Jana nilifanikiwa kupita maeneo ya makazi ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) pale Ukonga, Dar Es Salaam.
Ni makazi duni sana, yamechakaa, hayastahili kukaliwa kwa sasa! Japo sijawahi kuwakubali askari, lakini kama wanajitahidi kulitumikia Taifa, kwanini Serikali isiwaangalie kwa jicho la pekee?
Zile nyumba pale hazifai kabisa ni udhalilishaji kwa wapiganaji wetu ambao wamejitolea maisha yao kwajili ya taifa. Waziri Simbachawene hebu liangalie hili kwa jicho la upekee!
Nawasilisha.
View attachment 1830116
View attachment 1830122
View attachment 1830123
View attachment 1830124