Makazi ya FFU Ukonga yaangaliwe upya, yamechakaa sana

Makazi ya FFU Ukonga yaangaliwe upya, yamechakaa sana

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Jana nilifanikiwa kupita maeneo ya makazi ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) pale Ukonga, Dar Es Salaam.

Ni makazi duni sana, yamechakaa, hayastahili kukaliwa kwa sasa! Japo sijawahi kuwakubali askari, lakini kama wanajitahidi kulitumikia Taifa, kwanini Serikali isiwaangalie kwa jicho la pekee?

Zile nyumba pale hazifai kabisa ni udhalilishaji kwa wapiganaji wetu ambao wamejitolea maisha yao kwajili ya taifa. Waziri Simbachawene hebu liangalie hili kwa jicho la upekee!

Nawasilisha.

761D4D12-533C-4868-A4E4-D59920A91B18.jpeg

1D3C0C10-2241-4259-B605-E99DDCCB5156.jpeg

081B7A0E-D00A-4C61-A117-AC378C4EADF4.jpeg

32183ED4-5342-4791-98FA-930CE152FE73.jpeg
 
Labda wanatakiwa wakae mazingira magumu ili wawe na hasira , roho ngumu ili pale wanapohitajika wanawashughulikia watu kisawasawa...hawa jamaa waliwahi kunishughulikia kipindi nipo chuo.

Nakumbuka nilichapwa ngumi ya kifua halafu nikasikia kitu kigumu kinapiga mgongoni nikakata network, nakumbuka ilikuwa jumatano mida ya saa nane mchana nilijikuta hospitali ijumaa nimezungukwa na ndugu jamaa na marafiki........sijui walifanyaje nikatoka mikononi mwao wanasema wasingepata taarifa mapema ndio basi tena💀
 
Hawa jamaa wanatumiwa tu ila nchi haiwajali hata wenyewe nawasikia wakilalamikia juu ya hilo.Wanasema stahiki zao hawazipati.

Nachomshukuru MUNGU sijawahi ipenda hii kazi.[emoji1][emoji1][emoji23]
Mkuu kwani ulifeli kidato cha 4 mpk hukuipenda iyo kazi! Mana niliwasikia wenyewe wanasema hilo jambo[emoji23] eni wei utani tu[emoji13] tupambane tujenge za kwetu tusipende vya bure
 
Mkuu kwani ulifeli kidato cha 4 mpk hukuipenda iyo kazi! Mana niliwasikia wenyewe wanasema hilo jambo[emoji23] eni wei utani tu[emoji13] tupambane tujenge za kwetu tusipende vya bure
Utani tu ila kule kuna wasomi wengi.[emoji1]
 
Back
Top Bottom