Makazi ya Mbowe huko Machame yatufunze kujitegemea siyo kuiba mali za umma kama wafanyavyo wanasiasa wengi nchini

Hachukui Ruzuku serikalini?
 
Tofauti ya Mbowe na viongozi wengi wa chama tawala, Mbowe anasimamia biashara zake mwenyewe, analipa kodi zote muhimu na anajiendesha kwa kuzingatia sheria za nchi.[emoji419][emoji375]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wana nyumba za maana Dubai, UK na States wanakucheki tu.
 
Tukiacha chuki za kisiasa nyumba kama hizi huko mkoani kwetu ni za kawaida sana....

Mbowe na mzee mengi ni wajomba kabisa...wazee wao wameoleana...na hiyo familia ya kina mbowe ina hela miaka mingi sana...

Kuna kitu kwenye kila familia ya kitajiri kipo na ni siri mara nyingi ila ipo wazi..ni hivi kwenye utajiri mtoto mwenye akili ndio hukabidhiwa mali nyingi...ili aziendeleze...! Mbowe ana ndugu ila yeye ndio alikua na code zote na hakuzichezea!

Angalia...Dewji,Subash na wengineo...ila sasa kama mlilelewa kwa kupendana na wote mmeenda shule wote mtakua matajiri kabisa mfano hai ni familia ya kina ...

SHOO....!

Kaka mkubwa alikua tajiri Mkubwa shinyanga!
Anaefuata ni Harold nae ni tajiri wa kutupwa kanda ya kaskazini...HARSHO

Maskini kabisa ni mdogo wao Hillary mwenye Hill water na viwanda vya vyakula vya kuku

So mkiwezeshana mtatoka wote tatizo ni kwamba wakati mwingine kunakua na mmoja au wawili hawabebeki na hapa ndio lawama inakuja...!

Rejea uzi wangu wa mda kidogo utakufungua macho...usisite kulike ukijifunza kitu..siasa tuiweke kando...!

 
Wachaga huwa hawasahau kujenga kwao kamweeee...

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…