Kingdan
Member
- May 5, 2020
- 61
- 49
Nchi haiendeshwi kwa kwa idadi ya watendaji bali kwa Mipango na Mikakati ya kukuza Maendeleo ya watu na vitu...Panua ubongo wako kidogo. Tanzania tatizo kubwa siyo fedha ila ni matumizi. Matumizi yasiyo ya lazima na ufisadi ndiyo tanuru linalochoma fedha zetu. Kabla hawajaingia kwenye kumtoza mwananchi kodi mara mbili au hata tatu kwa kitu kile kile ingebidi kwanza wapunguze utitiri wa viongozi wasio na umuhimu wowote na malipo ya anasa. 1. Wabunge wapunguzwe kabisa kwani wengi hawana kazi yoyote. Watu kama ma-DC, maafisa mipango etc waondolewe na ngazi za wilaya na mikoa wabaki viongozi wachache. Mawaziri na makatibu wapunguzwe kabisa. Ununuzi wa magari ufanywe kulingana na hali halisi na siyo kununua magari ya kifahari. Viongozi wasafiri kwenye madaraja ya kawaida na kulala kwenye hotel za kawaida isipokuwa wale viongozi wakuu. Vikao vya kupiga fedha ambavyo Magufuli alikuwa amevipunguza kabisa vimerudi kwa kasi na ufisadi kwa ujumla na pia ukwepaji kodi. Njia za kupata fedha ziko nyingi na siyo kukimbilia kuwakamua wananchi.
Tatizo letu ni kwamba mambo yanaamriwa na wawakilishi wetu(Wabunge) bila sisi kushirikishwa...
In short hakuna uwazi na utoaji wa mawazo kwa wananchi bali kuna maamuzi na maelekezo kutoka kwa Viongozi kwenda kwa wananchi tu...
i.e Top down approach ndo inatuumiza.