kwa misingi ya ukabila, pamoja na kwamba hata mimi hilo hunikera lakii ndio demokrasia yenyewe hiyo, kwamba kila mtu ana uhuru wa kutumia kigezo anachotaka wakati anamchagua kiongozi.
Kama jinsi kwenu mnatumia uchama na ukanda, kwa mfano nikiwa hapo Bongo mwaka wa 2015, niliona jamaa mitaani wanashabikia CCM kwa povu halafu baadaye wanaomba wanunuliwe chai na hao wa UKAWA, eti kwamba wamefulia.
Sisi hapa tumehakikisha kila kitu kinafuata utaratibu wa sheria, kura zimepeperushwa kama sheria inavyosema na kama NASA walivyoaomba mahakama iamuru. Baada ya hapo wameitwa mawakala wa vyama vyote, wana habari na washikadau wote wamekusanyika kuhesabu na kuhakiki kila fomu neno kwa neno, herufi kwa herufi, yaani zaidi ya hapo hamna kingine ila kutangaza mshindi.
Wachunguzi wote wa kutokea mataifa mbali mbali zikiwemo nchi za Kiafrika na Ulaya wote wamekubali kila kitu kimefanywa ipasavyo.