Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Hapa Ubungo, Kisiwani, Wananchi tupo katika hali ngumu sana, maisha yamebadilika kisa Mto Gide, ambao kwa miaka mingi umekuwa ni chanzo cha wasiwasi mkubwa na umekuwa tishio kwa makazi yetu. Nyumba nyingi zimebomoka na kila mvua inaponyesha, hali inazidi kuwa mbaya.
Hadi sasa zaidi ya Wananchi 500 waishio Ubungo, Kisiwani wapo (Dar es Salaam) katika hatari ya kubomokewa nyumba zao kutokana na kuongezeka kwa kingo za Mto Gide unaosafirisha maji yake kutoka Mbezi kuelekea Mto Msimbazi.
Mpaka sasa inadaiwa nyumba za Wananchi zaidi ya 40 zimeanguka (kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo), zikiwemo za majirani zetu na hata Msikiti ambao tulikuwa tunategemea kwa ibada. Tumeshuhudia baadhi ya familia zetu zimebaki bila makazi na wengine kupoteza Maisha. Kila siku, tunahofia kuwa nyumba zetu zitafuata.
Tumefanya kila jitihada kuhakikisha tunabaki salama, wengine wamejaribu hata kujenga kingo za muda kwa kutumia matairi, kwa kuwekeza zaidi ya milioni mbili, lakini maji ya mto yameendelea kushinda juhudi zetu.
Kila siku, tunajua kuna hatari ya nyumba nyingine kubomoka, na bado suluhisho la kudumu halijapatikana.
Wananchi kadhaa walilazimika kuhama eneo hilo ambapo wahanga waliahidiwa kipindi cha kampeni za uchaguzi uliopita na Mbunge wetu wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo kupewa viwanja ahadi ambayo bado haijatimizwa mpaka sasa.
Wito wetu sisi Wananchi wa Ubungo, Kisiwani kwa Serikali, tunaomba itujengee mifereji ya kusafirisha maji ya mvua kutoka barabara kuu ambayo itakuwa ikimwaga maji kwenye mto huo moja kwa moja kuliko hali ilivyo sasa ambapo maji yanapita popote yanapopata njia ya kupita.
Mfano, katika Mto Ng’ombe kuna kingo zimejengwa ambazo zinasaidia mwelekeo wa maji hasa yanapokuwa mengi mfano wakati wa mvua, bila kufanyika kwa jambo hilo wote tutaondoka kwa kukosa makazi.
Tunajua kwamba iwapo kingo hizi zitajengwa, zitasaidia sio tu kuokoa makazi yetu, bali pia kutengeneza kivuko kitakachorahisisha maisha yetu ya kila siku, hasa kwa Watoto wanaovuka kwenda shule na sisi tunaotafuta huduma za kijamii kutoka Ubungo Kisiwani kuvuka Riverside.
Hadi sasa, matumaini yetu yamebaki kwenye hatua ambazo tunatumaini Serikali itachukua haraka, kabla hali haijawa mbaya zaidi. Tunataka tuishi kwa amani tena, bila hofu ya kupoteza nyumba zetu na maisha yetu.