Mbona hili jambo la mahakama ya Kadhi linakuzwa kuliko lipasavyo. Mahakama za hivi ( za kiislamu au dini nyinginezo ) ziko nchi nyingi na sinarahisisha sana watu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya kisheria. Hizi ni kama vyombo vya upatanishi au ufumbuzi. Kwanza hazihukumu mtu ambaye hataki kuhukumiwa nazo, hazihukumu watu wa dini au mila nyingine tofauti nazo. zinarahisisha na kupunguza gharama za mahakama sababu waumini wote watakubali uamuzi bila mapingamizi. Na mahaka hizi zaidi sinashughlikia kesi za kifamilia kama urithi, kuachika, haki za malezi n.k. Hazijihusishi na kesi za jinai.